Tuesday, 13 September 2016
Home »
Elimu
» Tamko la Umoja wa Vijana Wanaosubiria Ajira Tanzania (UVITA) Kuhusu ajira za walimu mwaka 2016
Tamko la Umoja wa Vijana Wanaosubiria Ajira Tanzania (UVITA) Kuhusu ajira za walimu mwaka 2016
*UMOJA WA VIJANA WANAOSUBIRIA AJIRA (UVITA)*
Tumekuwa tukidharaulika sana mitaani kwa kukosa *ajira* lakini pia kwa kusemwa vibaya kuwa sisi ni wazembe kwanini hatujishughulishi na mambo mengi ya kujipatia kipato hadi tuanze kulalamika lalamika kudai ajira.
Nataka niwakumbushe kuwa sisi tulimaliza mwaka *2015* kuanzia mwezi wa tano (may )hadi mwezi wa nane ( august . Kuanzia mwezi November hadi January ndio tulikuwa tunamaliza graduation kwa kila chuo.
Kwa hiyo tulianza harakati za kutafuta temple na kazi ndogo ndogo hasahasa kuanzia mwezi January. lakini kabla hatujakaa sawa tukapata kauli kutoka kwa naibu waziri tamisemi ndugu *Selemani Jafo* kuwa ajira zingetoka mapema sana mwaka huu. (wenye nia ya kufuga waliacha , wenye nia ya kulima waliacha, waliokumbana na mikataba walikataa ) kutokana na kauli ya Naibu waziri.
Kuanzia hapo tukambana na matamko mengi kitu ambacho sio tu kilitufanya kusite kuanzisha miradi lakini pia kilitupa hasara kwa mfano (akiwa bungeni waziri *Simbachawene* alisema ajira zitatoka mwezi mei) vijana walikopa nauli kwenda kufuata vyeti , sehemu mbalimbali ,wengine wachache waliobahatika kupata mkataba wa muda mfupi walisitisha mikataba *Mimi binafsi niliuza shamba langu* kwa lengo la kufuata vyeti vyangu ili kujiandaa. kwa masikitiko makubwa kabisa ajira hazikutoka ,wengi tulikata tamaa tuliingia kwenye madeni ,tulipata mkanganyiko wa mawazo na wengine walikosa vibarua.
lakini wakati tunasema ngoja sasa tuanze kufiriki kwa upande wa pili ,Mh rais anatuambia tusubiri baada ya mwezi mmoja au miwili (ni vigumu kuingia mkataba private wakati Rais kakuambia usubiri miezi miwili ). lakini cha ajabu miezi miwili hiyo imepita na hakuna lolote kiukweli tumesikitishwa sana na ahadi hewa ,tumedhalilishwa kisaikolojia , Mimi sasa nina vidonda vya tumbo , mana shamba langu niliunza.
BUNGENI DODOMA: N/ Waziri TAMISEMI Jaffo asema wahitimu shahada za sayansi ambao si walimu kupatiwa mafunzo wakafundishe, walimu wa ziada sanaa kupelekwa msingi
Kuna wasiwasi walimu wa sanaa kuwa idadi yao imepita mahitaji yaliyopo kwa sasa?
sasa *UVITA* inataka kujua mambo yafuatayo :-
1. *Je ajira za walimu mwa huu zipo au hazipo.*
2. *Kama zipo, Ni lini ajira hizo zitatangazwa?*
3. *Kama hazipo UVITA tunataka tupewe taarifa mapema (wiki hii) ili kuondekana na high depression tuliyokuwa nayo*
Sio kwamba sisi walimu ni wajinga sana hapana ila tumelelewa katika misingi ya *kizalendo* *hatulilii ajira tunalilia kwenda kumsaidia mtoto wa maskini*. Jua kwamba kuna walimu walikaa zaidi ya miezi mitatu hawakupata mishahara ila kwa kuwa nia yao kubwa ni kumkomboa maskini waliendelea kufundisha.
Je tukiamua kuingia mikataba katika shule za private mtoto wa maskini kama mimi kule kaliua Tabora atafundishwa na nani ?
*Sasa serikali iseme tu ..kuwa mwaka huu hakuna ajira , na watoto wa maskini huku ngara watajua wenyewe*. waone kama sisi tutalalamika tena kuhusu ajira.
inasikitisha kuona uzalendo wetu ndio unatuumiza.
~MUNGU MBARIKI RAIS WETU, ILI IKIWEZEKANA ATOE TAMKO, SI KAMA TUPENDAVYO SISI, BALI NI KWA MAPENZI YAKO EE MUNGU MUUMBA WA MBINGU NA NCHI~
0 comments:
Post a Comment