Recent

JIFUNZE MAMBO MBALIMBALI YATAKAYOKUPA MAARIFA NA UJUZI MAISHANI

Sunday, 31 July 2016

Je wajua vyakula vya aina 6 vinavyozeesha ngozi yako?Hivi hapa.....



Vifuatavyo ni vyakula 6 vinavyozeesha ngozi na unashauriwa kuvitoa katika mlo wako:

1. Chumvi
Chumvi hasa yenye madini ya iodine ni mbaya sana kwa afya ya ngozi. Inasababisha chembechembe za nyama katika ngozi kuvimba.

2. Sukari
Sukari japo tunaipenda sana ni adui mkubwa wa afya ya binadamu. Inadhoofisha mfumo wa kinga za mwili. Kiasi kingi cha sukari mwilini kinafanya ngozi kuwa kavu na kufanya mwili utengeneze makunyazi kwa sababu inaharibu kemikali ya collagen na elastin ambazo zinafanya kazi ya matengenezo ya ngozi kuifanya isiharibike na kuwa chakavu.

3. Vyakula Vya Kukaangwa
Vyakula vya kukaangwa kama chipsi,nyama za kukaanga vinasababisha uingizaji wa mafuta mengi mwilini. Mafuta haya yenye vitu vinavyoitwa “Free Radicals” yanasababisha uzibaji wa vijitundu katika ngozi. Ukiachia ngozi mafuta mengi mwilini yanasababisha madhara mengi mengine yakiwemo magonjwa ya moyo na kisukari.

4. Mkate Mweupe,Tambi Na Keki
Vyakula hivi vina kemikali ya glucemic kwa kiwango kikubwa ambayo inaleta madhara ya magonjwa ya ngozi (Ugonjwa wa madoa katika ngozi)

5. Pombe
Unywaji wa pombe unasababhisha kupoteza maji mengi mwilini kwa njia ya mkojo na huleta madhara mabaya kwa ngozi kwa kuifanya iwe kavu.

6. Kahawa (Caffeine)
Kemikali ya caffeine iliyomo katika kahawa na vinywaji vingine inasababisha ukosefu wa maji ya kutosha katika ngozi na kuifanya iwe kavu. Lakini pia caffeine inasababisha utengenezwaji wa kemikali ya cortisol ambayo inachangia uzeekaji wa ngozi.

Saturday, 30 July 2016

Zitto Kabwe atoa maelekezo Kwa Wanachama wa ACT- Wazalendo Kuhusu Kauli ya Rais Magufuli Jana Singida


Tangu kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Utawala mpya umekuwa ukifanya kila juhudi kuminya uwezo wa Vyama vya Siasa kufanya Kazi zake kwa kisingizio kuwa huu ni wakati wa kufanya Kazi na kwamba Siasa zisubiri mwaka 2020. 

Chama chetu kilipinga kwa nguvu zote uzuiaji huu wa shughuli za kisiasa kwani ni kinyume cha Katiba ya Nchi na Sheria ya Vyama vya Siasa, sheria namba 5 ya mwaka 1992 kama ilivyofanyiwa marekebisho Mara kwa Mara.

Mnamo tarehe 5 Juni 2016 Chama chetu kilifanya Mkutano wa Hadhara Mbagala jijini Dar Es Salaam na kutangaza Operesheni Linda Demokrasia. Lengo la Operesheni hiyo ( Tamko la Mbagala 2016 ) ni kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa Nchi ya kidemokrasia na kuepuka mwelekeo wa Utawala wa Imla ambao ni utawala wa kidikteta. Chama chetu asili ya uundwaji wake ni kupinga tabia za kidikteta tulizokumbana nazo ndani ya Vyama tulivyokuwamo. 

Hivyo ilibidi tuwe mstari wa mbele kupinga dalili zozote za kuielekeza Nchi kwenye Uimla. Vyama unaweza kuunda utakapo, Nchi huwezi kuiunda ndio maana ni LAZIMA Sisi Kama wanachama wa Chama cha Wazalendo kupinga kwa nguvu zote kuminywa kwa Demokrasia na kuilinda kwa nguvu zetu zote.


Kufuatia Tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano kwamba shughuli za kisiasa zimezuiwa kwa niaba yenu nilitaka Vyama vyote vya Siasa nchini na wadau wengine wa demokrasia kuungana kwa pamoja kukataa Tamko hili ambalo linavunja Katiba ya Nchi ambayo Rais ameapa kuilinda na kuitetea. Wito wetu unanukuliwa hapa chini;

"Tunatoa wito kwa Vyama vyote vya siasa nchini kuunganisha nguvu katika kuhakikisha tunapigana vita [ dhidi ya udikteta] pamoja. Huu ni wakati wa vyama vya siasa na wanasiasa kuacha tofauti zao na kupambana kulinda uhuru wa kufanya siasa wakati wowote kwa mujibu wa Sheria."

Hata hivyo, hakuna Kiongozi wa Chama chochote kile ambaye aliona umuhimu wa kuunganisha nguvu na hivyo kujikuta kila Chama kinaendelea na operesheni zake. 

Viongozi wetu akiwemo Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu walifanya juhudi zote kuwasiliana na watendaji wenzao wa Vyama vingine ili kufanya Kazi pamoja japo kwa uratibu lakini hatukupiga hatua yeyote ile.

Hivyo, Sisi sio sehemu ya operesheni yeyote ile iliyotangazwa na Chama kingine chochote kile isipokuwa Operesheni Linda Demokrasia ambayo sasa itaitwa Tamko la Mbagala la Juni 5, 2016.

Akiwa ziarani mkoani Singida, Rais amefafanua agizo lake la kuzuia mikutano ya kisiasa. Rais amesema kwamba hajazuia wabunge na madiwani kufanya mikutano ' KWENYE MAJIMBO YAO'. Kwanza Rais hana mamlaka ya kuruhusu au kuzuia Kazi za Wabunge na madiwani. Haya ni mamlaka ya KATIBA na sheria za Nchi. Hivyo ufafanuzi wake hauna maana yeyote ile.

Jambo la kushtusha ni agizo la Rais kwamba Wabunge hawana mamlaka ya kufanya mikutano nje ya majimbo yao. Hii ina maana hata Viongozi wa kisiasa ambao sio wabunge hawataruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa. Hii HAIKUBALIKI. 

Anna Elisha Mghwira ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa, anazuiwaje kufanya mikutano na wanachama wake nchini? Anazuiwaje kuongeza wanachama? Lakini mama Anna Mghwira aligombea Urais, kwanini asifanye mikutano kuwashukuru waliompa Kura japo hazikutosha?

Uchambuzi wa kitaalamu
Ni dhahiri Serikali ya Awamu ya Tano na sasa Chama tawala wameamua kubadili mwelekeo wa Nchi kisiasa ( kwa kubana uhuru wa kidemokrasia ) na kiuchumi ( kwa kuelekeza nguvu kwenye uchumi unaoelekezwa/endeshwa na dola ). Udhibiti wa Vyama vya Siasa ni moja ya hatua ya udhibiti wa jamii kwa ujumla wake. 

Siku za usoni tutaona udhibiti wa waziwazi wa vyombo vya habari na kwa sasa tunaona namna Asasi za Kiraia ( CSOs) zilivyo kimya tofauti na miaka michache ya nyuma. Hizi zimejiweka kimya zenyewe na zitakazoinua sauti zitafuatiliwa na dola. Yote haya yanaturudisha nyuma katika katika kujenga Tanzania ya Kidemokrasia na yenye Maendeleo.

Utawala wowote ' regime ' hutaka kupata nguvu ya wananchi katika kujijengea uhalali. Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kuichukua vita dhidi ya ufisadi kama njia ya kujijengea uhalali na kwa kweli wananchi wengi waliochukizwa na vitendo vya kifisadi wanaunga mkono juhudi hizo. 

Katika ziara yake ya Singida, Rais amenza kutumia maneno kama ' mabeberu ' na ' Maadili ya Mwalimu Nyerere ' maneno ambayo hayajawahi kutamkwa na kinywa chake. Hii inaonyesha kuwa Rais anaanza kukua/kukuzwa kiitikadi na hii itampa uhalali zaidi mbele ya jamii. 

Hata Uamuzi wake wa kutekeleza maamuzi ya kuhamia Dodoma, na iwapo atatekeleza, itamjengea zaidi uhalali. Rais atautumia uhalali huu kujikita katika utawala na kuminya zaidi Demokrasia.


Maelekezo ya Kiongozi wa Chama ( KC )
1. Chama cha ACT Wazalendo kiliundwa kwa madhumuni ya kurejesha Nchi kwenye misingi. Kupitia Azimio la Tabora linalohuisha Azimio la Arusha tumeeleza misingi hiyo kwa kina. Naelekeza kwamba wanachama wote wa ACT Wazalendo wasome, kuelewa na kujadili Azimio la Tabora na kuchambua muktadha wake katika mazingira ya sasa ya Siasa za Nchi yetu.
 
2. Kila Mwanachama wa ACT Wazalendo asione aibu kuunga mkono maamuzi yeyote ya Serikali au Chama kingine cha Siasa yanayoendana na Azimio la Tabora hususan vita dhidi ya ufisadi na kurejeshwa kwa Miiko ya Uongozi.
 
3. Kila Mwanachama wa ACT Wazalendo akatae kwa namna anayoweza lakini kwa Amani mbinu zozote za kuminya Demokrasia nchini. Tamko la Mbagala la kulinda Demokrasia litumike kuongoza juhudi hizo. Chama chetu hakijatangaza maandamano na hivyo wanachama wetu wasiingie katika mambo hayo. 

Hata hivyo kila mwanachama wa Chama chetu aandike barua kwa Rais Magufuli kwa namna anavyoona yeye kumtaka aache kuingiza Nchi kwenye utawala wa Imla. Chama chetu kina wanachama 431,120 wenye kadi. Ikulu ikipata barua 200,000 kutoka kila kona ya Nchi itafunguka macho.

Mwisho
Nawataka wanachama wa Chama Cha ACT Wazalendo kukumbuka kuwa uasili wa Chama chetu ni kupinga kuburuzwa, ufisadi na Siasa za ujanja ujanja. Tujitahidi kwa nguvu zetu zote kutofanya yale ambayo Sisi tumeyakataa.

Viongozi wa kuchaguliwa kwenye vyombo vya uwakilishi Kama madiwani na wabunge wawe makini sana kutii Chama na misingi ya chama. 

Tuwe mstari wa mbele kupinga ufisadi kwani rushwa ni adui wa Haki. Tuwe mstari wa mbele kutaka kurejeshwa kwa Miiko ya Uongozi. Sisi ndio Chama pekee chenye itikadi iliyo wazi. Tusiammie itikadi yetu popote tulipo na bila woga wala aibu.

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kiongozi wa Chama
30/7/2016

Wednesday, 27 July 2016

Vitu vizuri ambavyo madikteta 05 wamefanya na kuacha historia duniani


1:ADOLF HITLER
Pamoja na yote, Hitler atakumbukwa kama kiongozi wa kwanza kuanzisha harakati za Kuzuia Matumizi ya Sigara ili kuepusha madhara yake kwa raia (Anti-smocking compaign). 

Ndie aliyehamasisha wanasayansi wake kufanya utafiti wa kisayansi wa madhara ya sigara. 1943 mwanasayansi wa kiNAZi aligundua sigara Inasababisha KANSA na Aliokoa maisha ya wanawake zaidi ya 20000. Sifa za ugunduzi huu ziliyoyoma maana vita vilipoanza mradi ukahafifishwa na kumpa sifa ya ugunduzi huo mmarekani baada ya anguko la wanazi.


2: Genghis Khan: ALIANZISHA SHERIA NA UHURU WA KIDINI
Huyu jamaa aliua watu zaidi ya 40 Millioni karibu 12% ya watu wote waliokuwepo duniani maiti hao wanasadikika kudisturb kiwango cha carbon dioxide duniani miaka ya 1208.Pamoja na yote Huyu jamaa alianzisha Sheria(LEgal Code) zilizokuwa zinafanya kazi dola yake yote ya MONGOL na Hadi yeye akikosea ashughulikuwe. Pia aliweka uhuru wa dini na hata kuondoa taasisi za dini zisilipe kodi.



3:MUAMMAR GADDAFI: alianzisha Mradi Mkubwa wa umwagiliaji kuwahi kuwepo Duniani.
Mwaka 1969 huyu jamaa aliingia madarakani kwa mapinduzi na kuangamiza kila aliyempinga hata kutuma vikosi vya wauwaji kuwatafuta maadui zake nje ya nchi hiyo. Nchi nyingi za magaharibi zilimuona kama mtu hatari. 

Lakini chini ya Utawala wake wa chuma, Watu walisoma bure, walitibiwa bure, Umeme bure, Wakati anaingia madarakani mji wa Benghazi ulikuwa hauna maji, akaanzisha Mradi wa kuchimba mto hadi huko uliowapa maji 70% ya walibya. ALikuwa na mpango wa kufanya jangwa lote liwe la kijani hadi pale figisu za wazungu zilipoanza miaka ya 90 na vikwazo pia kufuatiwa na mapinduzi ya 2011.


4:FIDEL KASTRO ALIFANYA MAPINDUZI YA AFYA NA ELIMU CUBA
Alipoingia madarakani, alifanya nchi ya Cuba kuwa ya chama kimoja. Huku maelfu wakikimbilia uhamishoni, wengine wakifungwa na wapinzani wake kuuawa.
Cha ajabu, CUBA na US wote wana LIfe expectance sawa ingawa Marekani wametumia matrillion 20% zaidi. Akiingia madarakani 1959 1/4 ya Cuba walikuwa wajinga lakini leo Hakuna mtu mzima ambaye ni ILLITERATE/mjinga. 

Aliweka mipango mikali kupambana na majanga ya kitaifa. Mfano Kimbunga GUSTAV hakikuua mtu hata mmoja Cuba lkn kilivyofika Marekani kiliua watu zaidi ya 26 jimbo la Louisiana.


5:AUGUSTO PINOCHET: "kafanya muujiza wa mapinduzi ya kiuchumi CHILE"
Alipoingia madarakani watu 3000 walipotea hadi kesho, kafunga na kutesa watu zaidi ya 28,000 wakiwemo Rais wa sasa na mama yake. Mwaka 1973 aliingia madarakani Baada ya mporomoko wa uchumi kwa njia ya mapinduzi makali ya kivita.

Ndipo aliwaajiri kikundi cha vijana graduates na wataalamu wa uchumi kutoka Chuo kikuu cha Chicago "Chicago boys". kipindi hiki kinajulikana duniani kama "CHILEAN ECONOMIC MIRACLE" baada ya Mfumuko wa bei kushuka kutoka asilimia 375 hadi 9.9 ndani ya miaka 7. JAPO aliacha pengo kubwa kati ya maskini na matajiri.


Karibu kwa maoni, michango na changamoto.

Kila kibaya kina zuri lake.



Tukio la Ujambazi lililofanikiwa zaidi, kusisimua na kuushangaza Ulimwengu


Mwaka 2003 lilitokea tukio kubwa zaidi la ujambazi ambalo labda ndio lililotumia akili na maarifa zaidi pengine kushinda tukio lolote la ujambazi kwa miaka 50 iliyopita.. Tukio hili lilishuhudia wahusika wakitokomea na vitu vyenye thamani ya zaidi ya Bilioni 200 (100 mln USD)!
Uthubutu, ubunifu, akili na maarifa yaliyotumika kutekeleza tukio hili limefanya mpaka kampuni ya utengenezaji filamu ya Paramount Pictures kununua haki za hadithi ya tukio hili ili watengeneze filamu itakayo husu mkasa mzima wa tukio hili..

TUKIO LENYEWE

Mwanzoni mwa mwaka 2000 mfanyabiashara wa madini (almasi) Leonardo Natarbartolo alifungua ofisi mjini Antwerp nchini ubelgiji, mji ambao ndio kituo cha biashara ya madini ya almasi ulimwenguni.. Ofisi yake ilikuwa katikati kabisa ya kitovu cha mitaa ambayo ndio hasa biashara ya almasi hufanyika. Natarbartolo alijihusisha hasa katika manunuzi ya kiwangi cha kawaida cha almasi (small deals) lakini jambo ambalo watu hawakulifahamu ni kwamba walikuwa wamemkaribisha moja kati ya manguli wa wizi wa almasi ulimwenguni!
Kutokana na kujitambulisha kama mfanya biashara mwenzao, Natarbartolo alipata fursa ya kuingia katika Kuba (vault) za wafanyabiashara wengine ili aweze kukagua mali kabla ya kuinunua na aliutumia fursa hii kuyasoma mazingira ya Ofisi hizo zilizo hifadhi madini na kuja kufanya uhalifu kesho yake..
Natarbatolo aliishi hivi mjini Antwerp kwa miezi kadhaa kabla hajakutana na mfanyabiashara ya almasi Myahudi ambaye kukutana kwao kulipelekea kufanikisha tukio ambalo liliushangaza ulimwengu na limeendelea kuushangaza ulimwengu mpaka leo hii..



MAANDALIZI

Mwaka mmoja baada ya Natarbatolo kuingia Antwerp, siku hiyo akiwa kwenye mgahawa akinywa kahawa alifuatwa na Mfanyabiashara wa Kiyahudi ambaye alimuomba wazungumze faragha kuhusu biashara muhimu. Baada ya kukaa nae chemba Myahudi akamueleza amza yake kuwa anataka amshirikishe katika tukio la ujambazi na alimuuliza kama anahisi Vault ya Antwerp Diamond Center inaweza kuibiwa... Natarbartolo akamjibu kwa kifupi kuwa atamjibu swali hilo kama yuko tayari kumlipa dola laki moja! Na Myahudi huyo akakubali

Siku mbili baadae Natarbatolo alielekea ilipo Main Vault ya Antwerp Diamond Center (kumbuka kutokana na yeye kujitanabaisha kama mfanyabiashara ya almasi kwa mwaka mmoja aliokaa Antwerp hivyo alifanikiwa kujisajili ili aweze kuhifadhi almasi zake katika Main Vault ya Antwerp)..
Kitu ambacho watu wote wakiwepo walinzi hawakikugundua ni kwamba katika mfuko wa pembeni wa suti yake aliweka peni ambayo inaonekana kama peni ya kawaida lakini ilikuwa ni peni maalumu iliyokuwa na kamera ndogo ya siri.. Kamera hii ilimsaidia Notarbartolo kurekodi mandhali yote ya ndani ya vault na jinsi ulinzi ulivyo...
Kesho akajutana na yule myahudi na kumpa jibu lake kuwa ni immposible kuvunja na kuiba main vault ya Antwerp inayohifadhi almasi zote zilizopo katika mji huo.. Akampa ile peni ambayo imerekodi mandhali ya Vault pia akampa na maelezo ya mdomo kwanini haiwezekani kuiba katika ile vault na akamsisitiza zaidi juu ya matabaka ya ulinzi (security levels) ambayo yana protect vault hiyo. Matabaka hayo yapo kama ifuatavyo..

1) Combination dial ambayo unatakiwa uingize tarakimu nne za siri

2) Sehemu ya kuingiza funguo maalum

3) Sensor ya mitetemo (seismic sensor)

4) geti la Chuma lililo sambamba na mlangi

5) sensor ya sumaku (magnetic sensor)

6) Kamera ya nje ya mlango

7) Keypad ya kuzima alarm

8) sensor ya mwanga (light sensor)

9) Kamera ya ndani ya vault

10) sensor ya joto na mjongeo (heat & motion sensor)

Jumlisha; walinzi na ulinzi unaozunguka jengo hilo.. Natarbartlo akmsisitizia yule myahudi "..it is immposible to rob the Antwerp diamond center vault"..

TUKIO LILIVYOTEKELEZWA

Miezi kama mitano ikapita ndipo Notarbartolo akapokea simu kutoka kwa yule myahudi na safari hii alimuomba wakutane nje kidogo ya mji wa Antwerp... Baada ya kuonana yule myahudi alimchukua Notarbatolo mpaka kwenye nyumba moja inayofanana na ghala kubwa.. Ndani yake Notarbatolo alikuta kitu ambacho hakutegemea kabisa... Yule myahudi alikuwa ametengeneza replica inayofanana kabisa na main vault halisi ya kuhifadhia almasi ya hapo mjini Antwerp.. Pia akamtambulisha kwa watu watatu ambao pia aliwakuta hapo! Natarbartolo amekataa kabisa mpaka leo hii kutoa majina halisi ya watu hawa lakini anawasimulia kwa nicknames walizokuwa wanatumia, kulikuwa na The genius (huyu ni mtaalamu wa mambo ya kidigitali na eletroniki), kulikuwa na The monster ( huyu alikuwa ni mekanika na mtaalamu wa umeme) na kulikuwa na mzee wa makamo ambaye walimuita The King of Keys (huyu ni mtaalamu wa kufungua vitasa na makufuli ya aina zote pamoja na kufoji funguo)..
Yule myahudi aliwaambia kazi ya ile replica ni wao wafanye mazoezi na kuitafiti na hatimae wajue namna gani wataweza kuingia ndani ya vault ya Antwerp pasipo kugundulika..

Iliwachukua miezi mitano Natarbartolo na wenzake kufanya mazoezi na kutengeneza perfect plan itakayowawezesha kuingia katika vault na kuiba pasipo kugundulika..


SIKU YA TUKIO..

Siku moja kabla ya tukio, yaani February 14 2003 Notarbartolo alienda mchana kwenye vault kana kwamba kuna almasi ameenda kuhifadhi lakini akajitahidi akae karibu na kifaa cha kuhisi joto na mjongeo (heat/motion sensor) na kwa kutumia hair spray aliyoificha ndani ya jaketi lake akapulizia juu ya kifaa hicho hivyo kukifanya kisiwe na uwezo wa kuhisi mabadiliko yoyote ya joto au movement ndani ya vault...

Ilipowadia siku ya tukio lenyewe.. February 15
Notarbartolo na wenzake waliendesha gari mpaka karibu kabisa na jengo lenye vault! Jengo lilikuwa na ulinzi mkali kwa mbele lakini nyuma ya jengo hakukuwa na ulinzi mkubwa kwani watu wa ulinzi walikuwa na imani kubwa sana na teknolojia yao inayosaidia kulinda jengo lao..
Wote wakashuka kwenye gari isipokuwa Notarbatolo alibaki kwenye gari! Baada ya kushuka wote wakazunguka nyuma ya jengo ambako walitumia ngazi ambayo The genius alikuwa ameificha hapo mchana wake wakapanda mpaka ghorofa ya pili.. Baada ya wote kupanda katika balcony ya ghorofa ya pili ilibidi wakae mbali na madirisha kwani yote yalifungwa vifaa vya kuhisi joto na movement na vikigundua tu kuwa kuna mabadiliko ya joto au movement basi alarm inalia..
Alichokifanya The genius alichukua kitambaa kirefu kilichotengenezwa kwa polyester kujifunika na kusogolea kifaa kile cha heat and motion sensor.. Kutokana na yeye kujifunika kwa nguo yenye material ya polyester hii ilipelekea kifaa kile kushindwa kudetect kilichokuwa kinatokea na alipokifikia karibu kifaa kile akakifunika kabisa na nguo ile kwahiyo korido ikawa iko salama kwa wao wote kupita.. Wakafungua madirisha wakaingia ndani na kuanza kushuka ngazi kuelekea chini kwenye vault..

Baada ya kufika chini nje ya mlango wa vault ambako kulikuwa na giza kutokana na kuzimwa taa.. Wakatumia fursa hiyo kuzifunga kamera kwa mifuko meusi na kisha wakawasha taa.. Baada ya kuwasha taa ilikuwa sasa ni jaribio la kufungua mlango na hapa ndio wanatakiwa kuwa makini zaidi kwani wakikosea kitu kimoja tu maana yake alarm italia na mchezo utaishia hapo..

Kumbuka kuna matabaka kumi ya ulinzi wanayotakiwa wanayotakiwa kuyavuka mpaka waingie ndani.. Tabaka la kwanza ni lile la combination dial ambapo wanatakiwa waingize tarakimu nne za siri! Kabla ya siku hii ya tukio Natarbartolo alifanikiwa kumshawishi muhudumu wa vault wabadilishe mtungi wa tahadhali ya moto (fire extinguisher) jambo ambalo hawakulifahamu ni kwamba mtungi ule ulikuwa na gas ndio lakini ndani yake Natarbatolo aliweka kifaa maalumu kilichokuwa kinachukua data za kamera ya nje ya mlango wa vault! Kwa kutumia kifaa hicho Natarbartolo alinga'amua tarakimu nne za siri ambazo zilikuwa zinahizatijika kuingizwa... Kwahiyo waliingiza tarakimu nne na wakawa wamefanikiwa kwa hatua hii ya kwanza... Bado hatua tisa ili wafanikishe.!

Hatua ya pili chabgamoto ya pili ilikuwa ni namna gani wangeweza kudiable kifaa cha kuhisi usumaku (magnetic sensor) hii yenyewe ilitengenezwa katika katika hali ya kwamba plate moja ya sumaku iliwekwa kwenye mlango na nyingine ilifungwa kwenye ukuta pembezoni mwa mlango kwa maana ya kwamba mlango ukifungwa kunakuwa na magnetic field inatengenezwa pale katikati kwa maana ya kwamba kama mtu ukifungua mlango unadisturb ili magnetic field na alarm inalia...
Kwahiyo alichokifanya The genius alichukua plate ndogo ya aluminium aliyoitengeneza nyumbani alafu akaifunga na tape ya gundi kali na kunasisha katika zile plate za sumaku huku na huku yaani iliyopo ukutani na mlangoni (ametumia aluminium ili asiweze kudisturb magnetic field).. Baada ya hapo akafungua screw na zile plate na kuziweke pembeni ya mlango! Kwahiyo zile plate mbili bado zilikuwa na magnetic field katikati yake lakini zilikuwa zimewekwa pembeni ya mlango..
Kwahiyo tayari matabaka matatu yalikuwa yameshakuwa disabled bado matabaka saba.. Kumbuka kamera ya nje tayari ilishafungwa na mfuko mweusi.

Hatua ilifuata ilikuwa ni kudisable alarm inayo monitor seismic sensor na geti dogo la ndani. Kifaa hiki kilifungwa kama keypad pembeni kwenye ukuta, kilichokuwa kinatakiwa ni kuingiza tarakimu nne za siri kama pale juu kwenye mlango.. Tarakimu hizi za siri nazo walikuwa wameshazifahamu kwa kutumia kile kifaa kilichopo ndani ya fire extinguisher kwahiyo waliingiza tu tarakimu na tayari wakawa wamefanikiwa kudisable tabaka hili..

Shughuli ikabaki kwenye kufungua mlango kwa kutumia funguo.! Funguo iliyokuwa inatumika hapo sio kama funguo hii ya kuweka mfukoni.. Ilikuwa ni funguo kubwa yenye size sawa na mguu wa binadamu!
Sasa ilikuwa ni zamu ya The king of keys kufanya miujiza yake... Kumbuka kuna kifaa chao kile kilichopo kwenye fire extinguisher kinachorekodi kila kinachoendelea kwenye vault kwahiyo kabla ya siku hii ya tukio walikuwa na Picha halisi ya funguo ya mlango ilikuwa inafananaje.. Kwahiyo alichokifanya The king of chains ni kutengeneza funguo inayofanana kabisa na ile funguo halisi.. Lakini kabla hawajaijaribu hii funguo yao ya bandia The king of keys akawaeleza kuwa kwenye zile Picha za video walizonazo aligundua kitu kuwa kabla mlinzi hajafungua mlango ilikuwa lazima aende kwenye chumba kilichopo karibia na hiyo vault na The king of keys alitaka kujua alikuwa anaenda kufanya nini.. The king of keys alipoenda katika chumba kili hakuamini alichokikuta, ulikuwa ni uzembe wa kiulinzi ambao hakuutegemea utokee Antwerp.. Funguo halisi ya kufungua mlango wa vault ilikuwa imewekwa pale inaning'inia.
The king of keys alichukua funguo halisi akarudi kwenye vault na kuwasisitiza wenzake kuwa angeoenda watumie funguo ile halisi.. Kwahiyo wakachomeka funguo na kuizungusha kisha wakazungusha ringi (usukani) wa mlango wa vault na mlango ukafunguka bila hiyana.. Kwahiyo kwa nje ya vault walikuwa wamepita vizingiti vyote na kikibakia geti la Chuma lililopo baada ya mlango.. Geti hili ni mageti fulani hivi yanayotumika kwenye vault nyingi lenyewe linakuwa lina nondo dizaini kama madirisha yetu uswahilini ya nondo na mbao tofauti tu ni kwamba hili lilikuwa ni nondo na chuma pekee hakuna mbao.. Kwakuwa tayari walikuwa wamedisable kifaa cha kumonitor hili geti (pale ukutani unapoingiza tarakimu nne) kwahiyo hapa wakatumia nguvu tu kuliharibu na kuingia ndani..

Kwahiyo kwa walikuwa wamefanikiwa kupita matabaka yote ya ulinzi nje ya vault na wakibakiwa na matabaka machache ya ulinzi ndani ya vault ambayo ni Kamera ya ulinzi, sensor ya mwanga (light sensor) na sensor ya mjongeo na joto (heat & motion sensor)



#2

NDANI YA VAULT..

Baada ya ya kufanikiwa kufungua mlango wa vault kwa mafanikio kabisa sasa changamoto ilibaki ndani ya vault kukabiliana na matabaka matatu ya ulinzi kabla ya kuanza kufungua visanduku vya vilivyohifadhi almasi ambavyo navyo vilihitaji funguo na namba za siri..

Kumbuka kuwa siku moja kabla Natarbartolo alikuwa amepulizia hair spray kifaa cha kuhisi joto na motion! Lakini ile spray ingesaidia labda kwa dakika tano tu kama mtu angeingia na baada ya hapo ingeweza kuhisi kuna mabadiliko ya joto.. Kwahiyo kama wote watatu wangeingia maana yake labda kwa dakika moja au mbili za mwanzo isingehisi kitu lakini baada ya hapo ingeling'amua kuwa kuna mabadiliko makubwa ya joto.. Hivyo badi ilikuwa inatakwa mtu mmoja tu aingie na aweze kudisable system nzima ya zile alarm na hapo ndipo ilikuwa zamu ya The monster ambaye alikuwa ni mtaalamu wa umeme na mekanika (mechanics) kufanya miujiza yake..

The monster alitembea hatua kumi na moja mpaka katikati ya vault kama ambavyo alikuwa amefanya mazoezi kwa takribani miezi mitank kwenye replica waliyokuwa nayo nyumbani.. Baada ya kufika katikati ya vault aliinua mikono juu kugisa dari la vault ambalo hapo juu kulikuwa na kiboksi cha umeme ambaco chenyewe ndicho kilikuwa kinakusanya electric pulse kutoka kwenye vifaa vyote vya ulinzi ndani ya vault na kupeleka kwenye system ya alarm.. Yaani kwa mfano kama light sensor ikihisi kuna mwanga kwenye vault basi itatuma electric pulse mpaka kwenye kifaa hiki na chenyewe kitatuma taarifa juu kwenye system ya alarm na alarm italia..

Kwahiyo alichokifanya The monster ni kufungua mfuniko wa kifaa hiki kisha akazichuna plastiki ya juu inayofunika nyaya na hatimae zile nyaya zikawa wazi, kisha akachukua kipande cha nyaya alichokuja nacho na kufunga kwa ustadi kuunganisha nyaya hizo na kutengeneza 'bridge' ya umeme (alikuwa anafanya reroute) naamini watu wa umeme na fizikia watelewa vizuri..
Kwahiyo baada ya kufanya hii reroute ilimaanisha kwamba umeme uliokuwa unatoka kwenye alarm system unaishia hapo kwenye 'bridge' na kurudi nyuma na umeme uliokuwa unatoka kwenye vifaa vya ulinzi ulikuwa hauvuki hiyo bridge!! Kwa kifupi ni kwamba mawasiliano kati ya alarm system na vifaa vya ulinzi yalikuwa hayapo hivyo haikujalisha nini kilikuwa kinatokea ndani ya vault, alarm system isingeweza kudetect..

Baada ya hapo wote wakaingia ndani na kuanza kazi ya kufungua visanduku vidogo vilivyopo ukutani vilivyokuwa na almasi.. Walitumia drill ambayo ilitengenezwa na The king of keys nyumbani.! Kwa kila kisanduku walitumia kama dakika tatu kukidrill mpaka kufunguka hivyo mpaka mida ya saa kumi na moja alfajiri walifanikiwa kufungua visanduku 109 kati ya 120 vilivyopo ndani ya ile vault.. Ili kuogopwa kukutwa na watu maana kitongoji cha Antwerp kuanzia majira ya saa kumi na mbili na nusu mitaa inaanza kufurika watu! Kwahiyo wakajiridhisha kuwa wana mali ya kutosha wakabeba mzigo wao wakatokomea..



#3

WIKI CHACHE BAADE..

Natarbatolo alikamatwa wiki chache baadae kwa kuhusika na tukio hili!
Kukamatwa kwake kulikuwa ni kwa kizembe mno, walitupa taka taka za vifaa vyao vya maandalizi nje kidogo ya mji wa Antwerp na walipuuzia kuzichoma moto wakiamini hakuna mtu atakayeziona.. Katika takataka hizo pia kulikwa na kipande cha Sandwich ambacho Natarbartolo alikibakisha alipokuwa anakula.. Polisi walitumia kipande hicho cha sandwich kupima DNA na kukuta inamatch na DNA ya Natarbartlo..


MAMBO YENYE UTATA MPAKA LEO HII

Kuna vitu kadhaa ambavyo mpaka leo havitapata majibu sahihi..

i) yule myahudi aliyempa dili Notarbartolo ni nani?? Kuna watu wanadai kuwa Natarbartolo anajificha identity ya huyu mtu kwasababu inawezekana ni mpwa wake Benedetto Capizzi ambaye mwaka 2003 aliteuliwa kuwa Capo dei capi, ambacho ni cheo cha juu kabisa katika mtandao wa kihalifu wa Sicilian Mafia..
Natarbartolo anakataa kabisa mpwa wake kuhusika katika tukio hili..

ii) Natarbartolo anadai kuwa wao wenyewe waliingizwa mkenge na yule myahudi kwasababu anahisi kuwa yule myahudi na wenzake walitengeneza insurance scum ili waweze kujipatia fedha kutoka kwenye kampuni ya Bima.
Yaani iko hivi, polisi wanadai kuwa almasi iliyoibiwa zilikuwa na thamani ya dola milioni 100 lakini Natarbartolo anadai kuwa viboksi vingi wakivyovifungua ndani vault vilikuwa havuna kitu kana kwamba watu waliambiws wasiweke alamsi siku hiyo.. Natarbartolo anadai kuwa almasi walizozikuta zilikuwa na thamani isiyozidi dola milioni 20.!! Natarbatolo anahisi kuwa yule myahudi alipanga dili na wenzake wamshawishi aende akaibe lakini siku moja kabla yule myahudi na wenzake wengi wakatoa almasi kwenye vault, kwahiyo baada ya tukio lile la wizi watu wote wenye visanduku kwenye vault wataenda kulipwa na kampuni ya bima lakini huku almasi zao zikiwa ziko nyumbani wamezificha kwani walizitoa siku moja kabla ya tukio! Kwahiyo wanakuwa wamepata hela ya bima na almasi zao wanazo..

iii) Hizi almasi zilizoibiwa hazijapatikana mpaka leo, na hazijulikani ziko wapi licha ya Natarbattolo kukamatwa..


MWISHO...

Natarbartolo alikamatwa na kushtakiwa kwa wizi huu uliotokea! Kutokana na kukosekana ushahidi wa moja kwa moja (almasi zenyewe) ikabidi mahakama itumie ushahidi wa kimazingira (circumstantial evidence) ili kumtia hatiahani na alihukumiwa miaka kumi jela.. Mpaka hivi tunavyoongea Natarbartolo ameshamaliza kutumikia adhabu yake na yuko uraiani na ameingia mkataba na Paramount Pictures ili kutengeneza filamu kuhusu tukio hili na filamu itatengenezwa na Director nguli J. J. Abrams huyu ndiye aliyetengeneza filamu za Lost (series), Armageddon, Star Trek, Star Wars: Force Awaken pamoja na filamu ya Mission Impossible III

Tuesday, 26 July 2016

Jinsi Ya Kupanga Na Kupangua Ubongo Ili Kutimiza Ndoto (Hypnosis


:HYPNOSIS:

Habari Zenu Wanabodi Naileta Kwenu Mada Yangu Mpya Kuzidi Kuelimisha Kuwa Binaadamu

Yaani WeweNi Zaidi Ya Unavyojijua… Pia Ni Muendelezo Wa Mada Za "Rakims" Brain Power

Leo NaanzaNa Hii Ya Ku Hypnosis Yaani Pangua Panga Ya Ubongo Mchafu Kuwa Msafi Na

Wenye Kupinda Pinda Kukaa Sawa…...............

Kwa Kuanza Hypnosis Ni Rejea Inayohusu Au Inayohusiana Na Kudatisha Na Kuvuta Maono Kwa Hali Ya Juu Zaidi Ambayo Mara Nyingi Hutumika Kwa Kifaa Au Picha Inayoji rudia Rudia Mfano:

Bounce Watch Au Picha Iliyoganda Mfano Wa Animation Lakini Inafanyisha Movement Na Ubongo Wako Mwenyewe Kabla Ya Kuiongelea Mengi Kwanza Tuone Zipi Faida Zake….



FAIDA ZA HYPNOSIS:

1:Inamsaidia Muhusika Kufikia Kutamani Yale Asiyoweza Kuyafanya Na Akayafanya Na Akafanikiwa Vema Zaidi Ya Vile Alivyotegemea…..

2:Inamsaidia Muhusika Kuweza Kuondokwa Na Msongo Wa Mawazo,Wasiwasi Na Maumivu

3:KupunguzaMaumivu: Husaidia Kuondoa Maumivu Ya Kansa, Kufungua Njia Za Haja Kubwa NaMaungio Yake, Hupoza Maungio (Joints) Na Maumivu Yoyote Ya Kichwa Hupozwa Na Hypnosis

4: Kuondoa Majoto Mwilini: Husaidia Kuondoa Homa Za Sitambui Kama Kuhisi Baridi Kwenye Joto Joto Kwenye Baridi Au Kutaka Joto KWenye Baridi Na baridi Kwenye Joto..

5: Husaidia Kubadili TABIA: Kikojozi,Mlevi,WavutaSigara,Mwenye Kukosa Usingizi,Uoga,Wizi

Uasherati,uzinzi,upagani,uchawi…..Husaidia Kuacha Yote Hayo Na Kuwa Mtu Mwengine Na Tofauti Alivyokuwa Mwanzo..

Hypnotism puts you into a state of “focused concentration,” during which you’re vaguely aware of your surroundings — you just don’t care about them. There are different stages of hypnosis, some deeper than others. But when you’re in any of them, your imagination is open to suggestion.

The suggestions made to you while you’re hypnotized are part of hypnotherapy. This term, sometimes used interchangeably with hypnotism, simply describes the stuff that is suggested to you while you’re hypnotized to help make you better after the session is over. Often the suggestions are images — picturing your arm going numb, picturing yourself relaxed — rather than orders to “stop hurting.”



Good candidates for hypnosis

If you’re trying to lose weight, stop smoking, control substanceabuse, or overcome a phobia, hypnosis may be worth a try. And if you’re unhappywith your current treatment for warts or other skin conditions, asthma, nausea,irritable bowel syndrome, fibromyalgia, migraines, or other forms of pain,discuss the possibility of hypnotherapy with your M.D.

Hypnosis can work for almost anyone, though some people have aneasier time than others. If you’re lucky, you’ll be one of the few people(about 5 to 10 percent of the population) who is highly susceptible to hypnoticsuggestion.

Some of these folks reputedly can be hypnotized (with no otheranesthesia) before surgery and feel no pain. But even if you’re not in thisgroup, chances are high that hypnosis can help you: About 60 to 79 percent ofpeople are moderately susceptible, and the remaining 25 to 30 percent areminimally susceptible.


Children and young adults are often good candidates forhypnosis, perhaps because they’re so open to suggestion and have activeimaginations.

If you don’t trust your therapist, or don’t believe thathypnotism can work for you, it probably won’t. Hypnotism can only work ifyou’re willing for it to work and you have a clear idea about what you want itto do for you.

HATARI ZAKE:
Kama Tunavyojua Hakuna Chenye Faida Kisipo Na KIkwazo Hii Pia Ipo Japo hatari Zake Ni Nadra Lakini Yaweza Kukutokea Haya:

1: Kuumwa Kichwa
2:Kusinzia
3:Kizunguzungu
4:Wasiwasi au Tabu
5:Kutengeneza Kumbukumbu Ya Uongo

Pia Hii Haitakikani Kufanywa Kwa Watu Ambao Hawako Sawa Kiakiri Yaani Wagonjwa Wa Akili Hadi Ruhusa Itolewe Na Wazazi Au Wanaomlea Mtu Huyo Ndio Afanyiwe Katika Kurejesha AkiliYake Ni Hatari Kwao Kwa Maana Pale Alipo Tayari Kama Yupo On Hypnosis Mode Sawa Na Moto Kuzimia Petrol Atakuwa Kichaa Times Two

Lakini Pia Katika Kupoteza Kumbukumbu Waweza Kuingiza Kumbukumbu Ya Maisha Ambayo Hayakuhusu Kwenye Ubongo Wako Yani Unakuwa Unakumbuka Uliwahi Kufanya Kitu Fulani Lakini Hukufanya….
Hizo Ndio Hatari Za Hypnosis…

Jinsi YaKufanya Hypnosis:
Kuna Aina Mbili Za Kufanya Hypnosis Ambazo Ni:
1: Kufanya Mwenyewe
2:Kufanyishwa Na Hypothelapist/kumfanyia Mwenzio

Hapa Nitaielezea YA Kufanya Mwenyewe Kwa Uchache:

JINSI YAKUFANYA HPNOSIS MWENYEWE Bila MADHARA:
Huhitaji Kujiandaa Vyovyote Kama Unaenda KUfanya Hypnosis Labda tu kuvaa Nguo Zitakazo Kuweka Comfortable Na Kukufanya Ujihisi Relaxed..


SASA FUATAHATUA KWA HATUA:

Hatua Ya Kwanza:
Utulivu Unahitajika Kama Vile Unavyofanya Meditation..

Hatua Ya Kwanza Ni Kutuliza Mwili.. Kaa Kwenye Mkao Wowote, na jaribu kukwepa movement zozote zisizohitajika kwenye mwili wako.. jaribu kudhania kwamba kila sehemu ya mwili wako imetulia kutokea kwenye nywele roots, macho, pua, mdomo,lips za mdomo,shingo halafu unahamia kwenye mkono wa kulia,unaenda kushoto, halafu kifuani muscles za tumbo mpaka mguu wa kulia mguu wa kushoto anza na paja la kulia kisha la kushoto ndio mguu halafu kwa njia hii unakuwa umetulizanisha muscles za mwili mzima………..

2: Hatua YaPili… Ni Hatua YA Kujituliza Kiakili Kwanza, Unatakiwa Ujiweke KAtika Hali Ya MAwazo Mengi Mawazo Mengi Na Hofu Uitandaze Katika Fikra YAko.. Sasa Baada Ya HApo Unatakiwa Uanze Kusafisha Mawazo Na Hofu Zote Kutoka Katika fikra YAko Kuna Njia Nyingi Za Kuondoa LAkini Hapa NAkupa Hii Moja RAhisi……

Unaweza Weka Bakuli Uliojaza MAji Mbele YAko NA Kuanza Kubeba Hofu Na Mawazo Yote
(Elimu,Kazi,Mambo YA Familia N.k) Na Kuyatumbukiza Moja Baada Ya Jingine KatikaNjia Hii Sooner Or Later Fikra Yako Itaingia Katika Fikra Ya Pili Ya Kufikiri (Fikra Tupu Ya Kufikiri)

Ambayo Ni Bila Hofu Wala Woga Yani You Go Complete IntoUnconscious state mara zote kumbuka kuomba fikra yako mwanzo kwamba baada yamuda (Huu Muda Utaamua Mwenyewe) Kwamba Utaamka Katika Hii Hali Ya Unconscious Mind Mfano Nitakaa Humo Kwa Dk 15 au 20 baada ya hapo niamke kwenye (hypnosis sleep)

Pindi Tu Utakapofikia hii sehemu unatakiwa uwe kwenye hali ya amani Sasa Waweza Ianza Sehemu Ya Self Hypnosis Kama Ifuatavyo….

3: Hatua YaTATU:

Weka Mkono Wako Mbele Yako Sasa Jiambie Kwamba Mkono Wangu Upate Mwanga Na Mwanga YAseme Maneno Haya Hadi Yafike Kwenye Ubongo Au Fikra Yako Hadi Pale Utakapoona Mkono wako Umeanza Kuwaka Taa/Mwanga Na Unaanza Kuelea Hewani Mbele Yako NaKusababisha Mng'ao hata kama upo gizani Hutaamini Yani…

4:utakapofikia hiyo sehemu sasa sema tena mkono wangu uwe mzito zaidi na zaidiili uweze kushuka Chini? Ukiweza na hivyo sasa unaweza kuanza kuamrisha zingine ngumu wewe tu sasa na maamuzi yako lakini kumbuka muda uliojitegea kama ni alarm kama ni kukadiria ukifika tu muda huo unatoka automatically kwenye hiyo hali…

5: Sasa Jiambie NI Wakati wa Kutoka Kwenye Hali Hii Basi Utajikuta Umeshatoka Tayari..

Kumbuka Mara Zote Kwamba Fikra kwa muda huo inapokea chochote ambacho unasema hata kama utataka ikuonyeshe tukio lililopita uliosahau utalikumbuka mwanzo hadi mwishohuta poteza hata sekunde sasa kuwa makini na ufanye salama.. Katika Hili Wakuu Hata Kama Ulikuw a Huamini Mwenyezi Mungu Yupo Utaamini Hata Kama Ukijiaminisha Shetani Hata Kuweza Kamwe Hata Kuweza.. Hata Ukisema Kuanzia Leo Mimi Tabia Zangu Mbaya Naacha Utaacha,

Hata kama Ukisema Kuanzia Leo Mimi Mlokole Utaokoka Hata Kama Ukisema Kuanzia Leo Mimi Ni Muumin Yani Muislamu Dhati Basi Utakuwa Hii Ni PSYCHOLOGY Haina Utani Hapo.. If You Want To Do Something Do It Now………………. Because NO Body Knows Tomorrow ChangeNi Rakims Ni Wewe Ni Sisi.

Note:usijilazimishe kufanya ambacho ni kinyume na asili au mpaka wa dini yako wewetumia tu kujiponya na wenzio hofu na woga misongo ya mawazo na uhaba wa maisha ili kufanya watu waishi kwa amani duniani.....

Lakini Kama Hujafaulu Kufanya Hili NIpo Hapa Niambie Umefanyaje Hujafikia Usivunjike Moyo Twende Taratibu Utafika TU Na Jitahidi Usiweke Machaguo Magumu Ambayo Yatakuletea Vikwazo Na Kutoka Kwenye Hali Hii Kabla Hujafikia Lolote Anza Taratibu Tu And Practice Make Perfect…………

Monday, 25 July 2016

Fahamu historia ya Alexander Alexandrovich Prokhorenko shujaa kijana wa urusi wa mwaka 2016 katika mapigano ya Syria



Alexander Alexandrovich Prokhorenko ni kijana mdogo aliyekuwa Komandoo katika Kikosi cha Kazi Maalum cha Jeshi la Urusi kiitwacho SPETSNAZ akiwa na cheo cha Luteni Mwandamizi (Senior Lieutenant). Alizaliwa tarehe 22 Juni 1990 katika kijiji cha Gorodki, Orenburg Oblast, nchini Urusi au Russia. Alihitimu masomo yake katika Skuli ya Uhandisi ya Ulinzi wa Makombora ya Ndege na katika Chuo cha Ulinzi wa Anga cha Smolensk nchini Urusi. Ndo kwanza alikuwa ameoa na mkewe alikuwa ndo kwanza anatarajiwa kujifungua muda si mrefu.



Alexander Alexandrovich Prokhorenko alikuwa miongoni mwa Makomandoo wa Kikosi cha Spetsnaz waliopelekwa nchini Syria kuisadia serikali ya Rais Bashar Al Assad katika mapigano dhidi ya kundi la ISIS. Alikuwa ni miongozi wa wanajeshi waliopelekwa kuuhami mji wa kihistoria wa Palmyira dhidi ya kundi hilo la ISIS.

Siku ya tarehe 17 Machi, 2016, kijana huyu akiwa katika jukumu lake zito la kukusanya taarifa muhimu za kijeshi zilizolenga kuwabaini wapiganaji wa ISIS mahali walipo na silaha zao na kisha kuzituma taarifa hizo kwa marubani wa ndege za kivita wa Urusi kwa ajili ya kuendesha mashambulizi ya anga yenye kupiga malengo vizuri, alijikuta amezingirwa na wapiganaji katili wa kundi la ISIS baada ya kumng'amua. Kama ilivyo mila na desturi kwa askari aliyefunzwa vyema na akafunzika, hasa komandoo, ni haramu na aibu kubwa kwa askari kuangukia mikononi mwa adui yake akiwa hai kwani anampa adui faida ya kumfanya atakavyo na kumsaidia kupata taarifa za jeshi lake iwapo atazidiwa na mateso atakayopewa na adui yake huyo.

Kwa kulielewa vyema hilo, Alexander Prokhorenko, baada ya kubaini kwamba alikuwa katikati ya wapiganaji wa kundi la ISIS na hakuwa na namna nyingine ya kufanya, aliamuru ashambuliwe kwa kombora na jeshi lake la anga na jeshi lilifanya hivyo mara moja na yeye kupoteza maisha akiwa kazini.



Kwa kushirikiana na vikosi vya Kikurd, jeshi la Urusi liliweza kuupata mwili wake na kuusafirisha kwenda Urusi ambapo uliwasili Moscow tarehe 29 Aprili, 2016. Mazishi yenye heshima zote yalifanyika nyumbani kwao katika kijiji cha Gorodki tarehe 6 Mei 2016. Tarehe 11 Aprili, 2016, Rais Vladimir Putin alimtangaza Alexander Prokhorenko kuwa Shujaa wa Shirikisho la Urusi, ambayo ni Heshima ya Juu zaidi nchini humo.



Huyu ndiye Alexander Alexandrovich Prokhorenko, ameacha mke mjazito. Pumzika kwa Amani Shujaa Kijana!!

Sunday, 24 July 2016

Kauli ya CHADEMA baada ya wanachama wake kutangaza kujiunga CCM



Wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM jana mjini Dodoma, Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kiliwapoteza wanachama wake watatu baada ya kutangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wanachama hao waliokihama chama hicho ni Fred Mpendazoe ambaye alikuwa mwanachama wa CCM pia aliwahi kuwa Mbunge wa Kishapu mwaka 2005 hadi 2010 kupitia CCM, Mgana Msindai aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na mbunge wa zamani wa Iramba Mashariki na mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA alipohojiwa jana wakati kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kinaendelea alisema kuwa, hawana muda wa kukaa na kuanza kumjadili mtu mmoja mmoja anayesemekana kuhama chama hicho.

"Kamati Kuu ni kikao kizito sana, hatuwezi kuacha kujadili masuala ya msingi na kuanza kuwajadili hao wanaosemekana kuwa wamehama chama," alisema mjumbe huyo.

Kamati Kuu ya CHADEMA imekutana jana na leo katika vikao vya dharura ikiwa na lengo kubwa la kujadili mwenendo wa hali ya kisiasa nchini.