Sunday, 7 August 2016
Home »
» Maswali kumi na mbili (12) ya kujiuliza kama kweli Yusuph Manji amekodishwa timu ya Yanga
Maswali kumi na mbili (12) ya kujiuliza kama kweli Yusuph Manji amekodishwa timu ya Yanga
Kuna habari inayoendelea ya kuhusu Manji KUKODISHWA TIMU YA YANGA, nina maswali yafuatayo mwenye majibu yake anijibu na nielewe.
1.Manji anaikodi Yanga kutoka kwa nani ??
2.Je kulishatengenezwa mkataba wa kukodishana ??
3.Je, ktk kipindi chake cha kukodi uwekezaji gani umekulibaliwa kufanywa kwa mujibu wa huo mkataba wao ??
4. Ni nani msimamizi wa huo mkataba ??
5. Je kwenye huo mkataba kuna kipengere cha kuchukua timu kama hakuna maendeleo yanayopatikana hata kabla ya mkataba kuisha ??
6. Nasikia mapato ya 75% yatakuwa yake na 25% ni ya wanachama je, yeye anapata hayo mapato kwa kipi alichowekeza/atakachowekeza ???
7 Na hayo mapato ya wanachama ya 25% wanachukua wanachama kwa utalatibu upi ...... na kwa uwekezaji gani walioufanya ........ na zinagawanywa vipi ???
8.Nani msimamizi wa haya kudhibitisha hii ni 75% anastahili Manji na hii ni 25% ni ya wanachama ???
9.Hawa wasimamizi wanalipwa na nani ???
10.Kama jengo halimuhusu je yeye ofisi anazifanyia wapi ???
11. Sisi binadamu (siombei mabaya) tunaweza kufa muda wowote je, kwenye huo ukodishwaji wake unarithiwa ??
12. Mtaji wake ni sh'ngapi ??
0 comments:
Post a Comment