Wednesday, 17 April 2013
Watanzania tujifunze kusoma vitabu mbalimbali
Ndugu zangu watanzania,hivi sasa tunakabiliwa na changamoto nyingi sana ambazo mi nadhani tunahitaji kupata suluhisho lake.Lakini kupata suluhisho ni jambo gumu sana hasa ukizingatia tunakabiliwa na tatizo la uchambuzi na upembuzi wa mambo kutokana na ukosefu wa elimu ya kutosha kwa watanzania walio wengi.
Lakini watu wengi wanadhani kuwa na elumu ni lazma ufike chuo kikuu, sio kweli,unaweza kufika chuo kikuu lakini bado ukawa hujaelimika.
Sasa kutokana na tatizo hili nimeona katika blog hii nianze kuweka vitabu mbalimbali kmf;vya siasa,uchumi na vya kijamii ili kwa mwenye uwezo aweze kuvisoma ili akuze uelewa wake.
Hivyo nawasihi ndugu zangu mtembelee blog hii ili muweze kuelimika.

Sunday, 14 April 2013
HOTUBA YA MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA UFUNGUZI RASMI WA JENGO LA KITIVO CHA SAYANSI KATIKA CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO (MUM), TAREHE 14 MACHI, 2013, MOROGORO
Mzee Kitwana Suleiman Kondo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF);
Mheshimiwa Joel Bendera, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro;
Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro;
Profesa Hamza Mustafa Njozi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro;
Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na Jumuiya mliohudhuria;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Niruhusuni niungane na wenzangu walionitangulia kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa. Nakushukuru sana Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro na viongozi wenzako kwa kunialika kuja kujumuika nanyi katika siku hii adhimu ya ufunguzi wa jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro. Mmenipa heshima kubwa ya kuwa sehemu ya historia ya Chuo hiki. Kwa kweli, nimefarijika sana kuona Chuo chetu kinazidi kupata mafanikio ya kutia moyo hasa ukizingatia ukweli kwamba kina muda mfupi tu tangu kuanzishwa kwake.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Natoa pongezi nyingi kwako, Makamu Mkuu wa Chuo na wale wote walioshiriki kubuni wazo la kuwa na jengo la Kitivo cha Sayansi na kufanikisha ujenzi wake. Juhudi zao na moyo wao wa kupenda maendeleo ndio umetufanya sisi kujumuika hapa leo kushuhudia mafanikio haya. Hakika ni jambo la kujivunia. Pia, nawapongeza sana Wajenzi na Mhandisi Mshauri kwa kazi nzuri waliyofanya ya ujenzi wa jengo hili. Sote tunaliona jengo lilivyojengwa vizuri na kwa namna yake linapendezesha mandhari ya Chuo.
Kwa namna ya pekee napenda kwa niaba yenu nitoe shukrani zangu za moyoni kwa taasisi ya Al-Barakah kwa kufadhili ujenzi wa jengo hili. Asanteni sana kwa ukarimu wenu na upendo mkubwa mliouonesha kwa nchi yetu na watu wake. Naomba taasisi nyingine na watu binafsi waige mfano huu mzuri wa kusaidia miradi mbalimbali inayonufaisha jamii. Tukumbuke ule msemo wa wahenga kuwa “kutoa ni moyo, usambe si utajiri”.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Mabibi na Mabwana;
Kwa miaka mingi madhehebu ya dini na mashirika ya dini yamekuwa washirika muhimu sana wa Serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Yamekuwa yanajihusisha na kutoa huduma kwa jamii kama vile afya, elimu na nyinginezo. Kwa ajili hiyo watu wengi sana nchini wamenufaika na wanaendelea kunufaika na huduma zinazotolewa na mashirika ya dini.
Kwa miaka mingi mashirika na taasisi za madhehebu ya dini ya Kikristo ndiyo yaliyokuwa yakionekana kutoa huduma hizo. Kwa upande wa Waislamu, ukiacha Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan, mchango umekuwa mdogo sana. Ni jambo la faraja kubwa kuona Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF) ikionyesha njia. Kwa kumiliki na kuendesha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kwa ufanisi, MDF inatoa mchango muhimu katika kuendeleza elimu ya juu na maendeleo nchini. Idadi kubwa ya wanafunzi waliofuzu masomo yao na waliopo katika Chuo hiki tangu kilipoanzishwa mwaka 2005 ni ushahidi tosha wa kazi nzuri inayofanywa na MDF. Hongereni sana. Tunawaombea kwa Mola mpate mafanikio makubwa zaidi miaka ya usoni kwa upande wa elimu na huduma nyingine muhimu.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Katika kipindi cha miaka saba sasa, Serikali yetu imeongeza sana uwekezaji katika upanuzi wa elimu tangu ya awali hadi elimu ya juu. Tumeamua kufanya hivyo kwa sababu vijana wengi waliokuwa wanastahili kupata elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu walikuwa hawapati. Tanzania ni kubwa kuliko Kenya na Uganda kwa eneo na idadi ya watu lakini ndiyo tuliokuwa na idadi ndogo ya wanafunzi kwa ngazi zote hizo. Kwa mfano, mwaka 2005 idadi ya wanafunzi waliokuwa Chuo Kikuu nchini Kenya ilikuwa108,407, Uganda 88,360 na kwa baadhi ya nchi za SADC kama vile Afrika Kusini idadi hiyo ilikuwa 717,973. Wakati wenzetu wakiwa na idadi hiyo, sisi tulikuwa na wanafunzi 40,719 tu katika vyuo vikuu nchini. Hali ilikuwa hivyo pia kwa elimu ya sekondari. Kenya ilikuwa na wanafunzi 925,341, Uganda 619,519 na Afrika Kusini 4,186,882 wakati Tanzania ilikuwa na wanafunzi 524,325 tu waliokuwa katika shule za sekondari.
Tuliona hali hii haikubaliki hivyo tukaamua hatuwezi kuiacha iendelee. Tukaamua kudhibiti. Tukachukua hatua tulizochukua za kupanua elimu katika ngazi zote. Matokeo ya uamuzi huo ni kwamba vijana wanaopata fursa ya kupata elimu katika ngazi zote wamekuwa wengi kuliko wakati mwingine wo wote katika historia ya nchi yetu, tumewafikia na kuwapita majirani zetu. Kazi kubwa tunayoendelea nayo sasa ni kuwekeza katika kuimarisha ubora wa elimu waipatayo vijana wetu kwa kuongeza walimu, vifaa vya kufundishia, vitabu na huduma nyinginezo. Inshallah hata kwa dhamira yetu, hii njema Mola atatuwezesha. Mwanzo mgumu lakini hatma itakuwa nzuri.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Kufuatia juhudi hizo, idadi ya wanafunzi waliopo kwenye vyuo vikuu nchini imeongezeka sana, kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 166,484 mwaka 2012. Kwa upande wa sekondari mwaka 2011 tulikuwa na wanafunzi milioni 1.79 na wenzetu wa Kenya walikuwa na wanafunzi milioni 1.77. Haya ni mafanikio makubwa.
Serikali itaendelea kuwekeza kwenye upanuzi wa fursa za elimu na ubora wake. Hata hivyo ushiriki wa wadau wengine kuunga mkono juhudi za serikali ni jambo muhimu sana. Tumeweka mazingira mazuri kwa wadau hao kufanya hivyo na mafanikio yanaonekana wazi. Kama nilivyokwishasema awali, mashirika ya dini yamekuwa wadau wa kutumainiwa na mchango wao uko wazi. Unajieleza wenyewe. Kwa mfano, katika vyuo vikuu 49 vilivyopo nchini, vinavyomilikiwa na umma ni 14 tu. Vyuo vikuu 24 vinamilikiwa na mashirika ya dini na 11 na sekta binafsi.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa na muhimu unaotolewa na vyuo vikuu vinavyomilikiwa na mashirika ya dini na sekta binafsi. Ninyi mmekuwa washirika wazuri na wa uhakika katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya elimu katika nchi yetu. Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono na kushirikiana nanyi ili kuwawezesha vijana na Watanzania wengi zaidi waweze kupata elimu. Uamuzi wa kufanya utaratibu wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu uhusishe wanafunzi wa vyuo visivyokuwa vya umma ni moja ya mambo mengi muhimu yanayofanywa na Serikali kuthibitisha usemi wangu huo.
Tulipoingia madarakani mwaka 2005 tulifanya mambo mawili muhimu kuhusu mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Kwanza uamuzi kwamba, mikopo itolewe kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma na vile visivyokuwa vya serikali. Kabla ya hapo ilihusu vyuo vya umma pekee. Pili kwamba, kila mwaka tuongeze fedha zinazotengwa kwa ajili ya Mfuko huo ili idadi ya wanafunzi wanaonufaika iongezeke. Tulikuta Mfuko ukiwa na shillingi billioni 56.1 unanufaisha wanafunzi 16,345 mwaka 2005. Tukaongeza kila mwaka na katika mwaka huu wa fedha (2012/13) tumetenga shillingi bilioni 345 zinazowanufaisha wanafunzi 98,772.
Tutaendelea kuongeza fedha katika Mfuko huo ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike na hata ifikie siku moja tuweze kuwakopesha wote bila ya kujali sifa ya uwezo wa wazazi au walezi kulipa ada. Kwa kasi tuliyonayo na kwa jinsi tunavyozidi kufanikiwa katika kukusanya mapato ya serikali, naamini miaka michache ijayo tunaweza kufikia lengo hilo. Nawasihi Bodi ya Mikopo iwekeze katika kuimarisha uwezo wa kuwafuatilia waliokopeshwa kulipa mikopo waliyopewa. Matamanio yangu ni kuwa fedha zilizotolewa zizunguke ili tupunguze kiasi kinachotolewa na bajeti ya serikali kila mwaka.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Mabibi na Mabwana;
Niruhusuni nitumie nafasi hii kukupongeza wewe Mkuu wa Chuo, Makamu Mkuu wa Chuo, Wahadhiri na Jumuiya nzima ya Chuo Kikuu hiki kwa kazi kubwa na nzuri muifanyayo ya kuendeleza na kuboresha Chuo. Tumeshuhudia ujenzi wa jengo nililolifungua leo. Tumeona mafanikio kwa upande wa ongezeko la idadi ya wanafunzi, walimu, wafanyakazi na fani zinazofundishwa katika kipindi hiki kifupi cha uhai wa Chuo hiki.
Nimefurahishwa na kufarijika sana kusikia kuwa ubora wa elimu inayotolewa hapa chuoni ni jambo linalopewa kipaumbele cha kwanza. Jambo hili ni muhimu sana kulisisitiza kwani tunataka wahitimu wa Chuo hiki wafanane na wahitimu wa Chuo chochote kizuri nchini na hata duniani. Ningependa kuona wahitimu wa Chuo hiki wanagombewa katika soko la ajira. Hili ni jambo linalowezekana. Kinachotakiwa ni uamuzi wa Baraza na Seneti kuwa iwe hivyo na kuchukua hatua zipasazo. Sina shaka kuwa mnaweza kufanya hivyo. Hakika mnaweza, na sote kwa umoja wetu tunaweza.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Nimefurahi sana, pia, kusikia kuwa Chuo kinatoa mafunzo ya ualimu. Bila ya shaka mnaelewa kwa nini nafurahi. Tuna uhaba mkubwa wa walimu nchini hivyo Chuo cho chote kinachotoa mafunzo ya ualimu hunifurahisha. Endeleeni kuimarisha mafunzo hayo ili Chuo chenu kitambulike na kukubalika nchini kwa sifa ya kutoa walimu wazuri. Walimu wa kutoka Chuo hiki wawe wale wanaojua vyema masomo wanayofundisha, mahiri kufundisha na waadilifu. Naomba pia mtoe kipaumbele cha juu kwa mafunzo ya ualimu wa masomo ya sayansi na hisabati. Mkifanya hivyo, mtakuwa mnatoa mchango mkubwa katika jitihada za kupunguza uhaba wa walimu wa masomo hayo nchini. Naamini kitendo cha kuzindua Jengo la Kitivo cha Sayansi, kilichofanyika muda mfupi uliopita kinatoa matumaini ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kuchangia katika jitihada za kupunguza pengo la walimu wa sayansi nchini.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Nimewasikia mkieleza kwa ufasaha changamoto kubwa na ndogo ambazo Chuo inakabiliana nazo. Nawapongeza kwa dhati, wewe na viongozi wenzako kwa ubunifu wenu na hatua mnazochukua kuzikabili changamoto hizo. Nawaahidi msaada na ushirikiano wangu na wa serikali kwa yale yaliyoko kwenye uwezo wangu na wa serikali katika kutafuta ufumbuzi kwa changamoto zinazowakabili.
Nawapongeza kwa uamuzi wenu wa kutafuta vyuo vikuu rafiki vilivyoko katika nchi mbalimbali duniani mnavyoweza kushirikiana navyo. Endeleeni kufanya hivyo kwani vyuo vikuu vingi duniani hufanya hivyo. Hamtakuwa wa kwanza na wala hamtakuwa mnafanya jambo la kustaajabisha. Mnaweza, mkipenda, kuwaomba Mabalozi wetu waliopo katika nchi mbalimbali duniani wawasaidie. Ni wajibu wao kufanya hivyo kwani kusaidia kusukuma maendeleo ya hapa nchini kutoka huko waliko ndilo jukumu lao la msingi. Vile vile, nimefurahishwa na mipango yenu ya baadaye ya kuwa na matawi katika mikoa mbalimbali nchini. Hongereni kwa uamuzi wenu wa busara. Lazima Chuo kitanuke kwa maana ya kuwa kikubwa zaidi, makao makuu na kwa kuwa na vyuo vishiriki na shule au vitivo sehemu mbalimbali nchini.
Ndugu Mkuu wa Chuo;
Kazi iliyo mbele yenu ni kubwa, hivyo ni vyema kuweka mikakati mizuri na mipango thabiti ya utekelezaji na ufuatiliaji wa dhamira yenu hiyo njema. Rai yangu kwenu ni kuwaomba muwe wabunifu zaidi hasa katika kutafuta vyanzo vingine vya mapato vitakavyosaidia Chuo kujiendesha bila kutegemea ada peke yake. Chuo kiangalie uwezekano wa kufanya shughuli zitakazowaingizia mapato kama vile kufanya shughuli za kutoa ushauri. Pia muangalie uwezekano wa kuwekeza wenyewe kwenye miradi ya kiuchumi au kwa kushirikiana na wawekezaji katika baadhi ya maeneo.
Kuhusu nafasi mbili za ufadhili nilizopewa na Chuo kikuu cha Tun Abdul Razak cha Malaysia, nitafuatilia kujua kilichoendelea na kinachoendelea. Je, nafasi hizo bado zipo? Zikiwepo, nitawasiliana na wahusika waangalie uwezekano wa kuwapeni. Kama zimeshagawiwa basi tusubiri safari ijayo. Kwa masuala ya ardhi na maombi mengine nimeyasikia, yaleteni tuangalie namna ya kusaidiana.
Ndugu Makamu Mkuu wa Chuo, na
Wafanyakazi wote wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro;
Napenda kuwakumbusha kuwa mnayo dhamana kubwa na wajibu mkubwa na wa kihistoria. Ule ukweli kwamba ni mara ya kwanza kwa Taasisi ya Waislamu wazawa kuwa na Chuo Kikuu inawapeni wajibu maalum wa kuhakikisha Chuo kinafanikiwa. Ni mtihani na changamoto ya aina yake kuthibitisha kuwa Waislamu nao wanaweza kuwa na Chuo kizuri na chenye kutoa elimu ya ubora wa hali ya juu. Kwa sababu hiyo hamna budi kuhakikisha kuwa mna mipango mizuri ya kujenga Chuo cha hadhi na ubora wa hali ya juu. Ihakikishwe kuwa mipango hiyo inatekelezwa kwa ukamilifu.
Aidha jumuiya yote inao wajibu wa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, maarifa na weledi ili dhima hiyo ya Chuo iweze kutimizwa kwa ukamilifu. Timizeni wajibu wenu ipasavyo ili jina la Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro likue haraka. Sifa yake isambae na kuvuma kote nchini. Chuo kifanye vizuri ili wanafunzi waone fahari kuwa wahitimu wa Chuo hiki. Chuo ambacho, wazazi wapende kuleta vijana wao kuja kusoma hapa. Kwa jinsi Mkuu wa Chuo alivyoeleza, mimi nina imani mnaweza, fanyeni kweli.
Ndugu Wanafunzi wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro;
Naomba wote muone fahari ya kuwa wanafunzi katika Chuo cha kihistoria hapa nchini. Nawasihi mjitume kwa kadri ya uwezo na vipaji mlivyopewa na Mwenyezi Mungu mfanikishe kile kilichowaleta. Jifunzeni kwa bidii mfaulu vizuri ili mkihitimu muwe kielelezo kizuri cha mafanikio na ubora wa Chuo Kikuu Cha Waislamu cha Morogoro. Muwe Mabalozi na kioo cha ufanisi wa Chuo hiki. Nawasihi mjiepushe na mambo yatakayowapunguzia muda au kuwaondoa katika shughuli ya msingi iliyowaleta hapa ya kujifunza mpate digrii katika fani mliyochagua mwenyewe kuisomea. Vishawishi ni vingi na wapo watu wengi wanaopanga kuwashawishi mtumie muda wenu adhimu kufanya wanayoyataka wao ambayo mkishiriki huwatoa kwenye malengo na kutekeleza yao. Mambo ya dunia ya nje ya Chuo ni mengi huna budi kutambua lipi ufanye na lipi usifanye na kwa wakati gani!
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu ni mtu mzima, si mtoto. Lazima ujue kuwa unawajibika kwa kila unaloamua na kutenda. Amua kuwajibika vizuri. Fikiri kabla ya kutenda, changanua lipi ni lipi kabla ya kufanya uamuzi wa kile unachotaka kufanya. Wakati wote uongozwe na busara na hekima na siyo jazba na ushabiki wa matakwa ya kundi. Kama ni jema fanya na kama si jema usifanye. Kwanza tambua wewe ni nani na uko hapa kwa ajili gani. Lazima ujue kuwa hatma ya yote uko peke yako. Utafaulu au kufeli wewe. Utapata shahada wewe na si mtu mwingine. Hakuna ubia wa kufaulu au kufeli au kiwango cha kufaulu. It will always remain personal. Katika masomo unanufaika wewe. Shirikiana na wengi lakini usisahau kujali maslahi yako. Maslahi ya wengi yasiyojumuisha yako, yahoji vizuri kabla ya kuamua kushiriki au kufanya. Vinginevyo labda kama umeamua kujitoa muhanga, uwe shujaa. Hata kwa hilo, sijui utakuwa shujaa wa nani.
Mabibi na Mabwana;
Kabla ya kumaliza napenda kutambua na kumshukuru Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa na viongozi wa MDF kwa juhudi zao za pamoja zilizowezesha Chuo hiki kuwepo. Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru wananchi wanaokizunguka Chuo kwa ujirani mwema na wakazi wa Morogoro kwa ujumla kwa kukipokea vizuri na kuishi na wanajumuiya wa Chuo hiki kwa upendo mkubwa. Naomba muendelee na moyo na ushirikiano huo.
Baada ya kusema hayo, nawashukuru sana kwa kunialika. Nawatakia kila la heri na mafanikio tele.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.

Saturday, 13 April 2013
Majibu yangu kwa Mhariri wa gazeti la Raia Mwema-Joseph Mihangwa
Habari ndugu JOSEPH MIHANGWA?Mimi ni miongoni mwa wadau wakubwa wa
makala zako katika gazeti la RAIA MWEMA zinazoitwa NASAHA ZA MIHANGWA.Katika
nakala ya gazeti hili ya tarehe 03/04/2013 uliandika mada iliyokwenda kwa jina
la MAHAKAMA YA KADHI NA UZANDIKI WA WANASIA UCHARA.Kuna hoja kadha ambazo
ulijaribu kuzizungumzia katika makala hii kama ifutavyo;
i)Mahakama ya
kadhi na ofisi ya kadhi kugharamiwa na serikali
ii)Mahakama zetu
zimepewa uwezo wa kusikiliza kesi na kuamua kwa haki bila ubaguzi
iii)Kuruhusiwa kwa
misingi ya kidinikatika jamiiya kawaida hupelekea mifarakano na mitafaruku
inayoweza kutishia ustawi wa
jamii.
iv)Madai ya kidini
huwa na ajenda ya siriukafananisha na chui ndani ya ngozi ya kondoo na ukatoa
mafano yale yaliyotokea Algeria
na India.
v)Je taasisi hiyo
haitaenda kudai mfumo mpya wa kidini kuhusu elimu,sayansi,
technolojia,mabenki,bima na uhusiano wa kimataifa ili kukidhi matakwa ya
sehemu moja ya jamii kwa misingi ya dini?
Kimsingi yapo mengi uliyoyazungumzia kwenye makala yako na kuyatolea
ufafanuzi lakini hayo ni machache mbayo nimeona kuyatolea maelezo ili nijaribu
kukufanulia na pengine utaweza kunielewa na kupata ufahamu mpana juu ya
mahakama ya kadhi.Vilevile uweze kuandika vizuri juu ya hili kwa mustakabali wa
taifa na watu wake.
Kwahiyo kila namba ya hoja hapo juu itawakilishwa na maelezo
ya namba hiyohiyo hapa chini;
i)Kuhusu
serikali kugharamia shughuli za kadhi na ofisi yake-Ni kwamba serikali
kugharamia shughuli za kidini hapa nchini si mara ya kwanza wala si jambo la
kushangaza ila inawezekana likawa la ajabu na la kushangaza kwa
WAISLAMU,Kwasababu ni aghalabu sana kwa serikali kufanya hivyo.Unakumbuka mwaka
1992 serikali ilipo iingia mkataba na taasisi za kidini yaani TEC na
CCT?Mkataba uliokenda kwa jina la MEMORANDUM OF UNDERSTANDING (MOU). Katika
mkataba huo serikali inawajibika kugharamia huduma za jamii za WAIKRISTO kama
vile shule za seminary na hopsitali za waikristo.Gharama zinazotolewa na
serikali ni za mishahara kwa wafanya kazi, marekebisho ya taasisi hizo na mambo
mengine yote ambayo yanahitajika gharama ya fedha .
Kwahiyo
kuhusu gharama ya uendeshaji wa ofisi ya kadhi ni wajibu wa serikali na si
swala la ajabu hapa nchini kwetu.
ii)Kuhusu uwezo
wa mahakama za serikali kusikiliza kesi na kuamua kwa haki bila ya ubaguzi-ni
kweli kwamba mahakama zetu zimepewa uwezo wa kusikiliza kesi na kuamua kwa haki
lakini nadhani umeshindwa kuelewa vizuri kuhusu mahakama ya kadhi , yenyewe
inashughulika ndoa,talaka,mirathi na mahusiano baina ya waislamu wala haingilii
watu wasiokua waislamu na haihusiki na kesi zilizonje ya hizo.
Hivyo basi
kwakua serikali inaruhusu watu wake kufunga ndoa kufuatana na misingi ya dini
zao basi haina budi kuwaachia raia wake uhuru wa kuendesha taratibu za ndoa zao
kufuatana na misingi ya dini yao, kwasababu haiezekani ndoa ifungwe msikitini
chini ya Shekhe alafu matatizo yanayohusu ndoa yakitokea yakashughulikiwe
kwenye Mahakama za serikali ,badala yake matatizo yote yanayohusiana na
ndoa,talaka na mirathi kwa waislamu yashughulikiwe na Kadhi.
Zipo baadhi
ya nchi ambazo zina mahakama za serikali na zina uwezo wa kuendesha na
kusikiliza kesi na nyengine zina idadi ndogo za waislamu lakini bado zimewapa
waislamu uhuru wa kuwa na mahakama ya kadhi, Kwamfano;
*Kenya katika
katiba yao ibara ya 66(3) wanaruhusu mahakama ya kadhi
*Uganada ambayo
ina 12% ya waislamu lakini katika katiba yao ibara ya 129 inaruhusu mahakama ya
kadhi
*Gambia katika
katiba yao ya pili (1997) ibara ya 120(b) inaruhusu mahakama ya kadhi
*Nigeria katika
katiba yao(Federal republic of Nigeria 1999) ibara ya 262(2) na 277 inaruhusu
kadhi
Sasa hizo ni
baadhi ya nchi za kiafrika ambazo pamoja na ubora wa mahakama zake lakini zimewapa
uhuru waislamu wa kufuta sheria zake katika maswala ya ndoa,talaka, na mirathi
.Itakua Tanzani ambayo mahakama zetu zina mlundikano wa kesi na maamuzi
yasiyosthili yanayowafanya watu wasionacho ndio wahukumiwe kwa kukosa lakini
mafisadi wanaoiba mabilion ya ya fedha kuishia mtaani kwa kushinda kesi je ni
kweli mahakama zetu zina uwezo wa kuendesha kesi?
iii)Kuhusu
mifarakano na mitafaruku inayotokana na kuanzishwa kwa misingi ya kidini -Ni
kwamba matatizo hayo hayatokani tu kutokana na kuanzishwa na kwa mahakama ya
kadhi bali hutokana na matatizo mengi yanayowakabili wananchi katika jamii zetu
kwamfano halingumu ya maisha,matabaka kati ya walionacho na wasionacho,ukosefu
wa ajira na mengine mengi,ndiyo yanayochochea wananchi kupamabana na tabaka
tawala.
Lakini pia viongozi wa dini husababisha mifarakano katika
jamii na mauaji kwa mfano ;Mauji ya kimbari nchini Rwanda ,waliokamatwa kwa
kiasi kikubwa ni Maaskofu na wachungaji ambao ndio wachochezi wa kuu wa mauaji
hayo.Walikua wakitangaza makanisani kuwa wanaostahili kuongoza ni WATUSI na si
WAHUTU,hali hiyo ilipelekea wahutu wakikimbilia makanisani kuuwawa na hivyo
hukimbilia Misikitini kama sehemu yao ya amani.
Vilevile
umezungumzia kuhusu vita vya BIAFRA vya mwaka 1967,lakini kumbuka si tu
mifarakano ya kidini ndio yaliyopelekea vita hivyo bali hata kauli za baadhi ya
viongozi wa Afrika zilizokua zikichochea Kujitenga kwa taifa hilo zilipelekea
vita hivyo kwamfano;Mwl. Nyerere alikuwa akichochea kujitenga kwa taifa
hilo.Haya yalisemwa na Jenerali Ulimwengu katika kipindi cha Malumbano ya hoja.
iv)Kuhusu madai ya
kidini kuwa na ajenda ya siri-Ni kwamba katika madai haya ya mahakama ya kadhi
sisi waislamu wa Tanzania sio wa kwanza kudai bali zipo nchi nyingi ambazo
zilianza kudai na kufanikisha kupata mahitaji hayo kama nilivyo kuonsha hapo juu.Na
katika nchi za jirani yani Kenya na Uganda huu mfumo wa mahakama wanao na ni
zaidi ya miaka 15 na haijawahi kutokea hata siku moja vurugu zilizosababishwa
na uanzishwaji wa mahakama hiyo na wala ajenda yoyote ya siri ambayo
imeziathiri nchi hiyo kutokana na mahakama ya kadhi. na badala yake ni amani na
utulivu katika uendeshaji wa mahakama hiyo.
Kwa hiyo sisi
waislmu wa Tanzania hatuna ajenda yayate ya siri kwa serikali wala taifa hili
juu ya uanzishwaji wa mahakama ya kadhi ,isipokua tunataka haki yetu ya msingi
katika mirathi ,ndoa na talaka.Mbona Tanzani ni miongoni mwa nchi mbili barani
Afrika ambazo zina ubalozi wa Vatikan ?
Lakini nchi nyingi za kiafrika hazina ubalozi huo na
waislamu wa nchi hii hatujalalamika kuwa uwepo wake ni ajenda ya siri ya KANISA
KATOLIKI?
v)Hatuna haja ya
kwenda kudai mfumo mpya wa kidini kuhusu elimu,sayansi,teknolojia na mengine
ambayo umeyasema kwa sababu;
ELIMU-Tunazo
shule zetu za msingi na za sekondari ambazo zinatoa elimu kulingana na mfumo wa
kiislamu,sio nyingi kama za kwenu lakini hizohizo chache tunazo kwa mfano;Shule
ya sekondari ya kiislamu Ubungo,Shule ya sekondari ya kiislamu
Kirinjiko,Luqmani,Ridhwaa,Kinondnoni,ununio pamoja na nyengine nyingi.Vile vile
tunacho Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro ambacho kinatoa elimu kwa misingi ya
kiislamu,vyote ni vyombo muhimu katika
kutoa elimu kwa vijana wetu kwa mfumo wa kiislamu,pia zipo taasisi nyingi za
elimu ambazo zinashughulika na mfumo wa elimu ya kiislamu na elimu ya kawaida.
MABENKI NA
BIMA-Pia tunazo taasisi zetu za fedha ambazo zinatoa huduma kwa misingi ya
kiislamu.Kwamfano;
Amana Bank pamoja na benki nyengine za kawaida ambazo zina
mfumo wa kiislamu katika baadhi ya huduma zake kwa mfano;Stanbik Bank na
Natinal microfiance Bank(NMB).
SAYANSI NA
TEKNOLOJIA-Pia tuna taasisi za teknolojia kama Redio za kislamu mfano;Radio
Imani,Kheri,Sauti ya kuran na Tv Imani pamoja na nyengine nyingi zinazochangia
kwa kiasi kikubwa katika kuwaelimisha waislamu.Zipo pia Hospitali kama nile
Aljumaa Hospital ya Daresalama(Karoakoo)na Ahmaddiya Hospital ya Morogoro na
nyengine zikuzitaja ambazo hutoa huduma ya afya kwa waislamu na wasiokua
waislamu kwa taratibu na mfumo wa dini yetu
Katika mwezi wa
03 mwaka huu ,Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dr. Jakaya Mrisho
Kikwete alifanya ziara katika Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro ambapo alifungua
jengo la sayansi na ujenzi wa jengo jipya la Teknolojia ya habari (ICT) ambalo
litakapokamilika litashughulikia utoaji wa teknolojia ya habari kwa waislamu
hapa nchini.
Hivyo
hatuna sababu ya kiuanzisha mfumo mpya kuhusu hizo sekta ulizozitaja isipokua
tunachangamoto ya kuziendeleza ili tuweze kukabiliana na changamoto za waislamu
katika nchi hii pamoja na kutopata msaada kutoka serikaini lakini taratibu
ishallah tutafika tunapodhamiria kufika.
Tulichokikosa sisi waislamu wa nchi ni uhuru wa
kushughulikia wenyewe kesi zetu zinazohusu ndoa,talaka na mirathi kwa misingi
ya uislamu.
Hivyo mi nadhani ungetumia muda
wako mwingi katika kuyazungumzia matatizo ambayo watanzania yanawapata katika
nchi hii.Kama vile unongozi mbaya,rushwa,maradhi,umasikini uliokithiri,ubovu wa
miundombinu yetu,tatizo la ajira,huduma mbovu za afya na kufeli kwa wanafunzi
wetu.Na mengineyo mengi amabyo ungewagusa watanzania moja kwa moja ,na sio
kuanza kuponda mahitaji ya dini za wenzio kwani yatakupelekea kudharaulika na
watu na kuonekana kama mchochezi wa vurugu za vurugu za kidini kwasababu tayari
swala la mahakama ya kadhi lishakubaliwa na serikali kwani ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya
chama cha mapinduzi ,na lipo katika hatua ya awali ya utekelezaji.
Katiba izingatie maisha halisi ya mtanzania
Hivi karibuni kumekua na mjadala mzito katika taifa letu unaohusu mchakato wa katiba mpya, sasa kinachoendelea ni uchaguzi wa mabaraza ya kata na wilaya lakini swalhivia la kumshukuru Mungu ni kwamba mchakato unaendelea vizuri japokua kasoro kadhaa zimeanza kujitokeza na hii ni kwa sababu penye jambo la watu wengi hapakosi kupishana juu ya mitazamo,siasa,itikadi na hata falsafa.
Katika makala hii ninachotaka kuwakumbusha ndugu zangu watanzania ni kuhusu mambo ya msingi ambayo mimi nadhani yanasahaulika katika mchakato huu,watanzania tumekua tukibeba hoja za wanasiasa na kuzifanya za kitaifa kwamfano; kupunguza mamlaka ya Rais na kuwa na tume huru, hizi ni hoja ambazo mi nadhani wakuzisimamia ni wanasiasa wenyewe lakini sisi ndio tunaozisimamia kidete.
Katiba ieleze masikini ambaye hana kipato atapataje huduma zake za msingi kama chakula,malazi na mavazi lakini sisi tumekalia kupunguzwa madaraka ya raisi alafu?Raisi awe yoyote laikini katiba izingatie maisha ya mtanzania wa kawaida na sio tu tume huru ya uchaguzi
Huu ni mtazamo wangu naruhusu maoni kwa wanaotaka kuchangia,kupinga au kukubali nilichokizungumza.

Kuhusu bajeti ya serikali ya Tanzania
Tunahitaji bunge la bajeti lijadili hoja na kuzipitisha kwa kufuatana na mahitaji ya wa Tanzania ya leo.