Wednesday, 17 August 2016
Je wajua? Kinachoendelea Yanga chanzo ni tetesi za DANGOTE kutaka kuwekeza BIL 65
Hii issue imeanza nyuma kidogo. Kuna kiongozi mmoja mkubwa wa Yanga alipata Taarifa kuwa Dangote anataka awekeze Yanga Tsh Bil 65. Kiongozi huyu mkubwa wa hiyo team ambaye kiuhalisia ndiye mweenye maamuzi makubwa haraka haraka akaona amepata nafasi ya kutengeneza pesa.
Hivyo haraka akaanza michakato ya Kuvunja udhamini na TBL ili sasa aiingize Kampuni moja humo ndani na kwa kuwa yeye ni mhusika mkuu kwa ushawishi wake zile pesa zikija kwake awe ndiye muidhinishaji mkuu.
ili jambo hili likae sawa likaja wazo la haraka sana la mtu flan kukodi hiyo team ya Yanga. Ili atakapokodi yeye ile pesa ambayo itatyolewa tsh bil 65 itakuwa ka ajili ya kumnufaisha yeye na ndo likaja wazo yeye atumie asil 75 na Yanga wapate asilimia 25 hasara yake faida yao. Kwa akili za haraka haraka utagundua kuwa kwa bil 65 yeye hakuwa na uwezekano wa kupata hasara maana ile pesa imewekwa na mtu mwingine. Bwana Dangote. wanachama wa Yanga wakapiga Makofi na Kufurahia sana ukodishaji huu pasipo kujua nini kinaendelea mule ndani.
Mzee akilimali aliliona hili kwa sababu habari alizipata na akaona kuwa hapa kuna mtu anaenda faidika sana kupitia Yanga. ikaanza misuguano. ile misuguano ilipozidi ikamfikia kiongozi mmoja wa juu ambaye akahisi kuwa njama zake kuna watu wamezigundua. na huyu naye akaamua kutishia kujiuzulu nafasi yake ili kuliua jambo hili. hivyo yeye kubaki na team na hatimaye kumshawishi Huyo anayetaka wekeza bil 65 kuwekeza na akiwa yeye kiongozi ana uwezo wa kuzi control kimatumizi n.k ili aweze jinufaisha.
kwa wenzangu na mimi hili hawalifaham. hivyo tuzidi kumuombea Manji awe mwenyekiti wa hii team na pia tumkodishe ili team ya Yanga ifanye vizuri.
asanteni sana. source mwana Yanga Mnazi kabisa na mwenye mapenzi na team
0 comments:
Post a Comment