1. Mwenyekiti wa timu anaitisha mkutano wa dharura bila kufuata katiba
2. Mkutano unahusisha wanachama wa dar pekee ila unafanya maamuzi kwa niaba ya wanachama wa Tanzania nzima
3. Mwenyekiti anavua kwanza uanachama watu kadhaa ili kutishia wengine wasimpinge
4. Analeta ajenda ya dharula kuwa timu inapaswa kukodishwa ili iendeshwe kisasa
5. Haweki vigezo vya mtu kutimiza ili aikodi labda kuna wengine pia watakuwa interested
6. Anajipa mamlaka ya kukodi team bure bila hata kutoa sumuni(hata ukumbi ukikodi unalipia jaman)
7. Anawadanganya wanachama kuwa team ilikuwa inajiendesha kwa hasara wakati yeye ndiye mwenyekiti(kama inajiendesha kwa hasara je muuza duka anaweza kumuomba bosi wake akodi duka lake wakati yeye ndo huwa anauza na anajua duka lile halina faida zaido ya hasara?)
8. Anatengeneza mkataba mwenyewe
9. Anataka ausain mwenyewe pande zote mbili za mwenykiti wa timu anayeruhusu timu ikodishwe na sehem ya mkodishaji
10. Anawaaambia watu hana shida na uwanja wala jengo( kwani timu ni uwanja na jengo au nembo na timu?) maana hata awaachie jengo lile mtafanyia nini? Uwanja ule nani anaweza japo ukodisha aweke kigodoro pale?
Ushauri kwa wanachama wa Yanga kuhusu Manji kukodisha timu kwa miaka 10
Kwanza nitamke wazi kuwa mimi ni mpenzi wa Yanga. Mimi nakubaliana na Manji kukodisha Timu kwa miaka 10 ila Wanachama wazingatie yafuatayo:-
(1) Kuna uwezekano kwenye biashara kukawa na HASARA. Kiwepo kipngele kwenye mkataba kuwa Manji akipata hasara sharti awalipe Klabu Tshs.200,000,000 kila mwezi. Hii isiwe na mjadala.
(2) Kuilipa Klabu Tshs.250,000,000 kwa mwezi mimi kwangu naona ni kiduchu. Kiwepo kwenye mkataba faida inayopatikana iwe ni kwa njia ya wazi ambapo mahesabu yatapigwa na kufikia hiyo faida. Mahesabu yasifanyike kwa kificho. Nashauri Manji ailipe Klabu Tshs. 500,000,000 kwa mwezi na siyo Tshs.250,000,000 kwa mwezi.
(3) Wakati wa kuandika Mkataba Klabu ikodi Mwanasheria Nguli ili kusimamia mkataba huo na kuishauri Klabu. Nampendekeza Klabu impendekeze Wanasheria kama Albert Msando, Ndugu Kibatala au T. Lissu.
(4) Ukaguzi wa mahesabu yasimamiwe Mashirika kama PriceWaterhouse au ErnstYoung ili kupata ukweli.
(5) Nawashauri Wananchama kuwa siyo wazo linaloletwa mbele yenu ni kuitikia NDIYOO............. hapana. Pokeeni wazo mlitafakari kwanza na baadaye kulitolea uamuzi. Zama za Ndiyooo............. zimepitwa na wakati

0 comments:
Post a Comment