Siku moja baada ya klabu ya Manchester City kutangaza kumsajili winga na kiungo mshambuliaji wa Schalke 04 Leroy Sane na kumpa mkataba wa miaka mitano, leo August 3 2016 klabu ya Man City imetangaza kukamilisha usajili wa mshambuliaji waGagriel Jesus kutoka Palmeiras.
Man City imefanikiwa kumsajili Gabriel Jesus kutoka Palmeras kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 27 na kumpa mkataba wa miaka mitano, makubaliano ya Man City naPalmeras katika uhamisho wa staa huyo ni kuwa atajiunga na Man City baada ya msimu wa Ligi Kuu Brazil kumalizika.
Gabriel Jesus ambaye amewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi kutoka bara laAmerica Kusini, alikuwa akiwaniwa na klabu ya FC Barcelona ya Hispania, Gabriel Jesus ana umri wa miaka 19, lakini ni mmoja kati ya wachezaji wa Brazil watakaoshirikiOlympic.
0 comments:
Post a Comment