Recent

JIFUNZE MAMBO MBALIMBALI YATAKAYOKUPA MAARIFA NA UJUZI MAISHANI

Thursday, 21 July 2016

Muendelezo wa historia ya Idd Amin Dada

                                                                  Sehemu ya pili



Milton Obote.


Alipogundua kuwa Obote anampango wa kumfunga kwa hujuma ya kupotea kwa pesa za jeshi, Amin alimuwahi kwa kumpindua mnamo 25 January, 1971. Obote alikua katika kikao cha Jumuia ya Madola nchini Singapore. Wanajeshi waliomuunga mkono Amin walizingira kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Entebe, walizingira nyumba ya Obote na walifunga barabara. Walitangaza redioni kuwa serikali ya Obote haiko madarakani kwa shutuma za kutumia madaraka vibaya na ufujaji wa mali pia iliendesha serikali kwa upendeleo, hasa kupendelea watu wa mkoa wa Lango. Watu walisikika wakishangilia kwenye barabara za Kampala, Idi Amin alisema wazi kuwa yeye si mwanasiasa bali yeye ni askari mwanajeshi. Alisema pia uongozi wake utakuwa ni wa muda mpaka hapo serikali ya kidemokrasia itakapopatikana ki halali. Amin aliahidi kuwafungua wafungwa wote wa kisiasa.

Amin alimfanyia mazishi ya kitaifa Mfalme Kabaka wa Buganda na raisi wa kwanza wa Uganda Bwana Edward Mutesa aliefia ukimbizini nchini Uingereza. Mazishi haya yalifanyika mwezi April 1971, kitendo hiki kiliwapendeza sana Waganda. Pia aliwafungua wa kisiasa kama alivyoahidi na aliahidi kuleta uchaguzi huru na wa haki katika muda mfupi.





Mazishi ya kitaifa ya Sir Edward Mutesa, Mfalme wa Buganda na raisi wa kwanza wa Uganda 1971.

Wiki moja baada ya mapinduzi 02 February 1971 Amin alijitangaza kuwa yeye ndiye rais wa Uganda, Mkuu wa Majeshi pia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa serikali ya Uganda. Aliitisha kikako cha maofisa wa jeshi, yeye mwenyewe akiwa mwenyekiti na aliweka sheria za jeshi juu ya sheria za nchi. Maafisa wa jeshi walipewa madaraka makubwa serikalini na aliunda baraza la mawaziri ambalo lilifuata sheria na nidhamu za jeshi. Ikulu aliibadilisha jina kuwa The Command Post na alifuta idara ya upelelezi ya serikali iliyopita na kuipa jina State Research Bureau (SRB), ikiwa na makao makuu kando ya Kampla eneo la Nakasero, kwa kifupi hii ndio ilikua kitengo cha utesaji unyongaji na uuaji kwa kipindi chote cha utawala wa Amini.




Obote alikimbilia Tanzania, alipewa hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa na Rais Julius Nyerere. Obote alijiunga na Waganda 20,000 waliokimbia nchi yao na walifanya jaribio la kumpindua Amin mwaka 1972, jaribio hili lilishindwa kutokana na mipango mibovu.

Amin alikasirishwa sana na jaribio hili la kuvamia nchi yake lililopangwa na wakimbizi wa kisiasa. Aliwaondoa jeshini wale wote waliomuunga Obote hasa wale wa kabila la Acholi na Lango. Wanajeshi wa Acholi na Lango waliuwawa kikatili katika kambi ya Jinja na Mbarara. Mwanzoni mwa mwaka 1972 wanajeshi takriban 5,000 wa Acholi na Lango na raia wasio julikana idadi kamili waliuwawa na wengine walipotea na hakuna aliejua walikwenda wapi mpaka leo hii. Wahanga wa jaribio hili walikua pamoja na viongozi wa dini, waandishi wa habari, viongozi wa kuu serikalini, wasanii, wanasheria, majaji, wanafunzi, wanafalsafa, wanauchumi, majambazi walioshukiwa na raia wa kigeni. Katika hali hii visa vya kikatili vilifanyika na miili mingi ilitupwa mto Nile.


Mauaji haya, yalichochewa haswa na ukabila, sababu za kisiasa na uchumi, na yaliendelea kwa muda wote wa miaka nane wa utawala wa Idi Amin. Hakuna mtu anaejua idadi halisi ya watu waliouwawa. Jumuia ya kimataifa ya wanasheria inakisia idadi ya watu waliouwawa kuwa ni kati ya 80,000 na 300,000. Idadi ya wakimbizi na Amesty International inakisia idadi ya waliouwawa kuwa inafika 500,000. Katika waliouwawa alikuwa Benedicto Kiwanuka, ambae alikuwa waziri mkuu na Mwanasheria Mkuu Janani Luwum, Askofu wa kanisa la Anglicana Joseph Mubiru, Gavana wa benki kuu ya Uganda Frank Kalimuzo, Makamo wa mkuu wa Makerere University Byron Kawadwa, na mwandishi ns mtunzi pia mawaziri wawili kutoka kwenye serikali yake Erinayo Wilson Oryema na Charles Oboth Ofumbi.

Amin aliajiri watu wengi kutoka kabila lake la Kakwa na watu kutoka Sudani ya Kusini. Kufikia mwaka 1977 watu hawa walikuwa asilimia 60 ya magenerali wa jeshi na aslimia 75 za mawaziri. Wakati huo huo, Waislamu walikuwa asilimia 80 katika serikali ingawa kwa idadi ya raia wa Kiislamu ilikuwa asilimia 5 tu nchi nzima. Hii inajidhihirshia sababy kwanini kulikua na majaribio nane ya kumpindua Amin katika miaka nane aliyotawala. Askari wengi wa Amin walitokea Sudani ya Kusini na Kongo na asilimia 24 tu ya askari walikuwa Waganda hawa pia wengi wao walikuwa kabila la Kakwa na ni Waislamu.




'Tunalengo la kutengeneza Mganda wa kawaida kuwa mwongozaji wa maendeleo yake na ju ya yote afurahie utajiri wa nchi yake. Nia yetu ni kuhamisha uchumi wa Uganda uwe mikonini mwa Waganda kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu.' Idd Amin.

Mnamo August 1972, Amin alitangaza vita ya uchumi, aliweka policies pamoja kutaifisha ma mali zote azilizomilikiwa na Wazungu na Wahindi. Wahindi wapatao 80,000 wengi wao walitokea wengine walizaliwa Uganda wazazi wao walikwenda Uganda miaka mingi iliyopita wakati Uganda ikiwa koloni la Mwingereza, wengi wao walikua na biashara kubwa na zilikuwa moja ya uti wa mgongo wa uchumi wa taifa. August 04/08/1972, Amin aliwafukuza Wahindi wapatao 60,000 ambao ni raia wa Uganda. Wengi wao walikua na passport ya Mwingereza. Baadae zoezi hili lilibakisha Wahindi wenye taaluma kama daktari, wanasheria, walimu na wengineo. Karibia Wahindi 30,000 walihamia Uingereza. Wengine walikwenda Canada, Autralia, India, Kenya, Pakistani, Sweden, Tanzania na Marekani. Amin alitaifisha biashara zote na kuwapa wale waliomuunga mkono. Wengi wao hawakuwa na uwezo wa kuendesha biashara, matokeo yake nyingi zilikufa na uchumi kutikisika.




Wahindi wakiwa wanaondoka Uganda 1972.


Mwaka 1977, waziri wa afya Henry Kyemba ambae pia alifanya kazi katika serikali ya Obote aliachia madaraka na kwenda Uingereza kuishi kama mkimbizi. Aliandika nakala isemayo Nchi ya Damu.




Amin alipata ushirikiano mkubwa kutoka nchi za Magharibi kama vile Uingereza, Ujerumani, Israel, kipindi hiki kilikua ni cha vita baridi kati ya nchi za kijamaa na kibepari, Obote alishaonesha nia ya kufuata siasa za kijamaa na hili halikuwafurahisha sana watu wa Magharibi. Obote alitaifisha makamputni 80 ya waingereza na hii ilionyesha kabisa nia yake ya kuifanya Uganda kuwa Soviet Union. Kutokana na nidhamu ya Jeshi la Mwingereza alilojiunga nalo Amin, alikuwa na imani kubwa na Waingereza. Wengine wanasema Waingereza walimtengeneza Amin kuwa mtawala wa Uganda tangu 1966.




Amin aliwaamuru wafanyabiashara Waingereza wambebe kama mfalme huko Kampala.

Kufuatia kufukuzwa kwa raia wenye asili ya Kihindi nchini Uganda mwaka 1972 ingawa wengi wao walikua na hati za kusafiria za Uingereza lakini asili yao ilikuwa India, hivyo India mwaka huo ilikatisha mawasiliano ya kidiplomasia na Uganda, mwaka huo huo, Amini alitaifisha makampuni 85 ya Kiingereza. Mwaka huo huo Israel ambayo ilikua nchi mfadhili kwa silaha za kijeshi Uganda walichukizwa na maamuzi ya Amin.

Amin hakusikitika kwakua alimpata rafiki mpya mwenye uwezo wa fedha Muammar Gaddafi aliekua raisi wa Libya, Urusi ilimuahidi vifaa vya kijeshi. Amin alikemea kile alichoona si haki aliyotendewa na Israel wazi na hii ilipelekea Gaddafi kumpa msaada wa kifedha. Amin alijiandaa kuivamia kivita Israel kwa kutumia askari wa parachute, mabomu na silaha zenye sumu. Inaelekea Amin alipata ushirikiano mkubwa kwenye jambo hili, Urusi ilimpelekea silaha, Ujerumani Mashariki ilitoa mafunzo kwa askari wa upelelezi Uganda State Research Bureau, hizi ajensy mbili ziliogopewa sana ya Ujerumani Mashariki na ya Uganda. Wakati wa vita ya Tanzania na Uganda, Ujerumani mashariki alikanusha kabisa kujihusisha na Idd Amin.

IIn June 1973, Balozi wa Marekani nchini Uganda Thomas Patrick Melady, alipendekeza nchi yake kupunguza ushirikiano na Uganda. Balozi Melady alielezea serikali ya Amin kuwa ni ya kibaguzi, ya kikatili ya isiyotabirika, Marekani walifunga ubalaozi wao mjini Kampala. Kabla ya hapo CIA ilifanya kazi sana na serikali ya Amin ikisaidia kutoa silaha na mabomu kwa jeshi la Amin katika mipango mingi ya kijeshi na wanajeshi wa Uganda wakiwa watekelezaji.

Mnamo June 1975, Amin aliruhusu ndege ya shirika la ndege la Ufaransa iliyotekwa na vijana wa Popular Front for the Liberation of Palestine - External Operations (PFLP-EO) na watu wawili kutoka kikundi cha Ujerumani Revolutionare Zellento kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa Entebe. Entebe watekaji waliungana na watatu wengine hii inamaana Amin alijua mipango inavyoendelea. Baada ya hapo watu 156 ambao si Waisrael waliruhusiwa kuondoka, Wayahudi 83 na raia wa Israel na wengine 20 waliokataa kuwaacha pamoja nao alikua kaptani wa ndege na cabin crew waliwekwa mateka. Waisrael walifanya mpango wa kuwaokoa waliouita Thunderbolt (radi) Operation Entebe.

Kati ya 3-4 July, kikundi cha makomando wa Israel walikwenda kwa ndege na kuteka eneo la uwanja wa ndege Entebe, waliwaokoa karibu mateka wote. Mateka watatu walikufa wakati wa pambano na wengine kumi walijeruhiwa; watekaji 7 na askari 45 wa Uganda, pamoja na askari 1 wa Israel Yoni Netanyahu waliuwawa. Mateka wanne aliekuwa na umri wa miaka 75 Dora Bloch, bibi mzee Myahudi na Mwingereza alipelekwa hospitali kuu ya Mulago Kampala kabla ya kuanza kwa mashambulizi, aliuwawa wakati akiwa anarudisha fahamu hospitali. Tukio hili lilizidisha hali mbaya ya uhusiano na ilipelekea Uingereza kufunga Ubalozi wake Kampala. Uingereza ilipositisha uhusiano huo Amin alitangaza amewashinda Waingereza na alijipa title ya "CBE" kwa maana ya "Conqueror of the British Empire" kwenye majina ya vyeo vyake. Baadae Radio Uganda ikatoa vyeo vyote vya Raisi kama ifuatavyo; His Excellency President for Life Field Marshal Alhaj Dr. Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, CBE.

Uganda chini ya utawala wa Amin ilijenga jeshi lenye nguvu sana, hii ilikua tishio kwa nchi jirani ya Kenya. Mwanzoni mwa mwezi June 1975 maofisa wa Kenya walizuia shehena kubwa ya silaha zilizotengenezwa Soviet Union zikielekea Uganda katika bandari ya Mombasa. Hali kati ya Kenya na Uganda haikuwa nzuri kutokea hapo, Amin alisema anahakikisha ardhi ya Sudani ya Kusini na Magharibi mpaka kati kati ya Kenya vinarudi kuwa sehemu ya Uganda. Serikali ya Kenya ilijibu kwa kusema Kenya haitapunguza hata inchi moja ya mipaka yake. Amin aliamua kukaa kimya baada ya Kenya kupeleka wanajeshi na silaha katika mpaka wa Kenya na Uganda.

Baadae Idi Amin alitangaza kuwa Kagera ni sehemu ya Uganda, hii ilisababisha vita ya Uganda Tanzania ambayo ilimaliza utawala wa miaka nane wa Amin na hatimae Amin alikimbilia Libya na baadae Saudi Arabia ambako aliishi mpaka mauti yalipomkuta tarehe 18 August 2003.

Kufikia mwaka 1978, idadi ya watu waliomuunga mkono Amin ilipungua sana na alikua anakabiliwa na upinzani kutokana na kushuka kwa uchumi nchini Uganda pia miundo mbinu haikufuatiliwa. Askofu Luwum, na mawaziri wawili Oryema ana Oboth Ofumi mwaka 1977, waganda wengi walikimibia nchi yao. November 1978, baada ya makamu wa raisi Generali Mustafa Adrii kuumia katika ajali ya gari, wanajeshi wengi wa Amin walianza kuasina kukimbilia nchi jirani ya Tanzania, Amin alipeleka majeshi kupigana na wanajeshi wake walioasi katika mipaka ya Tanzanias Amin alianza kumshutumu rais wa Tanzania Julius Nyerere kwa kuanzisha vita na Uganda, Amin aliendelea kusema kuwa hata Kagera ambayo iko kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda ni sehemu ya Uganda, rais Nyerere alitangaza vita baada ya kauli hiyo..

Janurary 1979, Nyerer alituma majeshi ya Jeshi la Wananchi na kuanza mashambulizi, Jeshi la wananchi lilipata ushirikiano wa majeshi ya msituni yaliyokuwa yakimpinga Amin kama Uganda National Liberation Army (UNLA). Majeshi ya Amin yalipata kipigo kikali sana, pamoja na msaada mkubwa aliopata Amin kutoka kwa rais wa Libya Muammar Gaddafi, ilibidi Amin akimbie nchi kwa kutumia helikopta 11 April 1979 wakati Kampala iliposhikiliwa na majeshi ya Tanzania.

Amin alikimbilia kwanza Libya ambako aliishi mpaka 1980. Baadae familia ya kifalme ya watu wa Saudi Arabia walimpa hifadhi pia walimpa pesa nzuri tu ya kujikim. Kwa miaka mingi Amin aliishi kwenye maghofa ya ju ya hoteli ya Novotel barabare ya Palestine mjini Jeddahn.

Katika mahojiano yote Amin aliyoyafanya akiwa ukimbizini aliamini Uganda inamhitaji. Hakuonyesha masikitiko yeyote kwa aliyoyafanya wakati wa utawala wake. 1989 Amin alipanga kurudi Uganda kuongoza majeshi ya Kanali Juma Oris, alifika Kinshasa Zaire ambako Raisi Mobutu Sese Seko alimwamuru arudi Saudi Arabia.

Kifo chaa Idd Amin.
Mnamo 19 July, 2002, mmoja katika wake wa Amin Madina alieleza kuwa Amin ni mgonjwa mahtuti na anakaribia kukata roho katika hospitali ya Mfalme Faisal. Amin alikuwa na matatizo ya figo. Madina alimuomba rais Yoweri Museveni, aruhusu Amin arudishwe Uganda ambako ndiyo asili yake. Museveni alijibu kuwa Amin akirudi tu Uganda anashitakiwa kwa yote aliyoyafanya wakati wa utawala wake. Familia ya Amin iliamua kusimamisha mashine zilizomuongezea uhai akiwa hospitalidah. 16 August 2003 Amin alizikwa kwenye makaburi ya Ruwais Jeddah, yalikuwa mazishi ya kawaida.

Maisha binafsi ya Idi Amin.
Amin aliamni ndoa ya wake wengi na katika maisha yake aliishi na wanawake wasiopungua watano, watatu kati yao aliwaa talaka. Aliwaoa wake zake wawili wa kwanza Maryamu na Kay mwaka 1966. Mwaka uliofuatia alimuoa Nora na baadae alumoa Nalongo Madina mwaka 1972.



Malyam na Kay

Mwaka 1974 Amin alitangaza katika Radio Uganda kuwa amemuacha Malyamu, Nora na Kay. Malyamu alikamatwa baadae Tororo ambako ni mpaka wa Uganda na Kenya akiwa anakimbilia Kenya na jora la kitambaa. Baadae alihamia London ambako alifungua mgahawa London Mashariki (East London). Kay alifariki katika kifo cha kutatanisha katikati ya miaka ya 1970 na mwili wake ulikutwa ukiwa umekatwa katwa. Mora alikimbilia Zaire mwaka 1979 na hakuna anaejua habari zake zaidi.

Mwezi August 1975, wakati wa mkutano wa Wakuu wa Umoja wa nchi za Afrika (OAU), Amin alimuoa Sarah Kyolaba, bwana wa Sarah ambae aliishi nae kabla ya kukutana na amin alipotea na hakuonekana tena. Sarah alikua mcheza katika jeshi la Uganda, kikundi hicho cha jeshi kilitumbuiza wageni wa OAU baada ya sherehe kuisha mmoja alitunukiwa u firt lady. kufikia mwaka 1993, Amin alikua anaishi na watoto wake tisa wa mwisho na alikua na mke mmoja, Mama Chumaru ambae inasadikika alikua mke wa sita na mama wa watoto wake wanne wadogo. Mtoto wake wa mwisho alikua binti aliyepewa jina Iman alizaliwa 1992.




Harusi ya Sarah na Idi Amin iligharimbu shilingi million 2 za Uganda miaka hiyo.

Inasadikika mpaka mauti yanamkuta Idi Amin alijaliwa kupata watoto 45.


Ndugu wapenzi wasomaji wa BAHARI YA MAARIFA hapo ndio tumefikia mwisho wa makala yetu hii ya historia ya IDD AMINI DADA kwa maoni na ushari unaweza kutuma ili kuweza kuboresha mada zetu.




3 comments: