Inawezekana ukawa ni miongoni mwa watu ambao wanapata kero pale simu unapoiwasha na ikatumia muda mrefu kuwaka. Sasa good news ni kwamba simu mpya itakayozinduliwa ya Phantom 6 itakuwa na uwezo wa kuwaka ndani ya sekunde 35 tu, kitu ambacho kimekuwa mtihani kwa simu nyingine ambazo huchukua zaidi ya dakika moja na sekunde tisa.
Watuamiaji wengi wa simu wamekuwa wakijaribu kufanya simu zao ziwake haraka au kuwa na uwezo mkubwa wa processor kwa kuweka application kadhaa kama Bootmanager au Greenify na hata kujaribu mipangilio tofauti kwenye “Developer Setting”ili mradi ziwake haraka. Application hizo zimeweza kujiwekea umaarufu ila huwa hazifanyi kazi kwa watu wote.
Phantom itakayofuata imeonyesha kuongezeka kwa uwezo wa processor na kupiga hatua kubwa ikiiacha kwa mbali toleo lililoitangulia.
Unaweza kuifuatilia kwa undani zaidi ingizo hili jipya la simu ya Tecno phantom 6 Unaweza kupitia katika kurasa za Tecno za mitandao ya kijamii.
Twitter: https://twitter.com/TECNOMobileTZ
0 comments:
Post a Comment