Sunday, 17 July 2016
Vodacom yagawa tuzo mbalimbali za Premier league msimu wa 2015/2016
Wadhamini wa league kuu ya Tanzania Vodacom usiku huu wamekabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa tuzo za league hiyo kwa category zifuatazo.
1. Mshindi wa nne 4
Katika kategoria hii timu ya Prison ya mbeya iliyoshika nafasi hiyo imejinyakulia sh. Mil. 23
2. Mshindi wa tatu 3
Katika kategoria hii timu ya Simba iliyoshika nafasi hii ya imejinyakulia sh. Mil 29
3. Mshindi wa pili 2
Katika kategoria hii timu ya Azam iliyoshika nafasi ya pili imejinyakulia sh. Mil 40
4. Mshindi wa kwanza 1
Mabingwa wa league kuu ya vodacom Tanzania Dar es salaam Young Africa wamejinyakulia sh. Mil 81.
5. Timu yenye nidhamu bora
Tuzo hii imechukluliwa na timu ya Mtibwa ya mkoani morogoro iliyojinyakulia kitita cha sh. Mil 17
6. Mwamuzi bora
Tuzo hii i9mechukuliwa na Ngole Mwangole aliyejinyakuliwa sh. Mil 5.7
7. Kocha Bora
Tuzo hii imechukuliwa na kocha mkuu wa timu ya Yanga PLUIJIM aliyejinyakulia sh. Mil 8.
8. Goli kipa bora
Tuzo hii imechukuliwa na goli kipa wa Azama fc Aishi Manula ambaye amejinyakulia sh. 5.7
9. Goli bora
Tuzo hii imechukuliwa na kiungo mshambuliaji wa Wekundu wa msimbazi SIMBA Ibrahim Ajibu aliyejinyakulia sh. Mil 3.
10. Mchezaji bora wa kigeni
Tuyo hii imechukuliwa na kiungo mkabaji wa YANGA Thaaban Scara Kamusoko aliyejinyakulia sh. 5.7.
11. Mchezaji bora chipukizi
Tuzo hii imekwenda kwa beki wa kushoto wa Simba Mohemmed Hussein aliyejinyakulia sh. Mil 4
12. Mchezaji bora wa msimu
Tuzo hii imekwenda kwa beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul aliyejinyakulia sh. 9/
0 comments:
Post a Comment