Recent

JIFUNZE MAMBO MBALIMBALI YATAKAYOKUPA MAARIFA NA UJUZI MAISHANI

Tuesday, 19 July 2016

Fahamu ukweli juu Paji la uso na siri ya jicho la tatu



Hutaamini utakachogundua hapa kuhusu paji lako la uso...hapa ndio asili ya neno kipaji ilipatikana..hapa napo ni lango hapa ndio penye njia ya kuingilia mlango wa sita baada ya ile mitano. Hili ni jicho la ndani jicho lisioonekana.lango kuu la kiroho.

Tutaenda kwa mitazamo yote ya kidini na kiimani, kisayansi, kihisia na hata kwenye nguvu za giza.

1. Third Eye - Thalamus - Eye of Horus


Hapa ni kwa mtazamo wa kisayansi nafikiri ni kwenye somo la anatomy kuhusu ubongo, jicho la tatu linaonekana katikati ya ubongo (zingatia katikati) vertebrate brain hapo ndio zinapozalishwa homoni za kulaza au kuamsha hisia maono usingizi nk.

2. Mathematics


Katika ulimwengu wa mahesabu na hesabu, wanamahesabu kwenye ishu za ratio cos na tan watatusaidia hapa.

4. Baptism & Sijda



Kiimani katika ukristo, kwenye ubatizo alama ya msalaba kwenye paji la uso ndio hukamilisha tendo na kuwa Mkristo kamili sasa.. Lakini pia ukisoma kitabu cha ufunuo na habari za kutiwa Muhuri katika paji la uso utafahamu zaidi..

Kwenye Uislam tunajua nini maana na umuhimu wa swala tano na kuthibitisha uchaji wako katika swala tano ni sigida kwenye paji la uso.

5. A kiss on the Forehead

Kwenye mahusiano busu kwenye paji la uso ni tofauti kabisa na mabusu ya sehemu nyingine yoyote.

6. FREEMASONRY

Kwenye imani za mpinga Kristo freemason satanism nk alama yao kubwa ni jicho la tatu

7. SEVERE PUNISHMENTS (WATERBOARD)


Kwenye adhabu na mateso mbalimbali paji la uso hutumika kuleta adha ya ajabu mwilini... Mateso ya water board ni mfano mmojawapo. Unalazwa chini unafunikwa kitambaa usoni kisha unamwagiwa maji.. Ni aina ya adhabu isiyoumiza mwili bali inayoumiza hisia.

8. Michezoni:
Kwenye mchezo wa ngumi alama za juu ni zile ambazo zinaangukia kwenye paji la uso.

Nimejaribu kwenda na picha kuokoa ufafanuzi wa maneno mengi... Tunaishi kwenye ulimwengu wa ajabu mno.. Tunashiriki kitu hicho hicho lakini kwa maana matumizi na mitizamo tofauti. Tunafundishwa kutolala chali kuepuka ndoto za mauzauza na majinamizi kumbe siri ni jicho la tatu jicho la maono.

Manabii na watenda miujiza hupenda kuwapuliza ama kuwashika watu penye paji la uso na kifuatacho hapo ni mzinga kama si kupiga kelele... Baadhi ya tiba mbadala hutumia paji la uso kama lango la uponyaji.

Wahindi na wahindu kwenye imani zao hujipaka rangi katikati ya macho kama sehemu ya ibada nk.

Jaribu kutafakari kwa hatua hiki kinachoitwa jicho la tatu, paji la uso, imani yako na maisha yako ya kila siku... Mwishowe tunaweza kujikuta tunaabudu paji la uso kwa muktadha tusiojua.




0 comments:

Post a Comment