Habari ndugu JOSEPH MIHANGWA?Mimi ni miongoni mwa wadau wakubwa wa
makala zako katika gazeti la RAIA MWEMA zinazoitwa NASAHA ZA MIHANGWA.Katika
nakala ya gazeti hili ya tarehe 03/04/2013 uliandika mada iliyokwenda kwa jina
la MAHAKAMA YA KADHI NA UZANDIKI WA WANASIA UCHARA.Kuna hoja kadha ambazo
ulijaribu kuzizungumzia katika makala hii kama ifutavyo;
i)Mahakama ya
kadhi na ofisi ya kadhi kugharamiwa na serikali
ii)Mahakama zetu
zimepewa uwezo wa kusikiliza kesi na kuamua kwa haki bila ubaguzi
iii)Kuruhusiwa kwa
misingi ya kidinikatika jamiiya kawaida hupelekea mifarakano na mitafaruku
inayoweza kutishia ustawi wa
jamii.
iv)Madai ya kidini
huwa na ajenda ya siriukafananisha na chui ndani ya ngozi ya kondoo na ukatoa
mafano yale yaliyotokea Algeria
na India.
v)Je taasisi hiyo
haitaenda kudai mfumo mpya wa kidini kuhusu elimu,sayansi,
technolojia,mabenki,bima na uhusiano wa kimataifa ili kukidhi matakwa ya
sehemu moja ya jamii kwa misingi ya dini?
Kimsingi yapo mengi uliyoyazungumzia kwenye makala yako na kuyatolea
ufafanuzi lakini hayo ni machache mbayo nimeona kuyatolea maelezo ili nijaribu
kukufanulia na pengine utaweza kunielewa na kupata ufahamu mpana juu ya
mahakama ya kadhi.Vilevile uweze kuandika vizuri juu ya hili kwa mustakabali wa
taifa na watu wake.
Kwahiyo kila namba ya hoja hapo juu itawakilishwa na maelezo
ya namba hiyohiyo hapa chini;
i)Kuhusu
serikali kugharamia shughuli za kadhi na ofisi yake-Ni kwamba serikali
kugharamia shughuli za kidini hapa nchini si mara ya kwanza wala si jambo la
kushangaza ila inawezekana likawa la ajabu na la kushangaza kwa
WAISLAMU,Kwasababu ni aghalabu sana kwa serikali kufanya hivyo.Unakumbuka mwaka
1992 serikali ilipo iingia mkataba na taasisi za kidini yaani TEC na
CCT?Mkataba uliokenda kwa jina la MEMORANDUM OF UNDERSTANDING (MOU). Katika
mkataba huo serikali inawajibika kugharamia huduma za jamii za WAIKRISTO kama
vile shule za seminary na hopsitali za waikristo.Gharama zinazotolewa na
serikali ni za mishahara kwa wafanya kazi, marekebisho ya taasisi hizo na mambo
mengine yote ambayo yanahitajika gharama ya fedha .
Kwahiyo
kuhusu gharama ya uendeshaji wa ofisi ya kadhi ni wajibu wa serikali na si
swala la ajabu hapa nchini kwetu.
ii)Kuhusu uwezo
wa mahakama za serikali kusikiliza kesi na kuamua kwa haki bila ya ubaguzi-ni
kweli kwamba mahakama zetu zimepewa uwezo wa kusikiliza kesi na kuamua kwa haki
lakini nadhani umeshindwa kuelewa vizuri kuhusu mahakama ya kadhi , yenyewe
inashughulika ndoa,talaka,mirathi na mahusiano baina ya waislamu wala haingilii
watu wasiokua waislamu na haihusiki na kesi zilizonje ya hizo.
Hivyo basi
kwakua serikali inaruhusu watu wake kufunga ndoa kufuatana na misingi ya dini
zao basi haina budi kuwaachia raia wake uhuru wa kuendesha taratibu za ndoa zao
kufuatana na misingi ya dini yao, kwasababu haiezekani ndoa ifungwe msikitini
chini ya Shekhe alafu matatizo yanayohusu ndoa yakitokea yakashughulikiwe
kwenye Mahakama za serikali ,badala yake matatizo yote yanayohusiana na
ndoa,talaka na mirathi kwa waislamu yashughulikiwe na Kadhi.
Zipo baadhi
ya nchi ambazo zina mahakama za serikali na zina uwezo wa kuendesha na
kusikiliza kesi na nyengine zina idadi ndogo za waislamu lakini bado zimewapa
waislamu uhuru wa kuwa na mahakama ya kadhi, Kwamfano;
*Kenya katika
katiba yao ibara ya 66(3) wanaruhusu mahakama ya kadhi
*Uganada ambayo
ina 12% ya waislamu lakini katika katiba yao ibara ya 129 inaruhusu mahakama ya
kadhi
*Gambia katika
katiba yao ya pili (1997) ibara ya 120(b) inaruhusu mahakama ya kadhi
*Nigeria katika
katiba yao(Federal republic of Nigeria 1999) ibara ya 262(2) na 277 inaruhusu
kadhi
Sasa hizo ni
baadhi ya nchi za kiafrika ambazo pamoja na ubora wa mahakama zake lakini zimewapa
uhuru waislamu wa kufuta sheria zake katika maswala ya ndoa,talaka, na mirathi
.Itakua Tanzani ambayo mahakama zetu zina mlundikano wa kesi na maamuzi
yasiyosthili yanayowafanya watu wasionacho ndio wahukumiwe kwa kukosa lakini
mafisadi wanaoiba mabilion ya ya fedha kuishia mtaani kwa kushinda kesi je ni
kweli mahakama zetu zina uwezo wa kuendesha kesi?
iii)Kuhusu
mifarakano na mitafaruku inayotokana na kuanzishwa kwa misingi ya kidini -Ni
kwamba matatizo hayo hayatokani tu kutokana na kuanzishwa na kwa mahakama ya
kadhi bali hutokana na matatizo mengi yanayowakabili wananchi katika jamii zetu
kwamfano halingumu ya maisha,matabaka kati ya walionacho na wasionacho,ukosefu
wa ajira na mengine mengi,ndiyo yanayochochea wananchi kupamabana na tabaka
tawala.
Lakini pia viongozi wa dini husababisha mifarakano katika
jamii na mauaji kwa mfano ;Mauji ya kimbari nchini Rwanda ,waliokamatwa kwa
kiasi kikubwa ni Maaskofu na wachungaji ambao ndio wachochezi wa kuu wa mauaji
hayo.Walikua wakitangaza makanisani kuwa wanaostahili kuongoza ni WATUSI na si
WAHUTU,hali hiyo ilipelekea wahutu wakikimbilia makanisani kuuwawa na hivyo
hukimbilia Misikitini kama sehemu yao ya amani.
Vilevile
umezungumzia kuhusu vita vya BIAFRA vya mwaka 1967,lakini kumbuka si tu
mifarakano ya kidini ndio yaliyopelekea vita hivyo bali hata kauli za baadhi ya
viongozi wa Afrika zilizokua zikichochea Kujitenga kwa taifa hilo zilipelekea
vita hivyo kwamfano;Mwl. Nyerere alikuwa akichochea kujitenga kwa taifa
hilo.Haya yalisemwa na Jenerali Ulimwengu katika kipindi cha Malumbano ya hoja.
iv)Kuhusu madai ya
kidini kuwa na ajenda ya siri-Ni kwamba katika madai haya ya mahakama ya kadhi
sisi waislamu wa Tanzania sio wa kwanza kudai bali zipo nchi nyingi ambazo
zilianza kudai na kufanikisha kupata mahitaji hayo kama nilivyo kuonsha hapo juu.Na
katika nchi za jirani yani Kenya na Uganda huu mfumo wa mahakama wanao na ni
zaidi ya miaka 15 na haijawahi kutokea hata siku moja vurugu zilizosababishwa
na uanzishwaji wa mahakama hiyo na wala ajenda yoyote ya siri ambayo
imeziathiri nchi hiyo kutokana na mahakama ya kadhi. na badala yake ni amani na
utulivu katika uendeshaji wa mahakama hiyo.
Kwa hiyo sisi
waislmu wa Tanzania hatuna ajenda yayate ya siri kwa serikali wala taifa hili
juu ya uanzishwaji wa mahakama ya kadhi ,isipokua tunataka haki yetu ya msingi
katika mirathi ,ndoa na talaka.Mbona Tanzani ni miongoni mwa nchi mbili barani
Afrika ambazo zina ubalozi wa Vatikan ?
Lakini nchi nyingi za kiafrika hazina ubalozi huo na
waislamu wa nchi hii hatujalalamika kuwa uwepo wake ni ajenda ya siri ya KANISA
KATOLIKI?
v)Hatuna haja ya
kwenda kudai mfumo mpya wa kidini kuhusu elimu,sayansi,teknolojia na mengine
ambayo umeyasema kwa sababu;
ELIMU-Tunazo
shule zetu za msingi na za sekondari ambazo zinatoa elimu kulingana na mfumo wa
kiislamu,sio nyingi kama za kwenu lakini hizohizo chache tunazo kwa mfano;Shule
ya sekondari ya kiislamu Ubungo,Shule ya sekondari ya kiislamu
Kirinjiko,Luqmani,Ridhwaa,Kinondnoni,ununio pamoja na nyengine nyingi.Vile vile
tunacho Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro ambacho kinatoa elimu kwa misingi ya
kiislamu,vyote ni vyombo muhimu katika
kutoa elimu kwa vijana wetu kwa mfumo wa kiislamu,pia zipo taasisi nyingi za
elimu ambazo zinashughulika na mfumo wa elimu ya kiislamu na elimu ya kawaida.
MABENKI NA
BIMA-Pia tunazo taasisi zetu za fedha ambazo zinatoa huduma kwa misingi ya
kiislamu.Kwamfano;
Amana Bank pamoja na benki nyengine za kawaida ambazo zina
mfumo wa kiislamu katika baadhi ya huduma zake kwa mfano;Stanbik Bank na
Natinal microfiance Bank(NMB).
SAYANSI NA
TEKNOLOJIA-Pia tuna taasisi za teknolojia kama Redio za kislamu mfano;Radio
Imani,Kheri,Sauti ya kuran na Tv Imani pamoja na nyengine nyingi zinazochangia
kwa kiasi kikubwa katika kuwaelimisha waislamu.Zipo pia Hospitali kama nile
Aljumaa Hospital ya Daresalama(Karoakoo)na Ahmaddiya Hospital ya Morogoro na
nyengine zikuzitaja ambazo hutoa huduma ya afya kwa waislamu na wasiokua
waislamu kwa taratibu na mfumo wa dini yetu
Katika mwezi wa
03 mwaka huu ,Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dr. Jakaya Mrisho
Kikwete alifanya ziara katika Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro ambapo alifungua
jengo la sayansi na ujenzi wa jengo jipya la Teknolojia ya habari (ICT) ambalo
litakapokamilika litashughulikia utoaji wa teknolojia ya habari kwa waislamu
hapa nchini.
Hivyo
hatuna sababu ya kiuanzisha mfumo mpya kuhusu hizo sekta ulizozitaja isipokua
tunachangamoto ya kuziendeleza ili tuweze kukabiliana na changamoto za waislamu
katika nchi hii pamoja na kutopata msaada kutoka serikaini lakini taratibu
ishallah tutafika tunapodhamiria kufika.
Tulichokikosa sisi waislamu wa nchi ni uhuru wa
kushughulikia wenyewe kesi zetu zinazohusu ndoa,talaka na mirathi kwa misingi
ya uislamu.
Hivyo mi nadhani ungetumia muda
wako mwingi katika kuyazungumzia matatizo ambayo watanzania yanawapata katika
nchi hii.Kama vile unongozi mbaya,rushwa,maradhi,umasikini uliokithiri,ubovu wa
miundombinu yetu,tatizo la ajira,huduma mbovu za afya na kufeli kwa wanafunzi
wetu.Na mengineyo mengi amabyo ungewagusa watanzania moja kwa moja ,na sio
kuanza kuponda mahitaji ya dini za wenzio kwani yatakupelekea kudharaulika na
watu na kuonekana kama mchochezi wa vurugu za vurugu za kidini kwasababu tayari
swala la mahakama ya kadhi lishakubaliwa na serikali kwani ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya
chama cha mapinduzi ,na lipo katika hatua ya awali ya utekelezaji.
0 comments:
Post a Comment