Friday, 14 June 2013
Home »
» "WASANII TUTAZIDI KUPUKUTIKA MAANA TUNAROGANA SANA..NATAMANI KUACHA MUZIKI ILI NIYANUSURU MAISHA YANGU"....SHILOLE
"WASANII TUTAZIDI KUPUKUTIKA MAANA TUNAROGANA SANA..NATAMANI KUACHA MUZIKI ILI NIYANUSURU MAISHA YANGU"....SHILOLE
MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka
kuwa, suala la wasanii wa muziki kurogana linamuumiza kichwa kiasi cha
kufikiria kuachana na kazi hiyo.
Akiongea na mwandishi wetu pasipo kuwataja wabaya wake, Shilole alisema hivi sasa ‘kesi’
za wasanii kurogana zimeshika kasi kuliko siku za nyuma na anashindwa
kuelewa ni kwa nini watu wanamuasi Mungu kwa kuendekeza ushirikina.“Kwa staili hii wasanii tutazidi kupukutika, kuna
wakati huwa nafikiria hata kuachana na muziki maana tunarogana na
namuomba Mungu usiku na mchana hata kabla ya kupanda stejini kwani hali
ni tete,”
alisema Shilole....
0 comments:
Post a Comment