Recent

JIFUNZE MAMBO MBALIMBALI YATAKAYOKUPA MAARIFA NA UJUZI MAISHANI

Monday, 17 June 2013

Sunday, 16 June 2013

BETTY NA BOLT WANASWA TENA WAKIVUNJA AMRI YA SITA NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER


Mu Ethiopia Betty na mu Sierra Leon Bolt wameanikwa  tena  na  camera  za  Jumba  la  big  Brother  wakivunja  amri  ya  sita.

Hii  ni  mara  ya  pili  kwa  washiriki  hao  kutenda  tendo  hilo la  aibu  ndani  ya  kamera  hizo  

Saturday, 15 June 2013

BOMU LALIPUKA NA KUUA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA HUKO ARUSHA LEO

.Hazi ni baadhi ya maiti

Hizi ni damu za wahanga

 
 Watu saba wamejeruhiwa kwa mlipuko unaohisiwa kuwa ni bomu,mara baada ya mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliokuwa ukifanyika katikaViwanja vya Soweto Mjini Arusha. 
imeripotiwa kuwa watu wawili wamefariki dunia papo hapo, tunaelekea wapi Tanzania

NAPE: PUUZENI VITISHO VYA CHADEMA, JITOKEZENI KUPIGA KURA KWA WINGI

Adai kesho ulinzi upo wa kutosha.
Awapongeza Arusha kuitosa Chadema.
   
Atamba  CCM kuzoa kata zote.  
Awasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kesho.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg.Nape Nnauye amewataka wananchi kwenye kata zinazofanya uchaguzi mdogo kesho kupuuza alivyoviita vitimbi vya Chadema na wafuasi wao badala yake wajitokeze kwa wingi kushiriki kwenye upigaji wa kura kwa amani na utulivu.
Nape ameyasema hayo jijini Arusha jana wakati alipokuwa anajibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua tathimini ya kampeni na jinsi CCM ilivyojipanga kwenye uchaguzi mdogo katika kata mbalimbali nchini.
Nape alisema kwa ujumla wake kampeni zimekwenda vizuri karibu katika kila kata ukiacha matukio kadhaa machache ya vurugu ambayo alidai yamekuwa yakiratibiwa na Chadema na wafuasi wao baada ya kuvuta bangi na kunywesha vijana wao viroba.
“nimekuwa Arusha kwa siku mbili tatu, hakuna mashaka kuwa Arusha wamechoshwa na vurugu za Chadema , baada ya kuhangaishwa kwa miaka mitatu na vurugu za Chadema wameamua sasa kurudisha utulivu na heshima ya jiji la Arusha, hivyo nawapongeza sana” alisema Nape.
” ni kweli hata mie nimesikia wenzetu baada ya kuona maji ya shingo wameamua kutumia vitisho kujaribu kutisha watu hasa kina mama na wazee wasiende kupiga kura, lakini nawahakikishia CCM tumejipanga kuwalinda waende kupiga kura kwa amani na utulivu. Isitoshe taarifa tulizoziapata zinaonyesha serikali imejipanga vizuri sana kulinda amani na utulivu, hivyo tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura bila hofu” alisisitiza Nape.
Aidha Nape alidai kwa taarifa walizonazo wanamatumaini kuwa kata zote 25 zinazofanya uchaguzi mdogo CCM itashinda kwani wanaamini kuwa wananchi wana imani kubwa na CCM na kuwa vitimbi vinavyofanywa na wapinzani nchini vimewachefua sana wananchi.
Itakumbukwa kuwa chaguzi ndogo nchini zinafanyika kwenye kata 25 kufuatia kata hizo kuwa wazi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo vifo na baadhi kuhama au kufukuzwa vyama vyao vya siasa.
Ushindani mkubwa ulitegemewa sana jijini Arusha ambapo kuna kata nne zinafanya ucahguzi mdogo kufuatia Chadema kuwafukuza madiwani wake. Hata hivyo hali jijini Arusha inaonyesha Chadema kulemewa sana kiasi cha kuwa na uwezekano wa kupoteza kata zote ambazo walikuwa wakizimiliki mwanzoni.

PICHA ZA SHOW YA LADY JAYDEE NYUMBANI LOUNGE.... WATU WALIJAA MPAKA WAKAANZA KUBEBANA


Mwanadada Judith Mbibo aka Lady Jaydee usiku wa kuamkia Jumamosi ya June 15 amefanikiwa kuweka historia kwenye muziki wa Tanzania kwa kulijaza eneo zima la Nyumbani Lounge alipokuwa akifanya show yake ya kuadhimisha miaka 13 tangu aanze muziki. 
DSC_4275

Katika show hiyo, Lady Jaydee amesindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Juma Nature, Sugu, Profesa Jay, Wakazi, Grace Matata na wengine. Pia Jaydee ameitumia siku hiyo kuzindua albam yake mpya, Nothing But The Truth na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Hizi ni picha za show hiyo.

Umati wa watu unaoshuhudia show ya Lady J Dee sasa hivi hapa Nyumbani Longe.

Lady J Dee anatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki.

Professa Jay akiwa back stage anajiandaa kupanda jukwaani kutoa burudani nzuri kwa mashabiki
 

Miaka 13 ya Lady j Dee#sasa hivi ndiyo Mh.Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ameingia

Lady J Dee anatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki.

Lady J Dee anatoa burudani ya kutosha kwa mashabiki.

Team Times Fm 100.5 (Dj Jors Bless,Ndimbo na Mariam)

Sugu na Mkoloni wanatoa burudani kali kwa mashabiki.

Mama mzazi wa Lady J Dee naye amekuja kushuhudia show ya mwanae.

Juma Nature anatoa burudani kwa mashabiki

Sugu akitoa burudani kali kwa mashabiki
M 2 The P akiongea machache baada ya kukaribishwa kwenye jukwaa na Juma Nature.

Friday, 14 June 2013

SAFARI YA RAISI WA MAREKANI BARACK OBAMA YAHAIRISHWA..

Ikulu ya White House ya Marekani imekatiza safari ya Rais Obama na mkewe Michelle ya kutembelea mbuga ya wanaya ya mikumi iliyopo Tanzania kutokana na ukata unaoikabili serikali yake. Imeelezwa katika gazeti la Washington Post jana.

Gazeti hilo ambalo lilinukuu mipango ya siri ya safari hiyo imesema kuwa safari ya Obama na mkewe ambayo ilikuwa ifanyike baadaye mwezi huu, ingehitaji majasusi wa kumlinda rais huyo kwa njia za kipekee zaidi kuhakikisha usalama wake na mkewe.

Safari ya Rais katika mbuga za wanyama inahitaji ulinzi wa hali ya juu, silaha za hali ya juu kama siper rifles ambazo zitaweza kulenga wanyama wakali kama cheetahs, (duma, samba au wanyama wengine kama ikitokea wanataka kumsogelea au kumdhuru rais huyo.

(The safari "would have required the president's special counterassault team to carry sniper rifles with high-caliber rounds that could neutralize cheetahs, lions or other animals if they became a threat," the paper reported.)

Ikulu ya Marekani imefuta ziara hiyo ambayo rais Obama alikuwa atembelee mikumi national park kwa masaa mawili.
Hata hivyo msemaji wa Ikulu ya Marekani hakupatikana mara moja kutoa maelezo. Msemaji mwingine alisema ziara ya kutembelea Robben Island ambamo Mzee Mandela alikuwa amefungwa kwa miaka 27 ilikuwa ikipewa kipaumbele zaidi dhidi ya safari ya tanzania.

"Sababu kubwa za kufutwa kwa ziara hiyo ni kwa sababu ya ya kuwa na upungufu wa bajeti na vifaa vya kumlinda Obama katika mission yake hiyo, hivyo ikaonekana ni rahisi zaidi kutembelea Robben Island kuliko Mikumi National Park. "Alisema msemaji huyo Josh Earnest na kuongeza kuwa "ni ngumu kufanya safari zote hizo kwa pamoja."

Hii ilikuwa ni ziara ya kitalii ya kwanza kwa Rais Obama tangia amechaguliwa January 2009, safari ambayo ingeligarimu Taifa hilo kati ya dola milioni 60 hadi 100.

Mamia ya askari wa siri (secret agents) wanatakiwa kupelekwa katika sehemu ambazo Obama atatembelea pamoja na manuari ya kivita yenye kubeba ndege za kivita (Navy aircraft carrier or amphibious ship) ikiwa na wahudumu pamoja na wauguzi maalum ambao watakaa ufukweni kwa dharura yeyote itakayojitokeza.

Pamoja na hayo magari zaidi ya 56 yatapelewa kwenye nchi hizo tatu kwa njia ya ndege pamoja na vioo maalum vya kuzuia risasi (sheets of bulletproof glass) ambavyo vitazungushiwa kwenye hoteli ambayo atafikia Obama.

Kama vile ulinzi huo hautoshi, pia kuta kuwa na ndege za kivita zitakazokuwa zinazunguka katika anga ambalo Obama atakuwa amefikia na hizo ndege zitakuwa zinazunguka angani hapo kwa masaa 24 kwa kupeana zamu ("Fighter jets will fly in shifts, giving 24-hour coverage over the president's airspace")

"WASANII TUTAZIDI KUPUKUTIKA MAANA TUNAROGANA SANA..NATAMANI KUACHA MUZIKI ILI NIYANUSURU MAISHA YANGU"....SHILOLE

MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa, suala la wasanii wa muziki kurogana linamuumiza kichwa kiasi cha kufikiria kuachana na kazi hiyo. Akiongea na mwandishi wetu pasipo kuwataja  wabaya  wake, Shilole alisema hivi sasa ‘kesi’ za wasanii kurogana zimeshika kasi kuliko siku za nyuma na anashindwa kuelewa ni kwa nini watu wanamuasi Mungu kwa kuendekeza ushirikina.“Kwa staili hii wasanii tutazidi kupukutika, kuna wakati huwa nafikiria hata kuachana na muziki maana tunarogana na namuomba Mungu usiku na mchana hata kabla ya kupanda stejini kwani hali ni tete,” alisema Shilole....

OMMY DIMPOZ AMTANDIKA TUSI MAREHEMU NGWEA....ANADAI KUWA HAWEZI KUFA MASIKINI KAMA NGWEA NA AMECHOKA KUZIKA MASIKINI

KWELI asiye na adabu hakosi sababu ya kuharibu, mwenye mdomo mchafu ni ada yake kutoa neno chafu, mwanamuziki chipukizi, Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amedhihirisha kuwa ana kiwango cha juu sana cha dharau kwa kumdhihaki na kumtusi mtu aliyetangulia mbele za haki.


Omar Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
Utamaduni wetu Tanzania na kama ilivyo kwa mafundisho ya dini kupitia vitabu vinne vitakatifu, Torati, Zaburi, Injili na Kuran, fundisho ni kwamba mja aliyepoteza maisha hakashifiwi, hasimangwi, hahukumiwi, isipokuwa huhifadhiwa kwa heshima kisha kuombewa salama na amani mbele ya Mungu.

Ommy Dimpoz, kijana ambaye ni mwaka jana tu alikuwa ‘anawanga’ huku na huko mikono nyuma akiomba msaada wa kimuziki, hivi sasa anajiona ameota meno ya juu kuweza kung’ata, kiburi hicho kimempa uthubutu wa kumtusi Mfalme wa Freestyle, marehemu Albert Kenneth Mangwea ‘Ngwair’.

Thamani ya Ngwair na namna alivyozikwa kwa heshima hajaviona, badala yake akatusi kuwa Mfalme wa Freestyle alikufa maskini ndiyo maana mazishi yake yalikuwa ya kuungaunga michango ya wadau.


Kifo cha Ngwair, kilivuta makundi mbalimbali kushiriki kwa hali na mali kuchangia na kumzika, taifa lilizizima mkoa kwa mkoa, mguso huo wa kitaifa aliokuwa nao mwanamuziki huyo, Ommy hakuuona, isipokuwa akanena: “Sitaki kufa maskini kama Ngwair.”
Marehemu Albert Kenneth Mangwea ‘Ngwair’.

Akimweleza mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, Juni 10 (Jumatatu) na Juni 11, mwaka huu (Jumanne), Ommy alidhihaki hata ushiriki wa wanamuziki waliosimamisha shughuli zao kwa muda kisha kuungana na kushikamana kuhakikisha Ngwair anazikwa kwa heshima.
 
“Sitaki nikifa yatokee kama ya Ngwair, amekufa Afrika Kusini, hata kuusafirisha mwili kuuleta Tanzania imebidi mpaka watu wachangie, ile ni aibu sana,” alisema Ommy kwa dharau.

Kutokana na uzito wa maneno ambayo Ommy aliyatamka kuhusu Ngwair, siku iliyofuata (Jumanne), mwandishi wetu alimpigia simu kumuuliza kama maelezo hayo ya kashfa aliyatoa akiwa amelewa au la?

Ommy kwa kujiamini, alijibu kwamba alichokisema kuhusu Ngwair ni ukweli kwa asilimia 100.

MWANDISHI: Nakushauri kama mdogo wangu, siku nyingine usirudie kutamka maneno hayo ni mabaya sana kwa mtu aliyekufa.

OMMY: Sijaongea neno baya, nimesema ukweli wasanii hatutakiwi kufa maskini.

MWANDISHI: Wewe unaona mtu akichangiwa baada ya kufa ndiyo kipimo cha umaskini?

OMMY: Kuna mambo mengi ambayo yangefanyika kabla ya kuchangiwa lakini Ngwair alishindwa kuyafanya.

MWANDISHI: Sasa Ngwair angefanya nini wakati yeye ameshakufa?

OMMY: Kuna mambo yangefanyika, mfano kusafirisha mwili kutoka Afrika Kusini.

MWANDISHI: Sasa Ngwair angejisafirisha mwenyewe?

OMMY: Nachosema mimi ni kwamba wasanii hatutakiwi kufa maskini.

MWANDISHI: Sikiliza Ommy, hata mabilionea wakubwa huwa wanachangiwa. Mtu kuchangiwa siyo kashfa wala aibu kama unavyotaka kulionesha tukio la Ngwair. Marehemu Steven Kanumba alikuwa anatembelea Toyota Lexus V8, mbona alipokufa kila kitu alifanyiwa? Ni jambo la kawaida.
 
OMMY: Ngwair alikuwa na ‘stresi’ za maisha ndiyo maana alikuwa anakula unga.
 
MWANDISHI: Ulishawahi kumwona Ngwair akitumia unga?
 
OMMY: Kwanza nakusikia unanirekodi, sijui una malengo gani.


MANENO YA KASHFA MLIMANI CITY
Juni 8, mwaka huu, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA)  mwaka 2012-2013, Ommy Dimpoz alizungumza maneno ya kashfa ambayo moja kwa moja yalitafsiriwa ni dongo kwa Ngwair.
 
Baada ya kutangazwa mshindi wa kipengele cha Video Bora ya Mwaka na kukabidhiwa tuzo yake, Ommy alibwabwaja: “Jamani tumechoka kuzika wasanii maskini wenye majina makubwa.”
Japo hakutaja jina la yule aliyekuwa anamzungumzia, tafsiri ya wengi ni kwamba Ommy alikuwa anamzungumzia Ngwair kwa sababu ndiye staa aliyekuwa amezikwa kishindo cha siku moja tu kabla ya usiku huo wa tuzo. Ngwair alizikwa Alhamisi, tuzo Jumamosi.
 
“Huyu dogo ana nyodo sana, sasa haya ni maneno gani ya kuzungumza? Hapa anamzungumzia Ngwair, ila anapaswa kujua kwamba yeye bado msanii mdogo sana kumlinganisha na Ngwair,” alisema mtangazaji mmoja kwa masikitiko.

MAPOZI NI KAWAIDA YAKE, ATIMULIWA KIGOMA ALL STARS

 
Ndani ya Kampuni ya Kigoma All Stars, awali Ommy alikuwa mmoja wa wajumbe kwenye bodi ya wakurugenzi lakini hivi karibuni alitimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Peter Msechu.
 
Chanzo chetu makini ndani ya Kigoma All Stars, kimetonya kuwa Ommy alionesha tabia mbaya dhidi ya wasanii wenzake wanaounda kampuni hiyo, hivyo hakukuwa na jinsi zaidi ya kumtimua ujumbe wa bodi na kumuweka Msechu.
 
“Alikuwa ameshakuwa kero. Unajua pale Kigoma All Stars wote ni mastaa lakini yeye anajiona yupo juu ya wote. Tunaitisha vikao hatokei, tunakwenda kufanya shoo hatokei, tunamuona hana umoja na sisi na hatufai.
 
“Uamuzi wa kwanza ulikuwa ni kumtimua kabisa ili asiwepo kabisa kwenye kampuni yetu, maana siyo lazima kila mtu mwenye asili ya Kigoma awepo Kigoma All Stars. Baadaye kwa busara za mlezi wa kampuni yetu, Zitto Kabwe ndiyo tukamuondoa kwenye bodi.
“Tumembakiza kwenye kampuni kama mwanahisa wa kawaida tukiwa tunampima. Akiendelea kuleta mapozi yake, hatutamvumilia, tutamfukuza moja kwa moja,” kilisema chanzo chetu.
 
Chanzo hicho kiliongeza, ndani ya Kigoma All Stars kuna wasanii wakubwa kama Nasibu Abdul ‘Diamond’, Ali Kiba, Mwasiti Almasi, Sunday Mangu ‘Linex’, Banana Zorro na wengineo lakini hawaringi, isipokuwa Ommy ndiye fungakazi kwa maringo.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), vilevile Waziri Kivuli wa Fedha na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alipoulizwa kuhusu Ommy kutimuliwa kwenye bodi, alikiri hilo kufanyika.
 
“Ni kweli kuna mabadiliko kwenye bodi, wanamuziki wenyewe kwa sababu ndiyo wanahisa, waliamua kumuondoa Ommy Dimpoz na nafasi yake akawekwa Peter Msechu,” alisema Zitto.
 
Kuhusu kutimuliwa kwenye bodi Kigoma All Stars, Ommy hakutaka kuzungumza chochote, badala yake alijikanyagakanyaga.

OMMY NA NYIMBO TATU
Ommy anajiita super handsome, mapozi, kampuni yake anaiitwa Pozi Kwa Pozi, majina hayo yanatosha kueleza sababu kwa nini amemdhihaki Ngwair na haelewani na wasanii wenzake.
 
Ndiyo kwanza ana nyimbo tatu tu, Nai Nai (alisaidiwa sana na Ali Kiba), Baadaye na Me & You (amesaidiwa sana na Vanessa Mdee) lakini amekuwa wa migogoro na mbwembwe nyingi dhidi ya wasanii wenzake.
 
Alishawahi kurushiana maneno kwenye vyombo vya habari na mwanamuziki Cyril Kamikaze, baadaye akaingia kwenye gogoro zito na mwana Hip Hop wa Nako 2 Nako Soldier, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’.
 
Kuhusu Lord Eyez ambaye ni memba wa Familia ya Weusi, alidai alimuibia taa, power windows, vioo na vifaa vingine vya gari lake lakini kesi ilipofika mahakamani, Ommy hakwenda kutoa ushahidi.
 
Ommy alishindwa kutoa ushahidi lakini kabla yake alitangaza katika vyombo vya habari kuwa Lord Eyez ni mwizi na kwamba alimwibia vifaa vya gari lake, zaidi ya hapo alikusanya watu wakampa kipigo memba huyo wa Weusi kisha wakampeleka polisi ambako aliwekwa lupango.

Credit: GPL

Thursday, 13 June 2013

MAREHEMU LANGA KUZIKWA JUMATATU ALASIRI

kwa mujibu wa taarifa kutoka katika familia ya marehemu Langa Kileo, mazishi ya msanii huyo yatafanyika siku ya jumatau katika makaburi ya Kinondoni, mwili wa Marehemu utaagwa kuanzia saa saba mchana huko mikocheni nyumbani kwa wazazi wake Langa karibu kabisa na Hospitali ya AAR.
MAJINA NA KAMBI ZA JESHI WALIKOPANGIWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA 2013...TAREHE YA KURIPOTI NI 24 MWEZI HUU

MAJINA NA KAMBI ZA JESHI WALIKOPANGIWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA 2013...TAREHE YA KURIPOTI NI 24 MWEZI HUU

TANGAZO
MKUU WA JKT MEJA JENERALI RAPHAEL MUHUGA ANAWAITA VIJANA 10,849 WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA MWAKA 2013 KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KAMA IFUATAVYO:-

1. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOPATA DIVISION I NA DIVISION II.

2. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOSOMA MASOMO YA MCHEPUO WA SAYANSI NA KUPATA DIVISION III.

3. VIJANA HAO WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT TAREHE 24 JUNI 2013 BILA KUKOSA. AMBAYE HATARIPOTI ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

4. TANGAZO HILI HALIWAHUSU VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA 2013 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA UNGUJA NA PEMBA. AIDHA, SHULE 27 AMBAZO VIJANA WAKE WAMEHITIMU MAFUNZO YA JKT AWAMU YA KWANZA HAZIHUSIKI.

5. VIJANA HAO WATUNZE TIKETI ZAO KWA AJILI YA KUREJESHEWA NAULI WATAKAZOTUMIA MARA TU WATAKAPORIPOTI VIKOSINI.

6. TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA HAPA NCHINI.


Zifuatazo  ni  selection  za  kambi  walikopangiwa

 

"NAFIKIRIA KUAHIRISHA SHOW YANGU ILA SI KWA KUMUOGOPA MWANAMKE"...MWANA FA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Mwana FA anafikiria kuahirisha shoo yake ya kesho kufuatia kifo cha msanii mwenzake wa kizazi kipya Langa Kileo, kilichotokea leo  jijini Dar es Salaam.  

Mwana FA anafikiria kuahirisha shoo yake ya kesho iliyopangwa kufanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na tayari ameanza kuwasiliana na meneja wake kwa ajili ya hatua hiyo.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Mwana FA kuahirisha shoo yake, awali ilipaswa kufanyika Mei 31 mwaka huu lakini ikaahirishwa kutokana na kifo cha aliyekuwa msanii mwenzake wa Bongo Fleva Albert Mangwea.


Hata hivyo Mwana FA ametoa tahadhara ya kejeri juu ya hatua hiyo huku akimtupia madongo mhasimu wake mkubwa Mwanadada Lady Jay Dee...

Katika taarifa yake aliyoitupia katika mtandao wa kijamii wa Facebook Mwana FA amesema kwamba:

7 minutes ago via mobile · Like Mwana FA Halisi : "Msiba wa mwana HIPHOP mwenzetu Langa unanifanya nifikirie kuahirisha show ya kesho. Nawasiliana na manager wangu kisha nitawajuza ,but si kwa kumuogopa mwanamke,Let it be clear" 

POST ZA MWISHO ZA FACEBOOK NA TWITTER NA VIDEO YA MWISHO YA MAREHEMU LANGA KILEO

Ikiwa ni siku chache baada ya kuondokewa na mpendwa wetu Albert Mangwea, tasinia ya Muziki wa kizazi kipya imepata pigo jingine  kubwa kwa kuondokewa na msanii wa Hip Hop anaejulikana kwa jina la Langa Kileo.
 Langa  amefariki dunia  akiwa  katika  hospitali ya  Taifa  ya  Muhimbili  baada ya  kulazwa  jana  akisumbuliwa  na  malaria  kali
Zifuatazo  ni post za mwisho za facebook na twitter pamoja na video yake mpya ya marehemu Langa

JINAMIZI LAENDELEA KUTANDA KWA WASANII WA HAPA NCHINI KWETU

Aminiel Aligaesha ambae ni Afisa Uhusiano wa hospitali ya Taifa Muhimbili amethibitisha kwamba msanii Langa amefariki dunia June 13 2013 saa kumi na moja jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo toka juzi jioni ambapo kutokana na sababu za kimaadili kwenye tiba, Muhimbili hospitali hawawezi kusema rapper huyu alikua anaumwa nini bali ndugu ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo.

Kwenye maelezo aliyoyatoa kwa millardayo,  Aminiel amesema Marehemu Langa alipokelewa kwenye idara ya wagonjwa wa magonjwa ya dharura usiku wa kuamkia jana na kupatiwa huduma ambapo leo June 13 2013 ndio alihamishiwa kwenye chumba cha wagonjwa Mahututi na baadae kufariki dunia.

            

MSHANA JUNIOR: MSIBA WA MANGWEAH WAIBUA MAMBO

MSIBA WA MANGWEAH WAIBUA MAMBO:  Hatimaye wale maasimum wa kubwa ambao kila mara wamekuwa wakitupia maneno ya kejeli na dharahu katika nyimbo za Bongo Flava walikutana ka...

Wednesday, 12 June 2013

JIFUNZE VIPENGELE MBALIMBALI VYA RASIMU YA KATIBA MPYA

              Ndugu zangu kuanzia leo na ksiku zijazo natarajia kuwaletea vipengele mbalimbali vya rasimu ya katiba mpya na kuvitolewa uchambuzi ili mpate kujifunza.
Kwa kuanza leo nitaanza na ibara ya75. Mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya
‐ 30 ‐
            Madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa:
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa
Katiba hii na sheria za nchi;
(b) ni mwenye akili timamu;
(c) angalau mmoja kati ya wazazi wake ni raia wa kuzaliwa wa
Jamhuri ya Muungano;
(d) wakati wa kugombea, ana umri usiopungua miaka arobaini;
(e) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii;
(f) anayo angalau shahada ya kwanza ya chuo kikuu
kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi;

(g) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha
siasa au mgombea huru;
(h) sera zake au sera za chama chake si za mrengo wa kuligawa
Taifa kwa misingi ya ukabila, udini, rangi au jinsia;
(i) ni mwadilifu na anafuata maadili ya Taifa.
   
           Kipengele F cha ibara hii ya 75 kinachoelezea sifa za RAISI kinasema ni lazima mgombea awe amehitimu SHAHADA ya kwanza katika chuo kinachotambulika na serikali.Kwa hatua hii nawapongeza sana serikali na tume ya mabadiliko ya katiba kwani Elimu ya mgombea wa uraisi ni swala muhimu sana katika kutathmini weledi na uwezo wa kiutendaji wa mtu.