Sunday, 14 August 2016
Spika wa bunge Mh. Job Ndugai atoa ya moyoni kuhusu mwenendo wa bunge na serikali
Hii leo katika kipindi cha FUNGUKA kinachorushwa na Azam 2 ya Azama tv kulikuwa na mahojiano ya moja kwa moja katika mtangazaji Bw Tido Mhando spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na mbunge wa kongwa Mh. Job Ndugai.
Katika mahojiano hayo Mh. Ndugai amefunguka juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea katika taifa letu kisiasa, kijamii na kiuchumu.
Mh. Spika amesema kuwa kuhusu maandamano yanayotarajiwa kufanywa na wapinzani nchi mwezi ujao, hakuna haja ya kuandamana wala kuwa na mikutano ya hadhara baada ya uchaguzi na badala yake kama wana hoja yoyote kuhusu serikali wanapaswa kuiwasilisha bungeni.
Amesema pia kuwa, wengi wao ni wabunge katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hivyo wana fursa ya kuihoji serikali bungeni na sio kwenda kwa wananchi.
Pia amezungumzia kuhusu utoro wa baadhi ya wabunge bungeni, spika amewataka wabunge wa vyama vyote kuacha tabia hiyo kwani wametumwa kuwawakilisha wanachi wao. Lakini pia aliongezea kwa kusema tabia hii ya utoro wa wabunge haipo hapa Tanzania tu bali hata katika mabunge mengi ya nchi za kiafrika tabia hii ipo.
Alitolea mfano wa bunge la Kenya, kwamba kuna siku walihudhuria wabunge 12 tu. Hivyo amependekeza pengine kuwepo na mabadiliko ya sheria za bunge kuhusu mahudhurio ya wabunge bungeni.
Lakini pia amezungumzia posho za wabunge, spika ameeleza kuwa kumekuwepo na wabunge ambao wamemfuata mara kadhaa na kumwambia kuwa posho hazitoshi.
Pia spika ameeleza kuwa ni matarajio yake kuwa bunge lijalo litatawaliwa na amani pamoja na ushirikiano kwa wabunge wote bila ya kujali vyama vyao.
0 comments:
Post a Comment