Recent

JIFUNZE MAMBO MBALIMBALI YATAKAYOKUPA MAARIFA NA UJUZI MAISHANI

Thursday, 18 August 2016

Maswali 10 muhimu kuhusu serikali kuhamia Dodoma.


Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na mjadala kuhusu serikali kuhamia dodoma. Binafsi nadhani ni jambo jema haswa ukizingatia kuwa ni swala amablo lilishakuwepo toka kipindi kirefu nyuma.

Hata hivyo kama mtanzania wa kawaida kuna maswali najiuliza na sipati majibu hivyo nimeona nijaribu kuyaleta hapa ili kupata udadavuzi mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali

1: Neno serikali,kwa mujibu wa muktadha huu wa kuhamia dodoma ni kitu gani hasa? Yani ni wizara tu, idara tu, au wanamaanisha nini wanaposema serikali? Ili kueleweka vizuri nitatoa mfano. Wiza ya elimu ikihamia dodoma,taasisi zilizo chini yake kama vile NECTA, NACTE, TCU nk zitahama ama la?

Je, zisipohama hiyo wizara huko dodoma itakuwa inafanyaje kazi ili hali taasisi zake nyingi zitakuwa darisalama? Vivyo kwenye sekta nyingine kama viwanda na biashara -tbs, nk? Hapa naomba ufafanuzi mpana kidogo, ili tujue nai anahama nani hahami.

2: Je, kumetokea nini mpaka kuhama huku kuharakishwe namna hiyo?

3: Je, serikali imetafakari juu ya athari ya zoezi hili kwa ughafla huu? Kuna baadhi ya taasisi za serikali zimepangisha majengo kutoka kwa wadau mablimbali, na kuna mikataba wameingia na wapangishaji hao, Je serikali imliangalia hilo na athari za kuvunja hiyo mikata?

Je, serikali imeangali wazabuni katika tenda mabimbaili inazpata na kuangalia athari ya kuhamia dodoma kwa ishu za zabuni hizo? Je kampuni zenye kutoa huduma za ulinzi na usafi(mfano tu) zitakubali kuendelea kutoa huduma hizo dodoma na kwa makubaliano yapi?

4: Kwakuwa viongozi wakubwa waserikali wana makazi madogo dodoma na kwao haina athari sana kuhama, Je wamehakikisha kuwa wafanyakazi wote watapata makazi dodma maeneo pia mabayo hayataathiri ufanisi wao?

5: Binadamu anaitaji kujiandaa kisaikolojia zaidi kuliko kifedha na muda ni jambo muhimu katika kufanikisha hili, Je serikali imewaanda watumishi wake kisaikolojia juu ya wao kuhamia dodoma? Kwa muda mfupi watakaokuwa nao watuishi, serikali haini kuwa inaweza kunaweza kuwa na mtizamo mbaya wa zoezi hili kwa watumishi wake?

Je, wakihama, kwa muda mfupi huu watawezaje kuacha makazi ya salama? Uimara wa familia je? Hivi serikali haioni kuwa kuna uwezekano wa watumishi kuomba ruksa za mara kwa mara kwenda kuweka mambo ya kifamialia sawa pale ambapo watahama kwa muda mfupi bila ya wao kujiandaa vizuri?

6: Hivi serikali haikuona kuwa kuweka zoezi hili ndani ya muda mfupi kunaweza sababisha gharama za maisha dodoma kuongezeka sana kwakuwa kutakuwa na ongezeko la ghafla la mahitaji bila ya kuwa na ongezeko sawa la usambazaji? Mathalani kodi katika nyumba zitapanda sana,je hilo serikali imeliangaliaje?

7: Majengo yakokuwa yanatumiwa na serikali dar yatatumika kwa utaratibu gani haswa ukizingatia kutakuwa na kuondoka kwa ghafla?

8: Kauli ya mh raisi ilikuwa kuhamia dodoma ndani ya miaka hii minne, Je kama wizara zinahama ndani ya mwezi, kulikuwa na ulazima kweli wa kufanya hivyo?

9: Kwakuwa bajeti ilishapitishwa, ni kutoka fungu gani ambalo serikali italitumia katika kufanikisha zoezi hilo?

10: Kwakuwa serikali inafanya kazi na wadau mablimbali, ni kwanamna gani imejipanga kuhakiksha kuwa kuhama kwake hasa huku kwa muda mfupi hakutaathiri ushirikishwaji wa wadau hao katika nyanja mbalimbali? Kwamfano mabalozi, taasisi na mashirika ya imataifa nk.

NB: Tafadhali tuache ushabiki na tujikite kwenye hoja. Ingependeza kama ungejibu baadhi ya hoja(kama una majibu) ama ukaongeza maswali(kama unayo pia) ili mwisho wa siku tupate uelewa mpana wa hii dhana ya serikali kuhamia dodoma.

0 comments:

Post a Comment