"NAFIKIRIA KUAHIRISHA SHOW YANGU ILA SI KWA KUMUOGOPA MWANAMKE"...MWANA FA
MSANII wa muziki wa
kizazi kipya nchini Tanzania Mwana FA anafikiria kuahirisha shoo yake
ya kesho kufuatia kifo cha msanii mwenzake wa kizazi kipya Langa Kileo,
kilichotokea leo jijini Dar es Salaam.
Mwana
FA anafikiria kuahirisha shoo yake ya kesho iliyopangwa kufanyika
katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na tayari
ameanza kuwasiliana na meneja wake kwa ajili ya hatua hiyo.
Hii
itakuwa ni mara ya pili kwa Mwana FA kuahirisha shoo yake, awali
ilipaswa kufanyika Mei 31 mwaka huu lakini ikaahirishwa kutokana na kifo
cha aliyekuwa msanii mwenzake wa Bongo Fleva Albert Mangwea.
Hata
hivyo Mwana FA ametoa tahadhara ya kejeri juu ya hatua hiyo huku
akimtupia madongo mhasimu wake mkubwa Mwanadada Lady Jay Dee...
7 minutes ago via mobile · Like Mwana FA Halisi : "Msiba wa mwana HIPHOP mwenzetu Langa unanifanya nifikirie kuahirisha show ya kesho. Nawasiliana na manager wangu kisha nitawajuza ,but si kwa kumuogopa mwanamke,Let it be clear"
0 comments:
Post a Comment