Sunday, 21 August 2016
Je, ni kweli Rwanda iko salama toka kumalizika kwa mauaji ya Kimbari 1994?
Kumekuwa na mijadala mingi juu ya kile kinachoitwa "Kustawi kwa Rwanda katika medani za kimataifa kimaendeleo" kutokana na hii dhana nimevutika kuandika makala hii juu ya taifa hili dogo lenye kusifika kwa usafi na ustarabu Afrika maahaliki. Binafis naifahamu Rwanda kwani katika hii ziara yangu nimejifunza Mengi sana ikiwa ni pamoja na kujionea namna hali ilivyo na inavyo endelea Rwanda. Japo kuwa hii si mara yangu ya kwanza kuizuru Rwanda lakini ziara yangu nchini Rwanda kwa awamu hii ilioanza Tarehe 27/6/2016 mpaka 22/7/2016 imekuwa ya pekee kwani nimejifunza mengi sana kuanzia mpakani mwa Rwanda na Tanzania Rusumo mpaka mpakani mwa Rwanda na Burundi Kanyaru-Hutu na mpakani mwa Rwanda na Uganda Katuna(Gatuna) pamoja na kwenye miji mikubwa kama Kigar, mji wa Musanze(Ruengeri), mji wa Rubavu(Gisenyi), mji wa Kayonza na mji wa Rusizi.
Nimeona nisiwe mchoyo wa kuelimisha kwa kile nilichojifunza Rwanda kwa maana hata Papa Gregor wa Roma mwaka 1565 AD aliwahi kuyataja mambo matano ambayo Wakatoliki huyaita "Mizizi ya dahambi" moja ya mambo hayo ni (i)uchoyo (ii)Uvivu (iii)Uadilifu (iv)Ulafi na (v)Roho mbaya. Sasa binafsi nimeona nisije kuwa mwenye kuzibeba hizo mizizi ya zambi na kwa mantiki hii nikaona ni vyema niyaweke bayana yale ambayo nilijifunza. Katika makala yangu nitabobea katika nyanja kuu nne (4) ambazo twapasa kujiuliza juu ya Rwanda kama ifuatavyo.....
1- Je ni kweri Rwanda hakuna ukabila?
2-Je ni kweri uchumi wa Rwanda unasadifu rasilimali zake?
3-Je utawala wa mkono wa chuma (Paul Kagame) Rwanda ni demokrasia ambayo wanyarwanda wanalizika nayo?
4-Na Je Tanzania ina lolote lile lakujifunza kutoka Rwanda?
Mambo hayo manne niliyo yataja hapo juu ambayo ivi punde nitakwenda kuyafanyia upembuzi yakinifu na uchambuzi sanifu ndio ambayo kichwa cha makala yangu hii kimejibainisha wazi kuwa "Je Rwanda iko salama baada ya kumalizika kwa mauaji ya kimbali mwaka 1994?" kabla ya kuanza kuyapembua makala hii nivyema kwanza tukaifahamu Rwanda kinagaubagha.
RWANDA.
Rwanda ni taifa linalo patikana ukanda wa Afrika ya kati katika Afrika ya mashaliki na kaskazini imepakana na Uganda magharibi imepakana na DRC kusini imepakana na Burundi na mashaliki imepakana na Tanzania. Rwanda ndio taifa la kwanza katika jumuia ya Afrika mashaliki ambalo glafu yake ya kuimalika kwa uchumi imekuwa ikiimalika karibu mara kumi na saba (17) kwa miaka mitano (5) toka mwaka 2003-2008 na uchumi umekuwa kwa kasi ya 5.9% kwa miaka ya hivi karibuni yani 2013-2016 kwa maana ya report ya Benki ya dunia (WB) na shilika la tathimini ya maendeleo kwa nchi masikini Kupitia United Nationa development program UNDP.
Pamoja na ithibati hiyo Rwanda imekuwa ikisifiwa kwa kutekeleza mpango wa usawa katika jinsia (Gender Equality) kwa karibu 53% na imekuwa ndio nchi pekee ukanda wa Afrika mashariki na kati kwa kuongoza katika mapambano ya rushwa na kuwa nchi ya 3 Africa kwa kupunguza mianya ya rushwa ikiwa nyuma ya Visiwa vya shelisheli na Botiswana. Pia katika dhana ya kudhibiti fedha na kudhibiti matumizi mabaya ya mali ya umma Rwanda imekuwa nchi ya kwanza kwa Afrika karibu kwa mara ya nne sasa toka mwaka 2012, -2013, -2014 na 2015 na hii imeifanya kuwa nchi yenye kujivunia kwa kuimalika kwa uchumi wake pamoja na kupigiwa kerere na kulalamikiwa na mataifa makubwa ya magharibu kwa kuibinya demokrasia na utawala wa mabavu.
HISTORIA YA RWANDA.
Rwanda huko nyuma ulijulikana kama Uruanda kabla haijaja kuwa Rwanda kama inavyo julikana sasa toka mwaka 1943. wenyeji wa nchi hiyo ni kabila la Watwa (Batwa) ambao waliishi hapo toka miaka ya 300 BC na baadae kati ya miaka 110 AD na 340 AD walikuja jamii nyingine ya wabantu waliotoka kwenye misitu ya Kongo na Kameroni waliojulikana kama Wahutu (Hutu) ambao walitawanyika katika ukanda wote wa milima ya "Ruanda na Urundi" na walikuwa wawindaji na baadae wakaanza kujihusisha na shuguri za kilimo mnamo miaka ya 600 AD. Katikati ya miaka ya 900 AD jamii kubwa ya Nilotic kutoka kwenye kikundi cha jamii ya wafugaji ya Wahamatic iliyojulikana kama Watusi (Tusi) ilianza kuvamia ukanda wote wa nyanda za mashaliki ya Afrika ya kati kuanzia aridhi ya Kalamojog, Bunyoro na Buganda huko Uganda hali iliyopelekea kuzuka kwa vita za makabila dhidi ya kabila lenyeji na kabila vamizi kwa kuwa Watusi walikuwa na mifugo kuna mahali walishindwa vibaya sana na kukibia kama katika himaya ya Kalamoja lakin kuna mahali waliwashinda wenyeji na kuanzisha himaya mfano huko Nyankole na Bunyoro.
Wingi wa idadi ya wahamiaji wa jamii ya Watusi ilipelekea kuwafanya kutafuta aridhi na kujitanua ukanda wote wa kusini mwa Afrika mashaliki ya kati kitu kilichopelekea jamii hiyo ya Watusi kufika Rwanda na hatimaye miaka ya 987 AD mpaka miaka ya 1400 AD kalibu maeneo yote ya Ruanda-Urundi iikuwa ikikaliwa na kumilikiwa na jamii ya Watusi.
Na mpaka karne ya 16 Rwanda ilikuwa eneo lenye utawala wa kifalme Mwanzo wa himaya ya watusi iliyojulikana kama BAHIMA STATE (HIMAYA YA BAHIMA) ilianzia katika eneo la Ziwa la Muhazi na kufika mpaka milima ya Mulanvya. Watawala wenye cheo cha "Mwami" kutoka kikundi cha wafugaji (Watutsi) walitanua himaya zao tangu miaka ya 1200 mpaka 1680 AD hadi kufika eneo la leo hii ambalo linajumuisha kalibu Rwanda na Burundi yote. Wafugaji wa ng'ombe Watutsi walikalia nchi pamoja na wakulima wa Kihutu na wawindaji Watwaa.
UJIO WA WAKOLONI NCHNI RWANDA
Kuanza kwa uvamizi wa wazungu mwanzoni mwa miaka ya 1800 katika Afrika kuliifanya Rwanda kuanza kutawaliwa na Ujerumani ambapo koloni hilo lilijumuisha Burundi, Rwanda na Tanganyika zote zilikuwa ni nchi moja iliojulikana kama Ujerumani ya Afrika mashaliki (German east Africa teritory) ambapo baadae Rwanda alipewa Uberigiji mara baada ya vita ya kwanza ya dunia kumalizika ndipo Urundi yani Burundi na Urwanda yani Rwanda zilipo pewa koloni la Uberigiji kwa kile kilichoitwa "Fidia ya kushindwa vita kwa Ujerumani" kupitia mkataba wa "Anglo-Belgium Treaty 1919" mara baada ya mkutano wa Veriseyas (mkataba wa Verseryas).
Ujio wa mbelgiji nchini Rwanda ndio chanzo cha kuibuka kwa matabaka baina ya makabila mkubwa mawili yani Wahutu na Watusi, hapa mbeligi alianza kuwatumia Watusi katika shuguli zake za kiutawala kama makalani, walimu,maafisa wa ngazi za chini na kuwapa fursa za kijamii tofauti na ilivyo kwa kabila la Wahutu waliowengi na hii ni kutokana na kabila la Wahutu walikuwa watu wakolofi, wabishi na wakali huku Watusi walikuwa watu wakimya, wapole na wastaalabu kitu kikichopelekea wazungu kuwapenda na kuwatumia katika shuguli za utawala jambo lililopelekea kuongezeka kwa chuki baina ya hayo makabila mawili yani Watusi na Wahutu kwani Watusi waliwanyanyapaa Wahutu kwa kiasi kikubwa na chuki hiyo iliongezewa chuki maradufu na wakoloni wa kizungu (Wabeligiji) kwakuwa karibu sehemu nyingi za utawala walipewa Watusi kama Askali wa usalama, Askali wa mageleza maafisa suluhu na sehemu nyigi za utawala.
Na ilipofika miaka ya 1949 wabeligiji waliona kuwepo haja ya kubadili mfumo wa utawala na kuanzisha mfumo mpya ulioitwa "Tribe clasical system of administration" kwa kuwa tayali kulikuwa kuna dalili zote za kumalizika kwa ukoloni nchini Rwanda ili kupunguza vuguvugu lilokuwa likiendelea hivyo wakoloni wa kibeligiji waliamini katika ile dhana ya "Divide and Rule" (wagawanye ili uwatawale) na hii ndio iliyo kuja kuchochea ukabila uliopelekea vurugu na mauaji ya kikabila ya mwaka 1959, 1962, 1965, 1972, na yale mabaya kabisa kuwahi kutokea Afrika ya 1994 yaliyojulikana kama "Mauaji ya kimbali" .
Kwani Katika kubadili mfumo wa utawala wa (Tribe clasical system of administration) wabeligi walianza kubadili mweleko wa kuwapa fursa Watusi na kuanza kuwathamini Wahutu. Kwani 1950 mbeligiji alianza kuwapa kipaumbele Wahutu kutokana na msukumo wa wamissionari wa kikatoriki walioanza kuwatetea Wahutu kwa kuona wao ndio wanaonyanyaswa na kubaguriwa hivyo uberigiji aliona ni vyema kuwapa msukumo Wahutu kwakuwa kipindi hiko vuguvugu la Wahutu lilikuwa kubwa. Katika miaka ya 1950 ilionekana na kudhihirika ya kwamba ukoloni unaelekea mwisho wake. Uhusiano kati ya Wahutu na Watutsi ukawa vigumu kwa sababu Wabelgiji walibadilisha siasa yao yakupendelea Watutsi wakidai haki zaidi kwa ajili ya Wahutu waliokuwa wengi. Ni hasa wamisionari wa katoliki Mapadre Weupe waliosimama upande wa Wahutu wakiona ndio wagandamizwa.
Mwami Mutara Rudahigwa wa himaya ya Rwanda aliyejiita pia mfalime Charles alijaribu kuleta upatanishi kati ya vikundi katika nchi jambo ambalo lilishindikana kwani mwaka 1954 aligawa nchi ya kifalme kati ya kusini kwa Wahutu na kaskazini kwa Watutsi. Lakini alikuwa na wapinzani Watutsi wenye misimamo mikali walio mpinga na wakaamua kumua mwaka 1959. Mtoto wake Mwami Kigeri V. alisimikwa kwenye kiti hicho. Hatua hii ilisababisha ghasia na vurugu nchini Rwanda na kusababisha mauaji ya watu kwa sababu Wahutu walidai kuwa na neno katika mabadiliko ya serikali. Mwezi wa Novemba 1959 Mwami Kigeri V alilazimishwa kuondoka nchini akikimbilia Uganda Watutsi wenye siasa kali walijaribu kumwua kiongozi wa chama cha Mouvement Democratique Republicain (MDR) chama kikubwa cha Wahutu katika vuguvugu la kuwakomboa wahutu.
Wahutu walijibu kwa kuwashambulia na kuua Watutsi. Wabelgiji walitumia wanajeshi wao kupoza hali hiyo nchini Rwanda
VUGUVUGU LA UHURU NCHINI RWANDA
Mwanzoni mwa miaka ya 1950 vuguvugu la ukombozi nchini Rwanda lilianza huku likiwa limebeba sehemu kubwa ya ukabila hasa wa upande wa Wahutu ambao walikuwa ndio wengi. Hata hivyo Katika uchaguzi wa kwanza wa halmashauri, tarafa na miji kabla ya uhuru chama cha Parmehutu kilichoundwa miaka 7 nyuma ambacho kilikuwa ni chama cha Wahutu wenye misimamo mikali kilichokuwa kikiongozwa na kiongozi wake Gregol Kayibanda ambaye alikuwa muhutu mwenye misimamo ya kihafidhina juu ya uhutu kilishinda viti vingi na hii ni kwakuwa idadi ya Wahutu Rwanda ilikuwa ikizidi idadi ya watusi waliokadiliws kufika milion 1 na laki 3 huku wahutu wakiwa karibu milioni 3
Katika uchaguzi wa wawakilishi wa bunge la kikoloni wa mwaka 1960 chama cha Parmehutu ndicho kilichopata kura nyingi ya karibu viti 160 kati ya viti 200 Viongozi wa Parmehutu walitangaza serikali mpya mwaka 1961 na Uchaguzi wa Bunge ukafanyika rasmi mwaka 1962 na chama cha Permehutu kilipata kura ya 77% na MDR 41% hivyo chama cha Parmehutu kiliongoza na kutakiwa kuunda serekali na ndicho kilichomchagua kiongozi wake Grégoire Kayibanda mwanasiasa mahili mwenye misimamo mikali ya kihafidhina aliyekuwa na mitazamo ya kulifutilia mbali kizazi cha wafugaji wa kitusi alichaguriwa na chama chake cha Permehutu kuwa kiongozi na kupitishwa kuwa Rais wa kwanza wa Rwanda Tarehe 01.07.1962 Rwanda ilipata uhuru wake kamili chini ya chama cha kihutu Permehutu Wakati huo zaidi ya Watutsi 350,000 tayari walishakuwa wamekimbilia nchi za jiran kutokana na mauaji yaliyo anza kuonekana na kutekelezwa na wahutu wenye msimamo mkali na chuki kwa Watusi.
Mwaka uliofuata wa 1963 vikundi vya Watutsi kutoka nchi hizo za jirani walijaribu kufanya mapinduzi kwa kushambulia serikali mpya ya Gregol Kayibanda wakitokea uhamishoni Kitendo hicho kilifuatiwa na uangamizaji wa kwanza wa Watutsi zaidi ya 100,000 waliouawa na Wahutu. Hata katika miaka iliyofuata mauaji dhidi ya Watutsi iliendelea. Na kuongeza chuki na hali ya mauaji ya kitusi kushamili kitu kilicho pelekea Mwaka 1973 Generali Juvenal Habariyama kutoka chama cha MDR, mhutu mwenye msimamo wa wastani kuongoza mapinduzi ya kumpindua Rais Kayibanda na kumuweka kizuizini mpaka kifo chake Kayibanda kilicho sababishwa na njaa na mateso aliyofanyiwa na Jeneral Juvenal Habiyarimana. Ikumbukwe kuwa Juvenal Habiyarimana alikuwa ni mnadhimu wa jeshi la serikali ya Gregol Kayibanda.
Mara baada ya mapinduzi Juvenal Habiyarimana alianzisha serikali ya kijeshi akijaribu kupatanisha vikundi ndani ya taifa Lakini mwaka uliofuata 1974 mauaji ya Watutsi yalitokea tena yaliyotekelezwa na Wahutu wenye misimamo mikali. Mnamo 1990 ilikuwa wazi ya kwamba Rwanda ilikuwa na hali ngumu sana kufatwa na kukithili kwa mauaji ya kitusi na Wahutu Kwa upande moja nchi za mataifa zilisukuma serikali za Afrika kuruhusu kura huru za kisiasa nchi Rwanda.
Habyarimana alijaribu kutafuta suluhisho na utengamano wa kitaifa, akaanza kujadiliana na Watutsi wa nje ili kumaliza mivutano ya kikabila lakini alikutana na upinzani kwa upande wa Wahutu wenye misimamo mikali kwani hawakutaka kuwa na uelewano na Watutsi. Mivutano hiyo ilipelekea kuzuka kwa vuguvugu la watusi waliokuwa wamekimbia mapigano na mauaji dhidi yao moja ya kundi la watusi wenye misimamo ya wastani na waliotaka utengano wa kitaifa la RPF liliundwa na watusi waliokuwa nchini uganda.
Oktoba 1990 Watutsi waliokaa Uganda walianzisha chama cha RPF (Rwanda Patriotic Front) wakiwa na wafuasi wahutu wachache wakavamia Rwanda kwa silaha. Kiongozi wao alikuwa Paul Kagame aliyeondoka Rwanda akiwa mtoto wa miaka minne. Alikuwa amejiunga na jeshi la Yoweri Museveni na kupanda ngazi katika jeshi la Uganda hadi kuwa mkuu wa huduma ya usalama ya kijeshi ya Uganda. Walitaka kulazimisha serikali ibadilishe hali ya Watutsi kuwa raia bila haki Lakini uvamizi huu ulisababisha kuongezeka kwa ukali wa Wahutu dhidi ya Watutsi ndani ya Rwanda na siasa kali kwa upande wa viongozi Wahutu. Kikundi cha kihutu cha Interahamwe kilipewa silaha kujibu mapigo dhidi ya uvamizi wa Kagame, Maelfu ya Watutsi Warwanda waliuawa. Vita kati ya wapinzani kutoka Uganda na jeshi la serikali iliendelea mpakani hadi pande zote mbili zilikutana mjini Arusha Tanzania kutafuta ufumbuzi na kukomeshwa kwa migogoro ya kikabila kati ya Watusi na Wahutu katika mataifa mawili ya Burundi na Rwanda kwani kipindi hicho migogoro kati ya Watusi na Wahutu ulikiwa unafanana. Hivyo uliandaliwa upatanishi chini ya usimamizi wa Tanzania na kupatanisha ili kukomesha mauaji dhidi ya Wahutu na Watusi kwa vita 1992 chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.
Sehemu ya viongozi Wanyarwanda walijiandaa kutafuta utaratibu mpya lakini wengine walifanya mipango ya kumaliza swali la Watutsi kabisa wakipanga kuua Watutsi wote nchini. Tarehe. 06.04.1994 Rais Habariyama akirudi nchini Rwanda kutoka safari ya Tanzania katika upatanishi ndipo Ndege yake ilipigwa kombora kabla ya kutua ikaanguka chini yeye Juvenal Habariaman na Cypier Ntaramila Rais wa burundi kufariki. Uwezekano ni mkubwa ya kwamba ni Wahutu wenye msimamo mkali ndio waliomua, Juvernal Habiarimana na Cypier Ntaramila lakini wengine walisema ni Jenerali Paul Kagame na kikosi chake cha RPF walihusika katika utunguaji wa ndege hiyo ya marais hawo wawili. Kitendo hicho kilikuwa mdio mwanzo cha mauaji ambayo hayakuwahi kutokea Afrika.
MAUAJI YA KIMBALI 1994
"Viongozi wa Interahamwe walio pewa silaha na viongozi wa jeshi la kitaifa lilokuwa chini ya serekali ya kihutu na vikundi vikali vya Kihutu walitekeleza mipango wakishilikiama na wazungu webeliji na wafalansa ya kuwakusanya Watutsi kila mahali na kuwaua kikatili Hakujawa na idadi kamili lakini makadirio ya chini yanataja Watutsi wapatao 750.000 na Wahutu wasio wakali zaidi ya 100.000 waliuawa na Interahamwe na wanajeshi wa serikali ya Kihutu". Ndivyo alivyo sema msemaji wa makumbusho ya mauaji ya kimbali maeneo ya Nyakivuvu jijini kigari bwana Niyosenga Yisombere.
Kimsingi katika Mauaji ya Kimbari ya Rwanda yalikuwa mauaji ya halaiki nchini Rwanda mnamo mwaka wa 1994 ambapo Watutsi, Watwa na baadhi ya watu wa kabila la Kihutu waliuliwa na serikali iliyosimamiwa na viongozi wa Kihutu. Katika kipindi cha takriban siku 100, kuanzia kuuliwa kwa Habyarimana na Ntaryamira tarehe 6 Aprili hadi katikati mwa mwezi Julai, walau watu 500,000 waliuawa, au karibu asilimia 20% ya idadi ya watu nchini Rwanda wakati huo.
Ujumbe wa majaji wa Ufaransa waliwasili mjini Kigali kwa lengo la kuchunguza chanzo cha mauaji ya kimbari ya Rwanda na kuanguka kwa ndege iliyokuwa imembeba Juvenail Habyarimana rais wa wakati huo wa Rwanda. Kuuawa Habyarimana tarehe 6 Aprili 1994 kulikuwa chanzo muhimu cha mauaji ya kimbari nchini humo. Kuhusiana na kuuawa Habyarimana, Wahutu wenye misimamo ya kufurutu mpaka walihusisha tukio la kutunguliwa ndege yake na wapinzani wa Kitutsi na kulitumia kama kisingizio cha kuanzishia mashambulio na mauaji makubwa na ya kutisha dhidi ya Watutsi, Watwa na Wahutu wenye misimamo ya wastani.
Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yaliendelea kwa muda wa siku 100 hadi hali ya mambo ilipodhibitiwa na vikosi vya waasi wa wakati huo wa RPF, wapiganaji wake wengi wakiwa ni Watutsi. Inasemekana kuwa watu wapatao laki nane waliuawa, wengi wao wakiwa Watutsi, lakini wakiwemo pia Wahutu wenye misimamo ya wastani.
Huko nyuma Rais Paul Kagame wa Rwanda alituhumiwa na Jean-Lousi Bruguiere, mmoja wa majaji maarufu wa Ufaransa kuwa alishiriki katika mauaji ya halaiki ya wananchi wa nchi hiyo na vilevile mauaji ya Habiyarimana. Hatua hiyo iliipelekea serikali ya Kigali nayo kuwatuhumu viongozi wa Ufaransa kuwa walishiriki katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Kwa utaratibu huo Kamisheni Huru ya Kitaifa nchini Rwanda ambayo iliamuriwa na serikali ya Kigali ikusanye nyaraka na ushahidi unaothibitisha nafasi ya Paris katika mauaji ya Rwanda, ilitayarisha nyaraka zilizofichua jinsi Ufaransa ilivyoshiriki katika mauaji hayo, ambayo yalipewa jina la "Jinai za Watenda Jinai".
Kwa mujibu wa ripoti ya kamisheni hiyo, nduru za juu za kisiasa, za kidiplomasia na za kijeshi za Ufaransa ziliratibu na kutekeleza mauaji hayo ya kimbari. Vilevile ripoti hiyo ilisema kwamba, Paris ilishiriki katika kutoa mafunzo kwa wanajeshi na waasi wa Kihutu, kutoa silaha na suhula za kijeshi, kusaidia kwa siri mauaji, ubakaji na mateso katika ardhi ya Rwanda. Tuhuma hizo zilivuruga kabisa uhusiano wa Ufaransa na Rwanda.
Hata hivyo mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2009 viongozi wa nchi hizo mbili waliamua kuhuisha tena uhusiano wao na serikali ya Paris kuwapa majaji jukumu la kufuatilia faili la mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Wachambuzi wa jambo wanaamini kuwa, hamu ya nchi hizo mbili ya kutaka kuanzisha tena uhusiano wao wa kisiasa haiwezi kufuta shaka ya nafasi ya Ufaransa katika mauaji ya kimbari ya Rwanda. Wala nafasi ya Kagame na RPF kuhusika,
Ufaransa ambayo siku zote imekuwa ikisisitiza kuungwa mkono ngano ya mauaji ya kimbari ya Wayahudi katika Vita vya pili vya Dunia, hivi sasa inapaswa kutoa jibu kuhusiana na tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Kamisheni ya Uchunguzi ya Rwanda.
Ikumbukwe tu katika mauaji ya kimbali nchini Rwanda Watu walikimbilia sehemu mbalimbali kutafuta hifadhi makanisani lakini hata huko walifuatwa walichinjwa bila huruma. Wahutu waliokataa kushiriki katika mauaji waliuawa pia kwakuwa waliwaona kama wasaliti machinjo hayo yalikuwa ya kutisha na kusikitisha sana kwani ayakuwai kuonekana Afrika. Kwa miezi miwili mauaji na vita yalienda sambamba na vifo vya watusi na wahutu wenye misimamo ya wastani waliuwawa. Hakukuwa na hatua zozote za dharula zilizochukuliwa kukomesha mauaji kutoka nje ya Rwanda au jumuiya yoyote ile sio AU au UN. hadi pale RPF iliposhinda Julai 1994 na kuchukua madaraka ya serikali.
baada ya mapigano ya mstuni ya muda ndipo waasi wa jeshi la RPF lilipo shinda na kuchukua nchi Jeshi la serekali ya Kihutu, Parmehutu na serikali ya Kihutu walikimbilia jimboni Kivu nchini Kongo wakiwalazimisha wakazi wengi kuwafata huko na kuongozana nao hali iliyosababisha kutokea kwa makambi ya wakimbizi makubwa sana katika Kongo ya mashariki maeneo ya Goma, Beni, Bunia, Butembo, Ituri na Misisi huko jimboni kivu kaskazini yaliyokuwa na idadi ya Wahutu milioni mbili. Walio wengi wamerudi baada ya kuimarika kwa serikali mpya ya Kagame miaka ya 1999 na 2003. Tangu ushindi wa kijeshi mwaka 1994, RPF walianzisha serikali ya umoja wa kitaifa. Rais alikuwa Pasteur Bizimungu mwanasiasa Mhutu aliyeshikamana na RPF huku Paul Kagame akiwa makamu wake wa Rais.
Mwaka 2000 mikakati ya Paul Kagame ilipo kamilika kwa kile kilichoitwa "kuanza kwa mikakati ya upanuzi wa himaya ya Watusi" kwa kile kilichoitwa "Mkataba wa Remela phase I" ndipo ilipo andaliwa mapinduzi balidi ya kumuondoa Bizimungu madalakani. Baada ya kupinduliwa kwa Bizimungu mwaka 2000 Paul Kagame akawa Rais 2003 na kudhibiti siasa yote ya wahutu ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti wanasiasa wote wanaompinga. Palitokea uchaguzi wa kwanza wa kirai ambapo chama cha RPF chini ya Jenerali Paul Kagame kilishinda na kuaza kwa safari ya utawala wa mkono wa chuma chini ya Kagame iliyo ifikisha Rwanda hapa ilipo.
Jeshi la Rwanda limeendelea kuwa na vita ndani ya Kongo likipigana na mabaki ya Wahutu wa Interahamwe waliokuwa wanashambulia Rwanda mara kwa mara kutoka Kongo. Kutokana na mauaji hayo ya 1994, mahakama ya kimataifa ya The Hague iliyopo nchini Uholanzi imeendesha hukumu nyingi kwa wahusika wake, vilevile mahakama ya kimataifa ya Arusha nchini Tanzania ya ICTR nayo imeendesha huku stahiki kwa wahusika kazaa lakini pia Ndani ya Rwanda mahakama za vijijini zinazoitwa "gachacha" zimejaribu kutoa hukuma juu ya waliohusika na mauaji ya mwaka 1994.
Baada ya upembuzi huo wa kuifahamu Rwanda sasa ni vyema tuludi kwenye madhumuni ya makala hii.... Ambazo nimezielezea huko mwanzo kama ifuatavyo
1- Je ni kweri Rwanda hakuna ukabila?
2-Je ni kweri uchumi wa Rwanda unasadifu rasilimali zake?
3-Je utawala wa mkono wa chuma (Paul Kagame) Rwanda ni demokrasia ambayo wanyarwanda wanalizika nayo?
4-Na Je Tanzania ina lolote lile lakujifunza kutoka Rwanda?
Sasa tulejee kwenye hili swali la kwanza la "je ni kweri Rwanda hakuna Ukabila?" Katika hoja hii imekuwa ikitiwa upako mara kazaa na Kagame mwenyewe kuwa nchini mwake hakuna ukabila lakini kiyakinifu na kiundani jambo hili si la ukweri hata kidogo tena ni uongo ulio wazi ambao auhitaji hata akili kujua. Ukweri ni kuwa Rwanda kuna ukabila ambao ndani yake una utukufu kwenye kabila la Watusi na kuwagandamiza Wahutu na hili linajibainisha katika maisha ya wanyarwanda wenyewe kwani ni kitu cha kawaida Mtusi Rwanda kuwa na vipaumbele vyote katika huduma za jamii na maisha ya kawaida katika serikali ya Kagame karibu 78% ya watumishi ni kutoka kabila la Kitusi. Hiyo dhana ya ukabila katika Rwanda imewapa mamlaka watusi juu ya Wahutu kwani "katika sheria za Rwanda Mtusi huthaminiwa sana kuliko mhutu kwa mantiki kuwa watusi wapo kwenye njama ya kumalizwa na wahutu walio wengi hivyo nchini Rwanda ni hatari zaidi muhutu kumkashfu Mtusi kuriko mtusi kumkashifu muhutu" alisema Juvenal Bosco mkazi wa kigari.
Ikumbukwe kuwa hata katika madhimisho ya mauaji ya kimbali maarufu kama "Kwibuka" huadhimishwa kuwakumbuka "Watusi" tu jambo ambalo sio sahihi hata kidogo kuwakumbuka watusi peke yao wakati karibu wahutu wenye misimamo ya wastani 100000 waliuwawa. Isitoshe kumekuwepo na dhana ya kizazi kipya nchini rwanda kuaminishwa kuwa utawala wa wahutu ulikuwa mbaya na wakinyama na kila kitu kilicho fanywa na utawala wa kihutu ni kibaya kwani hata katika mitaala ya elimu Rwanda imejibainisha hivyo. Na katika utawala wa Paul Kagame mara baada ya kukamata dola ulifutilia mbali mifumo yote iliyoyokuwa ikitumiwa na serikali ya wahutu na kuanzisha mifumo mipya ambayo ndani yake ina sehemu ya tamaduni ya kabila la Watusi mfano tu ni nembo ya taifa ya Rwanda ambayo alama zake ni viashilio vya matambiko ya kabila la Kitusi. Jambo ambalo kabila la Wahutu hulazimishwa kuwa sehemu ya kuabudu matambiko ya kabila la watusi wakati kitu hicho cha kuitambusilsha Rwanda kama basic trats za watusi ni kuwanyima wahutu haki za miiko na matambiko yao kwa kisingizio kisicho kuwa na mashiko.
Pia kumekuwepo na njama za kueneza himaya ya kitusi nchini Rwanda na kongo mashaliki kwa kile kinachoitwa "Mkataba wa Lemela" unaotekelezwa na Rwanda, Uganda na Kenya" wa kupanua na kuimalisha himaya ya watusi dhidi ya kabila la Wahutu. Na ni vyema ileweke kuwa nchini Rwanda Kagame hutumia mabilioni ya fedha kujilinda huku akiwa amewekeza rasilimali kubwa katika jeshi lake la RDF. Na ndio maana huwezi tembea zaidi ya mita (5m) bila kukuta askali wa jeshi la Rwanda akiwa katika dolia karibu mitaa na balabala zote za miji na vijiji nchini Rwanda na hii limeshakuwa jambo la kawaida kila siku na hii ni jambo la kawaida Rwanda kusambaza wanajeshi kimlinda Kagame dhidi ya uvamizi askar wa kihutu wa interahamwe
Operation ya kuwaangamiza vikosi vya waasi wa interahamwe na vikosi vya FRDL huko kivu ya kaskazini ndio tishio la selekari ya Rwanda na ndio maana kagame amewatengeneza makachero hatari kama General Laurent Nkunda Mihigo na Sultani Makange (War Lord) katika misitu ya Nord Kivu (North Kivu) ili kudhibiti kuibuka tena hawo wanaoitwa "waasi wa kihutu" Ukiwa katika miji mikubwa kama kigari, Butare, Kayonza na Musanze raia wenye maisha bora utakuta ni watusi huku Wahutu wakiwa wamenyamanzishwa na kujengewa uwoga wa hali ya juu sana juu ya kuhoji mustakabali wa taifa lao.
"Rwanda kumekuwa na kutokuwepo na uhuru wa kusema wazi na kama unataka kuyaweka hatalini maisha yako jalibu kuwa msemaji wa kukosoa siasa na hali ya mambo nchini Rwanda" alizungumza mama mmoja mwenye asili ya kihutu kwa sauti ya chini sana aliyetaka nisilitaje jina lake kwa usalama wa maisha yake na familiya yake. Huku Rwanda sura za uoga zilizo jaa wasiwasi mkubwa juu ya mustakabal wa nchi ya Rwanda ni jambo la kawaida unapoanza kutaka kuanzisha mijadala ya siasa na hali ya mambo katika taifa la Rwanda na ni nadra sana kuona watu wakijadili siasa kwa uwazi kama ilivyo zoeleka nyumbani Tanzania. Pamoja na utilivu uliopo Wahutu wamekuwa wakionekana kutokulidhika na utawala wa kitusi kama alivyosema mwalimu wa chuo kikuu cha NUR cha Mjini Butare kuwa "bado kuna wasiwasi mkubwa wa hali ya amani Rwanda kwakuwa bado kuna chembe za kuonesha kuwa kunaubaguzi dhidi ya wahutu zinazofanywa na watusi katika njia za kiintelejensia"
Pamoja na hilo Kagame bado anaendelea kupambana na Wahutu wote wa ndani na nje ya Rwanda kwa kuwashambulia kijasusi ikiwa ni pamoja kuto ruhusu uwazi wa democracy kwa kuhofia kupenya kwa siasa za Wahutu walio wengi.
Mantiki ya pili katika makala hii juu ya "je kuna ukweri uchumi wa Rwanda kusadifu rasilimali zake?." Ikumbukwe kuwa uchumi wa Rwanda umekuwa ukiimlalika sana kwa miaka ya hivi karibuni na kumekuwa na ukweri usiopingika kuwa nchi ya Kongo DRC ndio ambayo rasilimali zake hasa za majimbo ya Kongo ya mashariki kama Kivu kaskazini na kusini zimekuwa zikiporwa na Rwanda na ndizo zinazotumika kuimalisha uchumi wa Rwanda. Itakumbukwa kuwa Rwanda ndio inayochochea pakubwa kuzorota kwa amani ya mashariki mwa kongo na ikumbukwe kuwa vikosi vyote vya kiasi vinavyo endesha mapigano mashaliki mwa kongo ni vikosi mkakati chini ya mikakati ya kikachero ya kagame ya kuiba dhahabu na madini ya thamani nchini kongo Kwa manufaa ya Rwanda na mkakati huu umekuwa ukiendeshwa na wazili wa ulinzi wa Rwanda jenerali James Ngabarabe ambaye huifahamu Rwanda kwakua aliwahi kuwa mkuu wa usalama wa Kongo na mkuu wa majeshi ya DRC katika kipindi cha utawala wa Laulent Desire Kabila kutokana na kishilikiana na kabila kumg'oa madalakani Mubutu.
Na hifahamike kuwa utawala huu wa Kongo tunaouona chini ya Joseph Kabila umewekwa madalakani na mataifa ya Rwanda na Uganda kupitia "mkataba wa Lemela" kitu ambacho baadae Laulent Kabila aliupinga na kuuita ni "mkataba wa msituni na kamwe hawezi kuiuza nchi kwa makubaliano ya mstituni" kitu kilicho pelekea kifo chake hapo baadae kwa kuuwawa kwa kupigwa risasi. Kabila aliuawa kabla hajamaliza kunyukana na Rwanda katika mgogoro uliojulikana kama "Ukaidi wa kabila juu ya makubaliano ya Lamela" Aliuawa na mmoja wa “watoto” wake yaani vijana wadogo waliokuwa watu wa karibu sana na waliomlinda tangu akiwa msituni. Kuna maelezo tatanishi juu ya kifo chake Kuna wanaodai aliyemuua alitumwa na waliokuwa wakitaka atekeleze makubaliano ya Lemera lakini wengine wanadai ni karata za nchi za Magharibi Kwakuwa Jonas Savimbi aliuawa katika mwaka moja tu baada ya kifo cha Kabila inadaiwa kulikuwa na mkono wa mataifa makubwa hili likitaka kuingia Kongo na hivyo kuomba msaada wa kuondoshwa kwa Kabila huku likiwezesha kukamatwa na kuuawa kwa Savimbi. Siasa hizi hazijafafanuliwa mpaka leo.
Ningeomba Ifahameke kuwa kile ambacho Kinachoitwa vita vya sasa nchini Kongo ni utekelezaji wa “Makubaliano ya Lemera” ya mwaka 1996 yenye shabaha ya kuigawa nchi hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati katika Makubaliano hayo yalifanywa kati ya Laurent Desire Kabila akiwa kiongozi wa chama cha “kuikomboa Kongo” kutoka utawala wa dikteta Mobutu Sese Seko, kwa upande mmoja; na wapiganaji wa Kinyarwanda kutoka Rwanda na Mashariki mwa Kongo ambao hapo awali walijulikana kama "Wanyamulenge" kabla ya kubadilishwa jina na kuwa AFDL. Makubaliano ambayo yalifanyika kwenye vilima vya Lemera vilivyoko Kivu ya Kusini na kujulikana kwa jina hilo la Lemela yalimtaka Kabila, baada ya kuwa rais wa Kongo aruhusu mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kuwa makazi ya Wanyarwanda wa kabila la Kitutsi.
Taarifa zinaonyesha makubaliano yaliandaliwa mwanzoni mjini Kigali na baadae kutiliwa saini pale katika milima ya Lemela Kivu ya kusini. Ilikubaliwa wakati huo kwamba hiyo ndiyo ingekuwa “asante” kwa Rwanda “kwa ukombozi wa Kongo.” Toka hapo kumekuwa na uendelezaji wa kupachikwa majeshi ya mistuni kongo na kuendelea kujichotea madini huko Kongo ambayo ndio yanayotumiwa kuijenga Rwanda. Na ndio maana Kagame alikuwa mkali kama mbogo mara baada ya Tanzania kutaka kuialibia ulaji pale Rais mstaafu Jakaya kikwete alipo peleka jeshi letu kule mashaliki kuwaondoa waasi wa M23.
Pamoja na hayo yote tulio yaona hapo juu katika upembuzi juu ya taifa la Rwanda. "Je utawala wa mkono wa chuma (Paul Kagame) Rwanda ni demokrasia ambayo wanyarwanda wanalizika nayo?". Katika swali hili tunapaswa kuitazama siasa ya serikali ya Kagame na kile kinachoitwa demokrasia ya Rwanda. Kagame amekuwa akitajwa kama mwanasiasa hatari zaidi katika ukanda wa maziwa makuu kwa kile kinacho tazamwa kama mbinu, mikakati, ujasusi na mipango yake ya kudhibiti wahasimu wake wa kisiasa na kiutawala pamoja na udukuaji wa taalifa za kintelejensia kwa kujalibu kuongeza ushawishi wake kimatifa na ukanda wa Afrika. Na hii imefanya kuwa na mazingira magumu ya siasa nchini Rwanda. "Ukiwa mpinzani wa kweri Rwanda basi maisha yako ujue ndi mwisho wake na wapinzani wote Rwanda ni vibalaka maalumu waliopandikizwa na kagame hakuna democracy hapa ni kiini macho tu" aliongeza kusema Juvenal Bosco mkazi wa Kigari. Na hili limekuwa likijionesha wazi hapa Rwanda kwani vyama vya siasa vilivyopo ni vile vyama pacha ikiwemo vyama vya NLP na SDP ambavyo vyote vimeonekana kuisapot RPF ya Kagame.
Ikumbukwe kuwa wakati wote Rwanda Kagame ndio ameonekana kuwa nyota kwa nchi na wala hakuna ruhusa ya vyama vya siasa kufanya shughuri za kisiasa kama mikutano ya hadharani wala kazi za kujijenga mpaka kipindi cha kampeni kwa maana baada ya miaka 7. Na pale anapojitokeza mpinzani wa Kagame basi kikosi maalumu kitiifu kwa Kagame kinamshugurikia mara moja na hii imejibainisha kwa mauaji ya viongoz kazaa wa jeshi na siasa ya watu wanao onekana kutaka kumpinga Paul Kagame.
Pamoja na yote hayo "Je Tanzania inalolote la kujifunza kutoka Rwanda?" Hili ndio swali "Mugharabu" ambalo twapasa kulitazama katika hitimisho la makala hii. Waswahili wanamsemo unaosema "elimu uchukuliwa mahali popote bila kujali anayokupatia elimu hiyo ata kama unaipata chini ya mti wa muembe". Pili Taifa lolote imara lazima lijifunze mambo mengi labda nikumbushe tu kupitia msemo wa wanazuoni wa kiarabu wa karne ya 9 unaosema " elimu yoyote chukuwa hata kama itakuwa ndani ya mdomo wa mbwa pamoja na mdomo wa mbwa ni najisi wewe acha najisi yake wew chukua na achana na najisi hii "(Hassa ib Batuta). Sasa ili taifa letu Tanzania tusiwe kama mbwa anayepotezwa na miruzi mingi na kujikuta msemo huu unatuhusu unaosema "Lakin mtu anayeongozwa na mihemuko ya kupenda ni lahisi mnoo kudanganywa" (Benjamin Nyetanyau).
Binafsi naamini yapo tunayoweza kujifunza kutoka Rwanda pamoja nchi hiyo kuwa na changamoto lukuki ambazo zinaipatia sifa mbaya Rwanda ni vyema zile ambazo azina faida na sisi tuka achana nazo na kuchukua yale ambayo yatatufaidisha kama taifa. Nitazitaja baazi ya mambo ambayo binafsi naamini tunaweza jufunza toka Rwanda.
1- Twaweza kujifunza Swala la Teknology kutoka Rwanda kwani Rwanda imepiga hatua kubwa ya kukusanya mapato kwa njia ya kielectronic compare to Tanzania. Rwanda wana mfumo wa kitaifa wa kukusanya taalifa zote za nchi zima kutoka katika idala zote za umma na binafsi kupitia mfumo maalumu unaokusanya taalifa zote na kuzipeleka mahali pamoja kwa siku wanaouita RNSS (Rwanda Network Softwer system) katika mfumo huu vitu vyote vime unganishwa katika system hii kutia ndani mashine za kodi za EBM (EFD), mifumo ya mabenki ya kuweka na kutoa pesa pamoja na uendeshahaji wa shuguri zote za benki, custom, import &Export, huduma za jamii katika vituo vya police,hospital, magereza na sehemu zote za umma na binafsi. Huu utalatibu unaongozwa na idala maalumu ya ofisi ya Rais chini ya usalama wa taifa. Hivyo ni vyema na Tanzania tukajifunza kutumia mfumo kama huu ili kurasimisha mambo yote ndani ya utalatibu jambo ambalo litaisaidia serekali kuongoza mambo kwaufanisi wa hali ya juu.
2- Kwani bei za vitu na huduma zote nchini Rwanda zimewekwa mtandaoni na kila mtu atakapo kupata huduma au kitu sokoni hutazama hivyo hiyo upunguza urasimu wa kupata huduma na yatupasa yamkini na sisi Tanzania kujifunza hatua hiyo nzuri ya kimaendeleo.
3- malipo yote nchini Rwanda katika idala ya umma yanafanywa kierectronic katika njia zote za malipo hata kama ni sent 1 ni kosa la jinai mtumishi wa umma kupokea pesa mkononi. Na nilazima utakapo lipa upatiwe list ya RRA (Rwanda Revenue Authorty) ni kosa kuto toa au kudai rist na adhabu yake ni faini ya milioni 20 ya Rwanda (Tsh 70 milion) na malipo yote nilazima ukalipe benki hata kama ni mfumo wa usafiri jambo Hili hata sisi tunapaswa kuiga kwani itasaidia hata katika ukusanyaji wa kodi sababu its easy kujua serikali imeingiza kiasi gani kwa siku kwani mfumo wote utaongozwa na mfumo mmoja. kujifunza njia hii nasi tuweze kupiga hatua zaidi katika makusanyo ya kodi hivyo mimi sioni Kibaya kipi sie kujifunza mambo kazaa kutoka Rwanda. *Au bado tunaamini kuwa kila kitu kizuri hutoka ulaya, Asia na America and Africans we have nothing to learn from Africa?* Mie nafikili si vyema.
4- Usafi ni utamaduni wa Rwanda na ni kosa kubwa sana katika Rwanda kuchafua mazingira zimetengwa kila jumamosi ya wiki kuwa siku maalumu ya usafi kitaifa na imewekewa mkazo na usipo shiliki azabu ya RF 30000 ( sawa na Tsh10000) na wamejenga uzalendo wa usafi kwa kila Raia.
Mwisho japo sio kwa umuhimu wake ningependa niweke taalifa wazi ili jamii ielewe kuwa "KWAMBA HATUTAKIWI KUWA NA HOFU NA RWANDA, PAMOJA NA KUONEKANA KUWA TAIFA JASUSI NA HATARI LINALO VURUGA AMANI UKANDA WA MAZIWA MAKUU BADALA YAKE KWA SABABU TUNATAKA MAENDELEO LAZIMA TUJIFUNZE NAMNA YA KUNUFAIKA HATA KUTOKA KWA MTU YEYOTE ILI MRADI HATUUMIUZI" .....( msaada wa ushindi ni mahali popote ama kwa shetani au kwa mungu ilimladi ushinde. Kauli hii ilinenwa na Erinesto Che Guavara 1949).
pili katika kutamatisha makala hii naikumbuka sana kauli ya mzee Mandela aliulizwa "INAKUWAJE AFRIKA KUSINI UNASHIRIKIANA NA FIDEL CASTOR WAKATI NI MTU MBAYA... ANAECHUKIWA NA DUNIA NZIMA" akawajibu kwa kusema "HUYO MTU MIMI ALINISAIDIA KUNIPA SILAHA YA KUPAMBANA NA MAKABURU....NAMI PIA NIMWITE MBAYA KWA SABABU NYINYI KWENU NI MBAYA?". Hivyo sababu Rwanda ni ndugu zetu tena wakihistoria tunayo haja ya kuongeza uhusiano wa kidpromasia ili kupanua nafasi ya ushawishi wa Tanzania ndani ya Rwanda na ukanda wote wa kusini mwa Afrika na Afrika ya kati pamoja na Afrika mashaliki ili kuongeza nguvu ya Tanzania katika biashara na kunufaika kiuchumi, sababu Rwanda ndio soko letu kubwa katika jumuiya ya Africa mashariki. Pia tunahaja ya kujipanua zaidi na kujenga Umajumui wa kisiasa,kijamii na kiusalama.
"Mungu bariki Afrika, Mungu ibaliki, Rwanda Mungu wabaliki Wanyaranda"
0 comments:
Post a Comment