Kwa mara nyingine tena Taifa letu
limepata fursa ya kuyafahamu mambo
yanayoendelea katika siasa za
Tanzania.Siasa za Tanzania zinatajwa
kuwa ni siasa za kipekee kabisa
duniani,siasa zilizojaa
hila,unafiki,usariti na ushawishi
unaotokana na nguvu ya fedha na
ahadi za vyeo.
Wadadisi wa mambo ya kisiasa nchini
waazitataja siasa za nchi hii kama
siasa uchwara zisizo na misimamo
ambazo hutawaliwa zaidi na "mahitaji
ya tumbo", kuliko uzalendo wa kujitoa
kulitumikia Taifa.Hizi ni siasa maslahi
ambazo badala ya kujikita katika
itikadi na falsafa za vyama,
zinaongozwa na njaa za wanasiasa
uchwara waliotayari kuvisariti viapo
vyao kukidhi mahitaji ya matumbo yao.
Matokeo ya wanasiasa wa aina hii ni
kuwakatisha tamaa wanamabadiliko wa
kweli waliojitoa muhanga kulitoa Taifa
letu katika utawala dharimu wa CCM.
Mara nyingi tumekuwa
tukijiuliza,inakuwaje mtu tuliyemuamini
kuwa amejitoa kwa dhati kulipigania
Taifa kupitia siasa za mageuzi,afike
mahali arudi nyuma na kuyarudia
matapishi yake huku akisahau majina
aliyoitwa majina kama " oil chafu na
mengineyo" wakati alipojiondoa CCM
na kuja upinzani?
Jibu la maswali haya nimelipata jana
hapa Kahama katika mkutano wa
hadhara wa JPM uliofanyika katika
viwanja vya milango kumi hapa
Kahama maarufu kama "uwanja wa
Magufuli". Katika mkutano huo
nilishuhudia nguvu kubwa ya ushawishi
aliyoifanya JPM akimshawishi
aliyekuwa mbunge wa Kahama na
mgombea ubunge kupitia CHADEMA
2015 James Lembeli alejee CCM.Umma
wa wakazi wa KAHAMA ulipigwa na
butwaa na kutoamini namna Rais
alivyokuwa anatumia madaraka yake
kumshaeishi James Lembeli arejee
CCM kwa ahadi kemkem.
Msikilize Magufuli katika video hii
akimshawishi Lembeli arudi CCM
Jambo la msingi tunalopaswa kujiuliza:
ikiwa Rais alitumia ushawishi wa
kiwango hiki hadharani mbele ya
mkutano wa hadhara kumuomba
Lembeli arejee CCM, ni nguvu gani ya
ushawishi hufanywa sirini kuwarubuni
makamanda wetu waviasi vyama vyao
na kurejea CCM?Unafikiri ushawishi ule
alioufanya JPM akimuomba Lembeli
arejee CCM ulianzia pale mkutanoni
katika viwanja vya Magufuli?Jibu ni
kwamba alichokuwa anakifanya JPM
pale mkutanoni ni mwendelezo wa
juhudi za chini kwa chini anazozifanya
na zifanywazo na wenzake kuwarubuni
viongozi na wanachama wa upinzani
kurudi CCM.
Ni dhahiri kuwa upinzani kunahitaji
moyo,ni wachache sana wanaoweza
kukataa " ushawishi wa Rais"wa
kujiunga na CCM, kwa siasa zetu
zinazoongozwa na tumbo, ni nadra kwa
mtu mwenye njaa kuukataa wito wa
rais,rais mwenye mamlaka za uteuzi na
anayeweza kukuteua na kukupa uraji
wa kukidhi njaa ya tumbo lako.
Inahitaji ujasiri wa kikamanda na moyo
wa kizalendo kuvishinda vishawishi vya
rais na nguvu ya fedha na ahadi za
vyeo ili usirejee ccm,vinginevyo hakuna
awezaye kushindana na ushawishi wa
aina ile nilioushuhudia jana hapa
Kahama.
Shukrani kwa Lembeli kwa "kusita"
kutimiza makubaliano ambayo naamini
tayari yalikuwa yameshafikiwa kabla ya
ule mkutano,lakini nilichokishuhudia
pale tayari "roho ya usariti"
imeshauingia moyo wa
Lembeli,kinachosubiriwa ni muda
muafaka tu ili aandaliwe mkutano
mwingine wa kumpokea akirejea tena
CCM.Pale mkutanoni alisita kutimiza
"usariti" wake,lakini alimuhakikishia
JPM kuwa "mkia wake bado upo" na
anasubiri kutekelezwa kwa mambo
flaniflani ili ayarudie matapishi yake
kwa kurejea tena CCM.
Njaa ni jambo la kawaida kwa viumbe
hai,lakini njaa hugeuka kuwa mbaya
pale inapohama toka tumboni na
kuingia kichwani. Lembeli huyu huyu
aliyeuaminisha Umma wa wanakahama
kuwa alishauriwa na mama yake
(Mwana Maria) na mizimu ya kwao
ilimpa baraka atoke CCM na kujiunga
UKAWA, leo anaisariti hadi mizimu
yake anayoiamini? Njaa mbaya
jamani!!!
Wapenda mabadiliko tusikatishwe
tamaa na makamanda waasi
wanaoikimbia kambi kwa ushawishi
upitao akili zao,ila jambo lililodhahiri
ni kwamba,wote wanaorejea CCM
hufanya hivyo baada ya vikao vya
muda mrefu vya ushawishi vifanywavyo
na ccm na serikali
yake,wanachokifanya jukwaani mbele
za watu ni hatua ya mwisho tu ya
kukamirisha usariti wao baada ya
mhusika kutimiziwa daadhi ya ahadi
alizoahidiwa.
Monday, 1 August 2016
Home »
» Siri za wanaorudi CCM toka upinzani zavuja
0 comments:
Post a Comment