Recent

JIFUNZE MAMBO MBALIMBALI YATAKAYOKUPA MAARIFA NA UJUZI MAISHANI

Thursday, 4 August 2016

Je wajua? TV1 Kuonyesha Ligi Kuu ya Uingereza Bure, Unajua idadi za mechi zitakazooneshwa kwa wiki?


Kituo cha Televisheni nchini, TV1 kimezindua kampeni yake inayokwenda kwa jina la Toroka Uje ambayo inawaletea watazamaji wake matangazo ya bure ya mechi zote za Ligi Kuu ya Uingereza maarufu kama English Premier League zitakazoanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 13 mwaka huu.

Akizungumzia kampeni hiyo Meneja Mkuu wa TV1, Joseph Sayi alisema kuwa Watanzania kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitumia pesa nyingi kuangalia ligi hiyo maarufu duniani lakini kupitia TV1 ambayo inapatikana kwenye king’amuzi cha Startimes, Watanzania watakuwa wakitazama mechi hizo bure bila gharama yoyote.


Naye Meneja Masoko wa TV1, Gillian Rugumamu aliongeza kuwa mbali na watazamaji wa TV1 kufurahia mechi hizo ambazo zitarushwa kuanzia mechi ya kwanza hadi ya mwisho wa ligi, pia wamejiandaa kukutana na watazamaji wa TV1 kupitia michezo mbalimbali, matamasha na mashindano yatakayokuwa na zawadi mbalimbali zikiwemo vifurushi vya king’amuzi cha Startimes na nyingine kibao.


Akizungumzia kuhusu kampeni hiyo ya Toroka Uje, Mkuu wa Uzalishaji vipindi wa TV1, Mukhsin Mambo, alisema kuwa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tarehe 10 mwezi huu kitakuwa katika siku tatu ambapo kutakuwa na mijadala ya kandanda, mpira laivu na uchambuzi kuhusu mechi zijazo ambapo uchambuzi huo utaongozwa na wachambuzi wakubwa akiwemo Dr Leaky Abdallah na Ally Kashushu.


Aidha Meneja Masoko wa Startimes, Damien Li aliwahakikisha Watanzania kuwa Startimes haitaongeza bei ya vifurushi wala kutoza chochote kwa watazamaji wa Ligi hiyo kupitia TV1 kwa kuwa ni bure kabisa.

0 comments:

Post a Comment