Recent

JIFUNZE MAMBO MBALIMBALI YATAKAYOKUPA MAARIFA NA UJUZI MAISHANI

Sunday, 4 September 2016

Je wajua? Bongo: Top 3 Celebrities wenye pesa chafu


Number 1: Masanja mkandamizaji-
Najua wengi kwa haraka haraka mlidhani hii namba itakuwa ni ya Diamond lakini La hasha, Masanja ni comedian maarufu Tanzania aliyewekeza kwenye miradi ya mpunga huko mbeya na pia anamiliki mgodi wake wa dhahabu,
Ni watu ambao hawana akili pekee watabeza juhudi za Masanja....Wakati mnapiga kelele mjini yeye yuko porini analima mpunga, wakati mnashinda vijiweni yuko polini anatafuta dhahabu, Wakati mnakula KFC yeye yuko busy anauza wali nyama na sahivi kafungua Burger points, Mwisho wa siku mnapiga kelele sijui unga sijui nini. hii pia imethibitishwa pale ambapo huyu bwana ana bmw x6 model ya kisasa na yenye bei kali kuzidi la mpinzani wake diamond platnumz


Number 2: Diamond platnumz-
Bongo tunamuita simba ila Afrika wanamuita king of pop, Hakuna msanii Bongo anayelipwa pesa nyingi kwa show moja kama Diamond, Kumekuwa na wasanii wenzake kama kina Ali kiba, Christian bela, n.k waliofanya mziki muda mrefu kuzidi yeye lakini kumkuta kimafanikio sio leo, Mafanikio hayaongelewi bali yanaonekana kijana ana nyumba yake nzuri madale na pia amewekeza katika kununua nyumba , pia kwa sasa ana label ya WCB ambayo amini usiamini inamuingizia pesa kila kukicha.


Number 3: Lady jay dee:
Miaka nenda rudi wasanii wenzake wanamkuta na wanamuacha, Kipaji anacho nauzuri wake kinamuingizia pesa za kutosha, ukiachana na muziki pia ni mjasiria mali ambae biashara zake zinamuingizia pesa chafu, Dada anamiliki ndinga matata range rover evoque model ya kisasa ambayo ni ndoto za mchana kwa wasanii wa kawaida

2 comments: