Ndugu zangu kuanzia leo na ksiku zijazo natarajia kuwaletea vipengele mbalimbali vya rasimu ya katiba mpya na kuvitolewa uchambuzi ili mpate kujifunza.
Kwa kuanza leo nitaanza na ibara ya75. Mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya
‐ 30 ‐
Madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa:
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa
Katiba hii na sheria za nchi;
(b) ni mwenye akili timamu;
(c) angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa
Jamhuri ya Muungano;
(d) wakati wa kugombea, ana umri usiopungua miaka arobaini;
(e) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii;
(f) anayo angalau shahada ya kwanza ya chuo kikuu
kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi;
(g) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha
siasa au mgombea huru;
(h) sera zake au sera za chama chake si za mrengo wa kuligawa
Taifa kwa misingi ya ukabila, udini, rangi au jinsia;
(i) ni mwadilifu na anafuata maadili ya Taifa.
Kipengele F cha ibara hii ya 75 kinachoelezea sifa za RAISI kinasema ni lazima mgombea awe amehitimu SHAHADA ya kwanza katika chuo kinachotambulika na serikali.Kwa hatua hii nawapongeza sana serikali na tume ya mabadiliko ya katiba kwani Elimu ya mgombea wa uraisi ni swala muhimu sana katika kutathmini weledi na uwezo wa kiutendaji wa mtu.
Wednesday, 12 June 2013
Home »
» JIFUNZE VIPENGELE MBALIMBALI VYA RASIMU YA KATIBA MPYA
0 comments:
Post a Comment