Recent

JIFUNZE MAMBO MBALIMBALI YATAKAYOKUPA MAARIFA NA UJUZI MAISHANI

Wednesday, 3 August 2016

Zitto Kabwe: Sababu zangu kwanini Naunga mkono MO kuwekeza Simba ila asipewe 51%


20bn tshs endowment fund for Simba SC ni moja ya pendekezo bora zaidi kutolewa na Mwanamichezo nchini kwetu. Mohamed Dewji anapendekeza kuwa yeye atatoa tshs 20bn na kuziweka kwenye Endowment Fund kisha riba kutumika kuendesha Club. Tutakuwa na club matata sana nchini. Vyuo vikuu vikubwa duniani Kama Harvard vinaendeshwa kwa Mfumo huu anaopendekeza MO. Tukiwa na usimamizi mzuri wa Fedha tutakuwa timu bora kabisa na tutaweza hata kuwa na academy ya Simba Kama ilivyo kwa club kubwa duniani.

Hata hivyo, nashauri kwenye muundo wa umiliki, mtu mmoja asiwe na Hisa zaidi ya 40%. Ushauri wangu ni mgawanyo ufuatao;

- Mwekezaji ( MO ) 40% ( mkataba wake wa uwekezaji uonyeshe kuwa kwa kupewa Hisa hizi atafungua endowment fund ya thamani ya tshs 20bn na atakuwa na uhuru wa kuteua trustees wa Fund hiyo. Mwekezaji atakuwa na uhuru wa kuifunga fund iwapo asiporidhishwa na matumizi Fedha zinazotokana na Endowment Fund ).

- Wanachama wote wa Simba wagawiwe sawa 40% ( kuwe na cut off ya siku ya mwisho Mwanachama kujiunga kuweza kufaidika na kugawiwa Hisa hizo. Hisa za Simba SC zikishaorodheshwa kwenye soko la Hisa, Mwanachama atakuwa na uhuru wa kuuza Hisa zake freely.

- 20% ya Hisa ziorodheshwe kwenye Soko la Hisa la Dar Es Salaam kwa ajili ya 1) kuvutia wawekezaji wengine 2) kukuza mtaji wa Kampuni 3) kuwezesha uwazi kwenye uendeshaji wa kampuni kwani Wanachama wote watakuwa wanajua kila kinachoendelea kwenye kampuni na club kwa sababu soko la Hisa Lina ' disclosure rules '.

Kwanini MO asiwe na 51%? Sio MO tu, Memarts za Simba ziwe wazi kwamba hakuna mtu mmoja au kampuni moja au taasisi yeyote moja itakayoruhusiwa kuwa na zaidi ya 40% ya Hisa za kampuni. Hii itamfanya MO au mwekezaji mwingine yeyote kuhakikisha anatafuta 11% zaidi ili kupitisha maamuzi. Kuna hatari ya kumpa mtu mmoja uwezo wa kufanya maamuzi peke yake. Lazima kumfanya ashawishi japo 11% ya wenye Hisa ili kuboresha maamuzi. Leo ni MO anaipenda Simba, kesho unaweza kuwa na mtu asiye MO. Nadhani 40% ni kiwango cha kutosha kwa Mwekezaji.

Nashauri wana Simba tusicheleweshe haya MABADILIKO. Tufanye sasa hivi ili msimu huu unaoanza tuwe na timu imara yenye uhakika wa kushiriki Premier League. Mpango wa MO wa Endowment Fund ni Mpango bora na tusipoteze nafasi hii.

0 comments:

Post a Comment