Aminiel
Aligaesha ambae ni Afisa Uhusiano wa hospitali ya Taifa Muhimbili
amethibitisha kwamba msanii Langa amefariki dunia June 13 2013 saa kumi
na moja jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo toka juzi jioni
ambapo kutokana na sababu za kimaadili kwenye tiba, Muhimbili hospitali
hawawezi kusema rapper huyu alikua anaumwa nini bali ndugu ndio wenye
mamlaka ya kufanya hivyo.Kwenye maelezo aliyoyatoa kwa millardayo, Aminiel amesema Marehemu Langa alipokelewa kwenye idara ya wagonjwa wa magonjwa ya dharura usiku wa kuamkia jana na kupatiwa huduma ambapo leo June 13 2013 ndio alihamishiwa kwenye chumba cha wagonjwa Mahututi na baadae kufariki dunia.






0 comments:
Post a Comment