Adai kesho ulinzi upo wa kutosha.
Awapongeza Arusha kuitosa Chadema.
Awapongeza Arusha kuitosa Chadema.
Atamba CCM kuzoa kata zote.
Awasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kesho.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg.Nape Nnauye amewataka wananchi
kwenye kata zinazofanya uchaguzi mdogo kesho kupuuza alivyoviita vitimbi
vya Chadema na wafuasi wao badala yake wajitokeze kwa wingi kushiriki
kwenye upigaji wa kura kwa amani na utulivu.
Nape
ameyasema hayo jijini Arusha jana wakati alipokuwa anajibu maswali ya
waandishi wa habari waliotaka kujua tathimini ya kampeni na jinsi CCM
ilivyojipanga kwenye uchaguzi mdogo katika kata mbalimbali nchini.
Nape
alisema kwa ujumla wake kampeni zimekwenda vizuri karibu katika kila
kata ukiacha matukio kadhaa machache ya vurugu ambayo alidai yamekuwa
yakiratibiwa na Chadema na wafuasi wao baada ya kuvuta bangi na
kunywesha vijana wao viroba.
“nimekuwa Arusha kwa siku mbili tatu, hakuna mashaka kuwa Arusha
wamechoshwa na vurugu za Chadema , baada ya kuhangaishwa kwa miaka
mitatu na vurugu za Chadema wameamua sasa kurudisha utulivu na heshima
ya jiji la Arusha, hivyo nawapongeza sana” alisema Nape.
” ni
kweli hata mie nimesikia wenzetu baada ya kuona maji ya shingo wameamua
kutumia vitisho kujaribu kutisha watu hasa kina mama na wazee wasiende
kupiga kura, lakini nawahakikishia CCM tumejipanga kuwalinda waende
kupiga kura kwa amani na utulivu. Isitoshe taarifa tulizoziapata
zinaonyesha serikali imejipanga vizuri sana kulinda amani na utulivu,
hivyo tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura bila hofu”
alisisitiza Nape.
Aidha Nape alidai kwa taarifa walizonazo wanamatumaini kuwa kata zote 25
zinazofanya uchaguzi mdogo CCM itashinda kwani wanaamini kuwa wananchi
wana imani kubwa na CCM na kuwa vitimbi vinavyofanywa na wapinzani
nchini vimewachefua sana wananchi.
Itakumbukwa kuwa chaguzi ndogo nchini zinafanyika kwenye kata 25
kufuatia kata hizo kuwa wazi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo vifo
na baadhi kuhama au kufukuzwa vyama vyao vya siasa.
Ushindani mkubwa ulitegemewa sana jijini Arusha ambapo kuna kata nne
zinafanya ucahguzi mdogo kufuatia Chadema kuwafukuza madiwani wake. Hata
hivyo hali jijini Arusha inaonyesha Chadema kulemewa sana kiasi cha
kuwa na uwezekano wa kupoteza kata zote ambazo walikuwa wakizimiliki
mwanzoni.
0 comments:
Post a Comment