Home »
» SAFARI YA RAISI WA MAREKANI BARACK OBAMA YAHAIRISHWA..
Ikulu
ya White House ya Marekani imekatiza safari ya Rais Obama na mkewe
Michelle ya kutembelea mbuga ya wanaya ya mikumi iliyopo Tanzania
kutokana na ukata unaoikabili serikali yake. Imeelezwa katika gazeti la
Washington Post jana.
Gazeti hilo ambalo lilinukuu mipango ya
siri ya safari hiyo imesema kuwa safari ya Obama na mkewe ambayo ilikuwa
ifanyike baadaye mwezi huu, ingehitaji majasusi wa kumlinda rais huyo
kwa njia za kipekee zaidi kuhakikisha usalama wake na mkewe.
Safari ya Rais katika mbuga za wanyama inahitaji ulinzi wa hali ya juu,
silaha za hali ya juu kama siper rifles ambazo zitaweza kulenga wanyama
wakali kama cheetahs, (duma, samba au wanyama wengine kama ikitokea
wanataka kumsogelea au kumdhuru rais huyo.
(The safari "would have required the president's special counterassault
team to carry sniper rifles with high-caliber rounds that could
neutralize cheetahs, lions or other animals if they became a threat,"
the paper reported.)
Ikulu ya Marekani imefuta ziara hiyo ambayo rais Obama alikuwa atembelee mikumi national park kwa masaa mawili.
Hata hivyo msemaji wa Ikulu ya Marekani hakupatikana mara moja kutoa
maelezo. Msemaji mwingine alisema ziara ya kutembelea Robben Island
ambamo Mzee Mandela alikuwa amefungwa kwa miaka 27 ilikuwa ikipewa
kipaumbele zaidi dhidi ya safari ya tanzania.
"Sababu
kubwa za kufutwa kwa ziara hiyo ni kwa sababu ya ya kuwa na upungufu wa
bajeti na vifaa vya kumlinda Obama katika mission yake hiyo, hivyo
ikaonekana ni rahisi zaidi kutembelea Robben Island kuliko Mikumi
National Park. "Alisema msemaji huyo Josh Earnest na kuongeza kuwa
"ni ngumu kufanya safari zote hizo kwa pamoja."
Hii ilikuwa ni
ziara ya kitalii ya kwanza kwa Rais Obama tangia amechaguliwa January
2009, safari ambayo ingeligarimu Taifa hilo kati ya dola milioni 60 hadi
100.
Mamia ya askari wa siri (secret agents) wanatakiwa
kupelekwa katika sehemu ambazo Obama atatembelea pamoja na manuari ya
kivita yenye kubeba ndege za kivita (Navy aircraft carrier or amphibious
ship) ikiwa na wahudumu pamoja na wauguzi maalum ambao watakaa ufukweni
kwa dharura yeyote itakayojitokeza.
Pamoja na hayo magari
zaidi ya 56 yatapelewa kwenye nchi hizo tatu kwa njia ya ndege pamoja na
vioo maalum vya kuzuia risasi (sheets of bulletproof glass) ambavyo
vitazungushiwa kwenye hoteli ambayo atafikia Obama.
Kama vile
ulinzi huo hautoshi, pia kuta kuwa na ndege za kivita zitakazokuwa
zinazunguka katika anga ambalo Obama atakuwa amefikia na hizo ndege
zitakuwa zinazunguka angani hapo kwa masaa 24 kwa kupeana zamu ("Fighter
jets will fly in shifts, giving 24-hour coverage over the president's
airspace")
0 comments:
Post a Comment