May 6, 2012 ilikua ni tarehe ya madiliko makubwa katika klabu hizi mbili kongwe hapa Tanzania. Hii ndio tarehe ambayo Simba iliifunga Yanga mabao matano kwa sifuri, kipigo kilichochangiwa na Mgogoro wa Yanga kwa wakati huo pia.
Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo mashabiki wa Simba walikua na furaha kubwa, wakati ilikuwa kinyume kwa mashabiki wa Dar-es-salaam Young Africans ambao waliondoka na huzuni.
Ni takriban miaka miwili tangu mechi hiyo ilipochezwa, hii leo mambo yamekuwa tofauti, ambapo Yanga wanaendelea kutawala ligi kuu wakati Simba imekua ikijaribu kuziba nafasi liyoachwa kati yake na mtani wake wa jadi.
Na hizi ni tofauti 4 kubwa ambazo kati ya Simba na Yanga kwa sasa.
1. UONGOZI
Baada ya kufungwa kwa mabao 5-0,Yanga walibadilisha uongozi kutoka kwa Loyd Nchunga na kwenda kwa Yusuph Manji,ni wazi kwamba tokea Manji aingie madarakani Yanga imekua imara kufuatia uongozi huo kushikamana kwenye kila jambo ili kuhakikisha klabu inaenda mbele kwenye nyakati zote,bila kutengeneza makundi hata kwenye nyakati ngumu.
Katika kuhakikisha klabu hiyo inasonga mbele kwa mafanikio makubwa,hivi karibuni Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji alikemea kitendo cha wazee kuzungumza maswala yanayohusu klabu kwa waandishi wa habari kwa kuwa yupo mtu maalum wa kuzungumzia mambo hayo,Kitendo ambacho kilikuwa kikijitokeza pia kabla ya Uongozi wa Manji bila kukemewa.
Wakati upande wa simba viongozi wanamakundi na haijulikani nani mwenye uamuzi wa mwisho katika klabu,kitendio kilichopelekea timu hiyo kuonekana kuwa na mgawanyiko kiasi jambo ambalo linaloaathiri hadi wachezaji kwenye ligi kuu Tanzania Bara.
2. VIKOSI
Ukilingisha vikosi vilivyocheza katika mchezo wa 5-0 na hivi vya sasa ni rahisi kuona kwanini simba ipo nyuma zaidi ya Dar –es-salaam Young Africans,ambayo kwa sasa ina kikosi imara kinachofahamu vyema nini cha kufanya uwanjani,huku wachezaji wa hakiba wenye uwezo pia.
“Star players” wa yanga : okwi, yondani, ngassa, niyonzima,kiiza, kavumbagu,domayo,dida,Msuva
Ukiangalia upande wa simba, wachezaji ambao walicheza katika mchezo wa 5 – 0, wengi wao hawapo simba. Ukiachia Merehemu General Patrick Mafisango, wachezaji watatu waliokua muhimu kwenye mechi hiyo wote wapo jangwani, “ okwi,yondani na kaseja”.
“Star Players” Singano na Tambwe
NB: star player ni mchezaji ambae ana uwezo wa kubadilisha matokeo ya mchezo either kwa kudominate mchezo au kufunga mabao.
3. DAR ES SALAAM DERBY
Hii ni mechi ambayo kwa kipindi cha karibuni yanga imekua ikifungwa na simba. Kuna mambo mengi yanayosababisha yanga kufungwa ila kwa mtazamo wangu kitu kikubwa kinachosababisha matokeo mabaya kwa yanga ni
Pressure Ya Mechi
Ni kitu ambacho kinaweza kukufanya ushinde au ushindwe kwenye mechi. Hii ndio mechi kubwa Tanzania ambayo inakuja na pressure nyingi kutoka kwa mashabiki. Kwa miaka ya karibuni yanga uingia kwenye hii mechi akiwa katika form nzuri kitu kinachowafanya wawe relaxed na wasijiandae vyema. Wanaichukulia hii mechi kama ya kawaida, ni kitu kizuri ila ni ukweli kwamba hii mechi sio ya kawaida.
Wanakutana na simba ambayo inapania kushinda hii mechi na kuipa uzito mkubwa sana. Hii inatokana na pressure kubwa kutoka kwa mashabiki. Wanatumia resources zote walizokua na nazo ili mradi washinde, hii ni kwasababu kwa miaka ya karibuni ushindi katika mechi ya watani ndio kitu peke ambacho simba inaweza kujivunia.
Viongozi na wachezaji wa yanga inabidi wabadilike, mechi hii bado ina umuhimu sana hasa kwa mashabiki. Ila kuna baadhi ya mashabiki ambao wameshaanza kuona mechi kati yanga na Azam ndio kubwa kuliko na simba.
4. USAJILI
Hapa ndipo kwenye utofauti mkubwa,
a) Uongozi wa Yanga unasera ya kusajili wachezaji bora tuu, watu wengi wanasema yanga inaua vipaji, mimi sioni kwa mtazamo huo,Timu nyingi kubwa duniani zinazotawala ligi zao kama Bayern Munich,Chelsea,Celtics ya Scotland,Barcelona,Juventus na nyinginezo zinafalsafa kama ya yanga
b) Kua na Ushindani kwenye kikosi, yanga ina wastani wa wachezaji wawili katika kila namba, kitendo kinachomsaidia mwalimu kua na chaguo kubwa na bora la wachezaji huku wachezaji wenyewe kutobweteka pia ili kupata namba kwenye kikosi cha kwanza.
c) Kwa upande wa simba usajili wao wa safari hii umekuwa kama wakujaza wachezaji tuu kwa kiasi Fulani,kwenye Dirisha dogo wamewasajili magolikipa wawili,Huku nafasi kama beki wa kushoto ikiwa ni tatizo,kitu ambacho kinamfanya mwalimu amchezeshe henry joseph kwenye nafasi hiyo,Simba imekubali dirisha dogo kupita bila kusajili mshambuliaji,wakionekana kuridhika na washambuliaji waliowapa matokeo kwenye mechi ya mtani Jembe akiwemo Tambwe.
Hata ni mawazo Yangu,si msimamo wa kituo,na wewe unaruhusiwa kua na yako