Recent

JIFUNZE MAMBO MBALIMBALI YATAKAYOKUPA MAARIFA NA UJUZI MAISHANI

Saturday, 23 July 2016

Serikali ya Kenya yamtimua Koffi Olomide Kwa kumpiga mnenguaji wake wa kike



Serikali ya Kenya mapema leo imechukua uamuzi wa kumtimua mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Koffi Olomide kufuatia tukio alilolifanya jana la kumpiga mnenguaji wake wa kike katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Taarifa za kuaminika kutoka jijini Nairobi zimeeleza kuwa Koffi Olomide alikamatwa na polisi jana majira ya saa nne usiku alipotoka kufanya mahojiano na Citizen TV.

Mwanasheria wa Koffi Ollomide, Prof George Wajackyah amesema kuwa tangu walipokamatwa jana usiku walitunzwa kama wanyama na kwamba Serikali ya Kenya imewatimua na kuwarudisha Congo hata bila kuwa na passport zao.

Alisema walitimuliwa kwa nguvu na kusindikizwa leo asubuhi hata bila kupewa nafasi ya kwenda mahakamani Jumatatu kama walivyokuwa wanatarajia.

Koffi Olomide alitua nchini humo jana akitarajia kufanya tamasha kubwa leo lakini limeota mabawa.

Jeshi la mitandao ya kijamii la Wakenya ambalo linatajwa kuwa na nguvu zaidi Afrika Mashariki hasa kupitia twitter kuanzia jana lilimshambulia vikali Koffi Olomide kwa hatua yake ya kumtwanga teke mnenguaji wake jijini Nairobi, katika tukio ambalo lilinaswa kwenye kamera.

0 comments:

Post a Comment