Recent

JIFUNZE MAMBO MBALIMBALI YATAKAYOKUPA MAARIFA NA UJUZI MAISHANI

Thursday, 8 September 2016

Tazama picha Hoteli mpya Tanzania, wateja hulipa shilingi milioni 22 kwa usiku mmoja


Hoteli hii iko katika kisiwa cha Thanda kusini mwa Tanzania, ina vyumba 5 vya kulala ambapo itakugharimu shilingi milioni 22 kulala hapo kwa usiku mmoja. 

Hoteli hii inakadiriwa kuwa na ukubwa wa ekari 20 ikiwa imezungukwa na viumbe mbalimbali wakuvutia waliomo ndani ya maji. 

Hoteli hii inapakana na kisiwa cha Mafia, unaweza kufika kwa kutumia helikopta kutokea Dar es salaam, au kwenda kwa ndege hadi Mafia na kisha kutumia Boti maalum kwa ajili ya wateja. 

Ukiwa katika hoteli hii unaweza kufurahia mambo mbalimbali kama kuogelea, uvuvi, diving. 

Hoteli hii inamilikiwa na Christin na Dan Olofsson kutoka nchini Sweden. Walikuwa na ndoto za kutafuta eneo ambalo halijakaliwa na watu na kutengeneza sehemu tulivu ya kupumzika na ndipo wakalipata eneo hilo Tanzania.

0 comments:

Post a Comment