Recent

JIFUNZE MAMBO MBALIMBALI YATAKAYOKUPA MAARIFA NA UJUZI MAISHANI

Wednesday, 20 July 2016

Fahamu kwa undani historia ya IDD AMIN DADA

Idi Amin Dada alizaliwa 1923 na alifariki mwezi wa nane 2003 alikua raisi wa tatu wa Uganda, alitawala 1971 mpaka 1979. Amin alijiunga na jeshi la kikoloni la Mwingereza likitumikia Kenya na Uganda. Amin alipanda haraka ngazi kufikia cheo cha umeja wakati huo ni baada ya uhuru ikijulikana kama jeshi la Uganda, alikua kamanda kabla ya kufanya mapinduzi mwaka 1971 na kumpindua Milton Obote. Baadae alijipandisha cheo kua field marshal akiwa raisi.


Amin hakuwahi kuandika kitabu cha historia yake wala hakuwahi kumruhusu mwandishi yeyote kuandika habari ya maisha yake. Hii inamaanisha hakuna uhakika ni lini na ni wapi alizaliwa. Maandishi mengi kuhusu amini yanaeleza alizaliwa Koboko au Kampala mnamo 1925. Habari nyingine zisizo na uhakika zinaeleza Amin alizaliwa 1923 na nyingine zinasema 1928. Mtoto wa Amin aitwae Hussein anasema baba yake alizaliwa Kampala mnamo mwaka 1928. Fred Guweddeko wa Makerere University, anasema Idi Amin ni mtoto wa Andreas Nyabire alieishi kati ya 1889 na 1976. Nybire ni mmoja wa kabila la Kakwa ambalo lilibadili dini kutoka Ukatoliki kwenda Uisilamu mwaka 1910 na kubadili jina kuwa Amin Dada. Yeye mwenyewe alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa.

Iddi Amini alitengwa na malezi ya baba akiwa mdogo, Idi Amin alikua na mama yake katika kijijini kwa shughuli za kilimo kaskazini magharibi mwa Uganda. Guweddeko anasema mama yake Amin aliitwa Assa Aatte alizaliwa 1904 na alifariki 1970, na alikuwa mganga wa kienyeji aliewatibu familia ya kifalme ya Buganda kati ya wateja wake. Amin alijiunga na shule ya Kiislam ya Bombo mwaka 1941, aliacha shule akiwa na elimu ya darasa la nne kwa elimu ya Mwingereza na alifanya vibarua kabla ya kujiunga na jeshi la Mwingereza na kuwa ofisa wa jeshi.


Amin alijiunga na Jeshi la Mwingereza la King's African Rifles (KAR), mwaka 1946 kama msaidizi wa mpishi. Baadae alidai mwenyewe kuwa alilazimishwa kuingia jeshini wakati wa vita kuu ya pili ya dunia World War II na aliwahi kupelekwa Burma. Alihamishiwa Kenya kwa mafunzo maalumu mwaka 1947 na alikua sehemu ya kikosi cha 21 ca tattaalion Gilgil, Kenya mpaka 1949. Mwaka huo kikosi chake kilikwenda kupigania Kenya zidi ya Wasomali vita ya Shfta. Mwaka 1952 Brigadia yake ilipigana dhidi ya Mau Mau wa Kenya na alipandishwa cheo kuwa koplo mwaka 1953.

Mnamo mwaka 1959, Amin alipewa cheo cha Afande Afisa Mteule (warrant officer), hiki kilikua cheo cha juu zaidi kwa askari Mweusi wa |Kiafrika katika jeshi la Mkoloni Mwingereza wakati huo. Amin alirudi Uganda mwaka huo huo, na mwaka 1961 alipewa cheo cha luteni na kuwa mmoja kati wa Waganda wawili kuwa na maafisa maalum (Commissioned Oficers). Alipangiwa kusuluhisha mapigano ya Karamojong na kabila la Turkana la Kenya uliohusu ngo'mbe. Kufuatia uhuru wa Uganda kutoka kwa Mwingereza, Amin alipandishwa cheo kuwa kapteni na 1963 kuwa meja. Aliteuliwa kua Afisa wa pili wa majeshi ya Uganda mwaka 1970.


Amin alikuwa mwanamichezo mzuri sana wa enzi zake kote katika Jeshi la Mwingereza na Jeshi la Uganda. Akiwa na urefu wa sentimeta 193 au futi 6 na inchi 4 na tambo lililo jaa, hivi vilimfanya kuwa nyota katika michezo. Alikuwa mwanamasumbwi wa uzito wa juu, muogeleaji, pia alicheza rugby kwa uwezo wa hali ya juu. Katika miaka ya 1950 alichezea Nile RFC. Kuna usemi wa mjini kuwa alichaguliwa kama mchezaji wa ziada kaitka michezo ya Afrika Mashariki kwenye mechi dhidi ya British Lions. Amin hatahivyo hakutokea kwenye picha za mchezo huo wala jina lake halikua kwenye orodha ya wachezaji. Kutokana na maongezi na askari wenzake wa kizungu Amin alianza kujenga ushabiki na timu ya mpira ya Hayes, ushabiki huo uliendelea maisha yake yote.


Mwaka 1965, Waziri mkuu Milton Obote na Amin walishutumiwa katika mpango wa kuingiza meno ya tembo na dhahabu nchini Uganda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mpanga huu mbao Generali Nicholas Olenga, rafiki wa aliekua kiongozo wa serikali ya Kongo Patrice Lumumba, alikuwa mmoja wa washiriki ili kusaidia majeshi ya upinzani dhidi ya serikali ya Kongo kwa siri kufanya biashara ya dhahabu na meno ya tembo kubadishana na silaha na mpangaji mkuu wa mpango huu akiwa Amin kwa Uganda. Bunge la Uganda lilidai utafiti ufanyike dhidi ya shutuma hizi. Mwaka 1966 Obote alifuta sherehe za kiraisi zilizofanywa na Mfalme Kabaka Mutesa II wa Buganda, na kujitangaza kuwa yeye mwenyewe ni raisi na kumtangaza Amin kuwa Kiongozi wa Majeshi. Amin aliongoza mapigano dhidi ya jumba la kifalme la Kabaka na kumfanya Kabaka na familia yake kukimbilia hifadhi ya ukimbizi nchini Uingereza ambako aliishi mpaka mauti yanamkuta mwaka 1961.


Amin alianza kuingiza watu wa kabila lake la Kakwa na Lugbara kutoka Kusini mwa Sudani na makabila mengine kutoka Magharibi mwa eneo la Nile linalopakana na South Sudan. Watu wa Sudani ya Kusini walihamia Uganda tangia karne ya 20, walikuja kujiunga na jeshi la mkoloni. Jeshi la Amin lilijaa watu wa Sudan ya Kusini na wengi wao waliishi katika nchi zote mbili.

Milton Obote ndiye aliyekuwa raisi wa pili wa Uganda ambae alipinduliwa na Idi Amin mnamo mwaka 1971. Ugomvi kati ya Obote na Amin ulianza baada ya Amin kuwa na nguvu na kubwa jeshini kutokana na kuajiri watu wa kabila lake. Hii pia ilisaidia kusaidia majeshi ya waasi wa serikali ya Sudani ya Kusini pia jaribio la kumuua Obote mwaka 1969. Oktoba 1970 Obote alichukua madaraka makubwa jeshini na kumpunguzia Amin nguvu aliyoanza kuifurahia jeshini kwa miezi michache.

..................Itaendelea..................

0 comments:

Post a Comment